Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Ndugu yangu Mnyika kaza buti endelea na harakati zako za kuwakomboa Wanyonge hadi kieleweke. juhudi zako unazozifanya bungeni tunaziona, na manyanyaso unayoyapata tunayaona. tunakupa pole sana. achana na hao akina Ridhwani kwani yeye ni msanii kama baba yake. pia Nape hana lolote. badala ya kuzijibu hoja na kutekeleza yale aliyowahidi Wananchi anakazana kulumbana na CHADEMA. Kwa vile viongozi wote wa CCM wameshindwa kazi na hawajui la kufanya ndo maana wanaparamia hata majabali. Achana nao.
 
kwa kweli mheshimiwa mnyika wewe ni kichwa , haupaswi hata kuendelea na shule kwani ni vema wakutunuku tu Doctrate kwani uwezo wako ni mkubwa muno; hao wanaoongea hvyo ni kwa sababu tu wanajiuliza mbona uwezo wako mkubwa sana ukizngatia ni bado kijana mdogo sana, achana nao watajibeba 2015 sisi tumewachoka hasa huyu jamaa anae itwa nape jamani mwenzenu personally simpendii kupindukia.

waulize hao wenye ma phd wamefanya nini wambie elimu cyo cheti ni uwezo kichwani, mbona waliowengi hatareport zao wanatengenezewa tuu? angalia mfano kawambwa ni Doctrate lakini mutathimin amefanya nn kpndi chote hki zaid ya kupotezea malengo wanafunzi wetu tu, jamani ccm hatuwapendi muelelewe hilo tumewachoka jamaniiiiiiiiiiiii

mwisho; mnyika wewe ni kichwa na utazd kuwa kichwa zaidi ya hapo. be blased na mungu akuongoze. Amina
 
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM. Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.Kwa mara nyingine tena zinafanyika jitihada za kuhamisha wananchi kwenye mjadala kwa kumshambulia mtoa hoja badala ya hoja, sasa ili turejee kwenye mijadala ya msingi ni muhimu niweke kumbukumbu sawa kuhusu masuala kadhaa kama yalivyoombwa.Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam). Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne; nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa. Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tambaza kwa sababu nilitaka kusoma huku nikiendelea na harakati ambazo nilizianza kabla.Hapa ndio ilikuwa chanzo cha mimi kuingia kwenye kazi ya kuhamasisha mabadiliko kwenye mimbari nje ya utumishi wa madhabahuni. Tukio lililobadili mwelekeo wa maisha yangu, mwaka 1998 nikiwa kidato cha nne; nimesoma na tumeanza mitihani tukatangaziwa kwamba mitahani yote imefutwa baada ya kuvujishwa.Tukarudishwa nyumbani kipindi hicho nikaenda kwenye mafungo kujitafakari kwenye mkoa mmoja nikarejea Dar es Salaam nikakutana na wanaharakati kadhaa wa asasi zisizo za kiserikali; maelezo kuhusu ufisadi yalinifanya nione nina wajibu kwa nchi yangu, nikarejea Seminarini kufanya mitihani nikiwa na fikra tofauti.Matokeo yakatoka nimefanya vizuri, kwa mifumo yetu mibovu ya wakati huo kwa mara ya pili tena Serikali hii inayoongozwa na CCM haikutambua vipaji na nikapaswa niendelee kujilipia ada mwenyewe kama ilivyokuwa kwa ngazi nyingine za elimu zilizotangulia; hapa nikakata shauri kwamba nitatumia uwezo na uadilifu wote ambao Mwenyezi Mungu amenijalia kuwezesha mabadiliko katika taifa letu.Nikaamua kuacha kwenda kwenye shule za bweni mikoani na kubaki Dar es salaam nisome Tambaza huku nikiendelea na kazi za harakati; wakati huo nikihamasisha masuala ya ukombozi wa vijana nchini. Pamoja na kusoma kutwa huku nikifanya kazi nilipata daraja la pili katika kidato cha sita. Taasisi nilizoanzisha au nilizoongoza katika kipindi hicho na kazi nilizofanya sio siri na zinapaswa kujieleza zenyewe kwa matendo badala ya maneno. Katika kipindi hicho, wakati huo kukiwa hakuna Mfuko wa Elimu wala Bodi ya Mikopo nikashiriki katika ushawishi wa mabadiliko ya kimfumo; nilikwenda Dodoma, tukakutana na wabunge na mawaziri nikawasilisha mada “Towards a more functional education in Tanzania”, wakati huo nikiwa mwanafunzi wa Sekondari.Kati ya wabunge waliosikiliza mada niliyoiwaisilisha wakati huo sasa ni Rais Jakaya Kikwete ( Ridhwan ukiwa nyumbani unaweza kumwuliza maoni yake aliyotoa siku hiyo kuhusu ugharamiaji wa elimu na suala la mauaji ya mwanafunzi wa Iyunga Michael Sikupya). Nilipotoka kwenye mkutano ule Dodoma mwishoni wa miaka ya tisini, nilikata shauri kwamba mwaka 2005 nitagombea Ubunge hii ni baada ya kushudia aina ya wabunge waliokuwepo. Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam kusomea “Bachelor in Business Administration (BBA) kwenye programu ya jioni; nilifanya hivyo kwa kuamua kwa kuwa nilitaka nisome huku nikiendelea na kazi. Mkuu wa Programu hiyo wakati huo alishangaa sana kwa umri wangu (wakati huo shahada hiyo walikuwa wakisoma wazee watu wazima wafanyakazi) na matokeo yangu (kwa kuwa yaliniruhusu kwenda kuingia kusoma katika mfumo wa kawaida). Nikamweleza akanielewa kwamba sitaki kusoma kama wanachuo wengine wa kawaida, uamuzi wangu huo ulikuwa na gharama kwa kuwatafsiri yake ni kuwa nilipaswa kujisomesha binafsi. Kwa hiyo mimi ni kati ya wale ambao hatudaiwi na nchi hii kwa maana ya kwamba sijawahi kuchukua ruzuku wala kusomeshwa na Serikali hii inayoongozwa na CCM; nimesoma kwa jasho la wazazi wangu na langu binafsi. Kwa hiyo, nijibu tu kuhusu elimu yangu ya juu kwamba nimesoma miaka mitatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (mtu aliyosoma kwa kiwango hicho kwenye baadhi ya vyuo duniani hupewa associate degree). Mwaka 2004 ikaanza misukosuko mbalimbali, mwaka huo ulikuwa ndio unatungwa muswada wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, haya matatizo yanayotokea leo niliyatabiri wakati huo. Niliwasilisha mada kwa wanachuo kwenye ukumbi wa Nkurumah kuchambua udhaifu wa muswada huo na kupata maoni ya wanafunzi kuhusu marekebisho yanayohitajika; wanachuo wakapitisha azimio la kwamba muswada huo upingwe.Kesho yake nikiwa Morogoro kikazi kukafanyika mgomo hatimaye wanafunzi wakapigwa na kukamatwa.Nakumbuka nilikatiza kazi niliyokuwa nafanya nikarejea kwa kuwa Chuo kiliweka sharti kwamba lazima wanachuo waache mgomo ndio waliokamatwa waachiwe. Wakati huo Serikali ya wanafunzi ilikuwa haisikilizwi, mimi na wengine wachache tukajitolea kuzunguka kampasi na hosteli zote kushawishi wanafunzi kurejea masomoni na wakafanya hivyo.Serikali ya CCM ikatoa maelekezo kwamba kama tumeweza kuwafanya wanafunzi warudi, hata kama sikushiriki mgomo na sihusiki na masuala ya mikopo kwa kuwa ni mwanafunzi ninayejilipia mwenyewe lazima nisimamishwe; nikiwa mwanafunzi pekee wa BBA niliyesimamishwa wakati huo.Nikarejea baada ya muda tayari kukiwa na mvutano kati yangu na utawala, mwaka 2005 nikaamua kugombea Ubunge wakati huo nikiwa mwanafunzi; mvutano ukaongezeka zaidi. Na utawala wa Chuo ukawa unapata mashinikizo mengi kutoka kwa Serikali na CCM; wengine wakipendekeza nifukuzwe, wengine nifelishwe na wengine nisiruhusiwe kuingia katika maeneo ya Chuo jioni masomoni kwa kuwa nitakuwa nafanya kampeni.Nikawa katika mtanziko(dilemma) wa kuchagua ama kuendelea na masomo na kujitoa au kupunguza nguvu kwenye kampeni (mbinu nyingi zilitumika wakati huo, sio sehemu ya majibu yangu ya leo) au niendelee na kampeni. Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki.Mwaka 2006 nikiwa Marekani nilitafakari sana na kufikia uamuzi wa kuendelea na kazi hii ya kusimamia mabadiliko na kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2010. Mwaka 2010 niligombea tena na kushinda wakati huo huo nikiongoza kazi za kitaifa za kampeni makao makuu pamoja na Profesa Baregu na wengine; hakuna mahali popote nilipowadanganya wananchi kuhusu elimu yangu, kama nilivyoeleza hapo juu. Naamini wananchi wa Jimbo la Ubungo walinichagua kwa uwezo na uadilifu wangu, na walijua pia kwamba nilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mitatu. Naamini elimu ni kitu muhimu sana kwa kiongozi, lakini wapo wenye elimu kubwa ya vyeti lakini hawajaelimika na wapo wenye elimu ndogo sana ya vyeti lakini wanaelewa mkubwa wa kutimiza majukumu yao ya uongozi. Tangu mwaka 2012 na 2013, nimekuwa kwenye mtanziko mwingine na viongozi wangu ndani ya chama wanafahamu; niliomba kuachia majukumu mengine yote katika chama ili nibaki na ubunge peke yake niweze kuwatumikia wananchi wakati huo huo niendelee na masomo zaidi ya elimu ya juu katika fani inayoendana na kazi ninayoifanya ya sasa na matarajio yangu ya baadaye.Hata hivyo, kwa mwelekeo huu wa Serikali na CCM leo nieleze tu kwamba nikifanya hivyo itakuwa faida zaidi kwa watawala tunapoelekea mwaka 2015; hivyo, nimeamua kama nilivyoamua mwaka 2005; kwamba nitarejea masomoni baada ya CCM kuondoka madarakani na Tanzania kupata Serikali mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho.Wakili Ridhwan katika maandiko yake amefanya rejea ya suala Kihiyo wa CCM Temeke, nashauri arejee kwenye hukumu ya kesi ile na marekebisho ya sheria yaliyofanywa na Serikali yaCCM kuwalinda wabunge wake vihiyo baada ya hukumu. Mifano hailingani kwa sababu mimi sijatoa maelezo ya uongo popote. Lakini hata kwa wabunge wa CCM wanaotoa maelezo ya uongo wa wapiga kura, marekebisho hayo yamewawekea wigo wa mianya yakutokea mahakamani. Zamani fomu zakuogembea zilikuwa na mahali pa kujaza elimu ya mgombea, sasa kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo, suala la kughushi na kutoa taarifa za uongo haliko kama ilivyokuwa awali, isipokuwa kesi inaweza kufunguliwa ya ukiukwaji wa kawaida wataratibu za kampeni kwa kuwashawishi wapiga kura kwa taarifa za uongo (ndani ya ule muda wa kisheria wa kesi kufunguliwa ambao ulishapita). Halafu ni jukumu la mlalamikaji sio tu kuthibitisha kwamba uongo ulitolewa bali uongo umeathiri vipi matokeo. Ndio maana leo kuna vihiyo wengi tu wa CCM ndani ya Bunge lakini ni vigumu kuwabana kwa mfumo wetu wa sasa. Baada ya majibu hayo marefu, naamini sasa Nape unaweza sasa kurejea kwenye kujibu; Elimu ya Mnyika ina uhusiano gani na CCM kuahidi kwenye ilani yake na kushindwa kutekeleza kwamba ifikapo mwaka 2010 asilimia 90 ya wananchi wa mijini ikiwemo Dar essalaam watakuwa wanapata maji safi na salama? Ridhwan kwa kuwa umeweza kufanya rejea unaweza pia kueleza ni kwanini Rais Kikwete mwaka 2011 aliahidi kuwa tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa historia mwezi Februari 2013 lakini mwezi huo umefika na matatizo bado ni makubwa?JJ
You got good head John, uwezo wako katika kujenga hoja na kutetea wananchi wa Ubungo na Taifa kwa ujumla ni wa zaidi ya mwanasiasa, baadhi yetu hatukuwa na wasiwasi na elimu yako, bali tulikuwa na uhakika wa hoja zako 'cause we knew you since high school and we' re still appreciate ur efforts. Taifa hili linahitaji vijana wenye mitazamo chanya ya kimaendeleo kama unayoionyesha.
 
[h=5]Nimeitoa FB Myika njoo, najua wewe high class huendagi FB nimekuletea huku, nawe weka chako tumkome nyani usoni.....(mood tafadhali sana usiunganishe thread hii, pls pls)[/h]

Like · · Follow Post · 3 hours ago via BlackBerry





 
nimekusoma mkuu! we ni jembe la kizazi hiki hata hao wanaolopoka upuuzi wanalifahamu hilo. endelea kuwabuluza hao vilaza wa li chama la kijani.
 
[h=5]Nimeitoa FB Myika njoo, najua wewe high class huendagi FB nimekuletea huku, nawe weka chako tumkome nyani usoni.....(mood tafadhali sana usiunganishe thread hii, pls pls)[/h]

Like · · Follow Post · 3 hours ago via BlackBerry






Vyeti vya mzumbe bwana mbona viongozi wote wachakachuzi wa elimu ni wanakimbilia kusema wamesoma Mzumbe refer Kamala,Nchimbi,Mama Makinda,na huyu Nape Elimu zao hazilingani na uwezo wao wanauwezo mdogo mno wa kujenga hoja,na wasiwasi na elimu hizo.
 
Nimeitoa FB Myika njoo, najua wewe high class huendagi FB nimekuletea huku, nawe weka chako tumkome nyani usoni.....(mood tafadhali sana usiunganishe thread hii, pls pls)



Like · · Follow Post · 3 hours ago via BlackBerry


John Mnyika alipita masomo ya jioni hakumaliza hana cheti!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mnyika huwa anamwendesha mwanasheria mkuu wa serikali, utafikiri kahitimu sheria harvard, kweli serikali ya CCM ina vihiyo wengi! Wana taarifa za uongo za kusoma lakini hawajawahi kusoma! Matukio aliyoyataja Mnyika waliokuwa UDSM 2004 watakubumbuka alivyotutetea na alivyotushawishi kusitisha mgomo turudi madarasani, lakini still serikali ya CCM ikatufukuza! Nakwakuwa alikuwa si mwanafunzi wa kampasi sidhani kama kuna mtu alijua kuwa msaada aliotusaidia ulimgharimu yeye asimalize elimu yake na ukampa misukosuko mikubwa kiasi hicho! Huu upendo alionao kwa wengine ni mkubwa kiasi cha kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine! Mungu ambariki!

Kama kumaliza kidato cha sita ni kusoma sawa ila huyo mbunge wenu mtamkweza lakini ukweli ndio huo hana cheti; kweli upate A tisa O level ushindwe kusema kutoa matokeo yako ya kidato cha 6 zaidi ya kusema kapata div 2; na aweke tuone kama div 2 hakupata kutokana na B ya Bible knowledge; huyo mtuuuupuuuu kashindwa kusoma hata BBA tena masomo ya jioni msitake kututia kichefuchefu!
 
nikusaidie kidogo, Mh. mbunge hataki majibizano yasiyo na msingi hivyo kaamua kuwaeka kila kitu ili msiendelee kuuliza maswali, atakae uliza tena hapo basi huyo ni mbulula.

Hana cha kujibizana hana cheti hakumaliza chuo tena masomo ya jioni; lol!!!
 
Na kwa akili yako yote, untendaji wa Mnyika bungeni - hasa ujengaji wa hoja zake - unafanana na huyo yarabi salama 'mzaa mtihani?

Pili, kuhusu Mnyika kutoenda kusoma Ilboru na baadaye kusoma evening class; ungesoma majibu yake vizuri, maana kaeleza kila kitu.

Tanzania tuna tatizo moja kubwa, ambalo linajitokeza sana hapa JF, tunataka tutafuniwe kila kitu na hata ikiwezekana tulishwe! Mnyika amendika in great details safari nzima ya elimu yake, mikanganyo, na hata dilema ambazo amekuwa nazo na ultimately maamuzi yake. Lakini kwa bahati mbaya bado kuna watu hawaelewi!

Hebu tushughulishe bongo zetu kidogo!

Hapa hatuzungumzii ya bungeni tunajadili mtu aliyepata A Olevel lakini anaficha majibu yake kidato cha 6; hivi div2 ya kidato iliyotokana na Bible knowledge unaweza kujigamba nayo?
 
Kwa walio wahi kupita shule (sekodari) wanaelewa inahitaji uwezo wa juu kiasi gani kupata A 9. Hii ni zaidi ya kipaji maalumu. Nachelea kusema mheshimiwa Mnyika ndiye Mbunge Pekee katika bunge la sasa aliyefaulu sekoari kuliko wote

A tisa za kusaka mitaani? Watu wanaopata A O level kidato sita wanapiga A za kumwaga hebu tusaidieni hiyo div 2 aliyopata form 6 iwekeni matokeo yake tuone kama haitakuwa kichekesho
 
Kama kumaliza kidato cha sita ni kusoma sawa ila huyo mbunge wenu mtamkweza lakini ukweli ndio huo hana cheti; kweli upate A tisa O level ushindwe kusema kutoa matokeo yako ya kidato cha 6 zaidi ya kusema kapata div 2; na aweke tuone kama div 2 hakupata kutokana na B ya Bible knowledge; huyo mtuuuupuuuu kashindwa kusoma hata BBA tena masomo ya jioni msitake kututia kichefuchefu!

Aliye kwambia kusoma ni kuelimika ni nani wangapi wamesoma lakini hawana uwezo wa kupambanua mambo mfano huyo Nape mwenye elimu ya kuungaunga na asinge kuwa mtoto wa kiongozi kama mnyika hata hapo asinge fika mkuu.
 
Kwanza nianze kwa kuwashukuru Wakili Ridhiwan na Mh. Nape kwa kuibua hoja kuhusu Elimu ya Mh. Mbunge Mnyika kitu ambacho binafsi nilikuwa sikui na nilikuwa najiuliza sana Hivi Mnyika anaelimu gani hasa nikizingatia uwezo wake wa kuhoji( Reasoning capacity) Kitu ambacho naamini kwa watu ambao kweli wanamfahamu au kumuona tu bungeni inatosha kukubaliana nami kuwa Mh. Mnyika ni zaidi ya mbunge wa Ubungo kwani anawakilisha kwa maana halisi, na wala huhitaji kuhoji zaidi kuhusu elimu yake.

Pili, nirudi kwenu wakili Ridhiwan na Mh. Nape hivi kweli nanyi ni watanzania na wazalendo wakweli au mamluki? Badala ya kuhoji kuhusu elimu na uwezo wa wabunge na mawaziri ambao wapowapo tu kama hawapo kwani katika wizara zao maendeleo yamepigwa sindano za ganzi mf. Wizara ya Elimu kufelisha zaidi ya theluthi mbili yaani div. IV na 0 huyu ndio tujiulize alikuwa akifanyanini na vyeti alivyonavyo anaweza kuvitafsiri kuwa matendo? Kwani Matokeo ya mwaka jana yalitosha kumfanya afanye kitu ambacho kingefanya matokeo ya mwaka huu yasiwe hivi yalivyo. Lakini kwakuwa wengi wao huishia kusinzia tu wawapo ofisini, semina za msingi kabisa na bungeni, haya ndio matokeo yake.


Tatu, jiulizeni hata nahodha mwenyewe, vipi G.P.A yake, reasonable decision making etc? Kama rubani unapoona mambo yanaenda mrama, au unabaharia asiejua kuogelea vizuri mweche ajifunze kuogelea kwanza ndipo uambatane nae. Vipi majibu rahisi kiasi hiki kwa maswali magumu? Mfn waziri anasema sababu kubwa za kufeli kwa wanafunzi ni Kwanza uhaba wa walimu, pili ukosefu wa maabara na maktaba n.k. Kitu ambacho sikweli mfano Kuna shule zina kila kitu kinachotakiwa Mfano Korogwe girls ina maktaba nzuri, maabara, walimu wakutosha na idadi ndogo ya wanafunzi lakini bado wana div I-0, div II- 5, div III- 4, div IV-19 na fld 25 kwa darasa lenye wanafunzi 54 hapa napo kuna upungufu huo aliousema Mh. waziri Kawambwa? Anasahau kuwa alichagua wanafunzi ambao aliwaongezea alama kubwa tu katika ufaulu wao kujiunga kidato cha kwanza na wengi wao hawajui hata kuandika majina yao.
Lakini pia mtihani wao ni wa kuchagua jibu hata hesabu washafanyiwa wao wanachagua jibu sahihi tu.

Nne, nami pia sasa najiuliza kwanini Elimu ya Tanzania isiingie kwenye maajabu ya dunia? Mwanafunzi anaefeli anaongezewa alama iliafaulu, mathalani mwanafunzi asiejua kuandika hata jina lake anafaulu mfn. darasa la saba na kadato cha pili.

Mwisho, Najiuliza hivi ni usomi wa namna gani huu ambao hadi msomi mwenye Phd kama Mh. Kawambwa hajui umuhimu na heshima ya kujiudhuru?
Niseme tu katika nchi yetu kuna vitu vingi vyenye maslahi kwa taifa vinavyotakiwa kuhojiwa nikianza na uzalendo na utendaji wa baadhi ya viongozi wetu na vitu wanavyovifanya, mauaji yanayoongezeka hasa yanayohusisha imani, Na kubwa kabisa ni ufisadi usiomithilika likini bado nahodha anawachekea tofauti na enzi za mwl. Nyerere. Hojini hivi basi kwakuwa nyinyi mpokaribu kabisa na wahusika.
 
nape na riz one shame on you mmejidhalilisha sana kwa kuparamia mwamba!
 
Mzumbe University ni kama Pombe ya Ngomani yeyote anaweza kwenda pale akajiregister, akaendelea na shughuli zake then baada ya miaka miwili anarudi kuvaa joho.
 
hongera kamanda mnyika kwa kuondoa wingu hili naamini watanzania wanatambua uwezo wako katika kusimamia mambo ya msingi na hili ni muhimu zaidi katika kipindi hiki cha harakati za kulikomboa taifa hili pia uwezo wako darasani ni elimu tosha kwa wengine wote waiokuja na hoja mfu ya elimu yako hongera sana kamanda tupo nawe hadi kieleweke.
 
Back
Top Bottom