Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Tatizo nape ndio anajisheuwa na na kimaster chake.ukweli ni kwamba mnyika anakipaji.
 
Hili suala tatizo sehemu nyingi linajadiliwa kwa muungo wa kishabiki wa Kisiasa bila ya kuangalia mantiki yenyewe. As much as kufaulu sana darasani ina ashiria 'brilliance' ya mtu; bado ukweli unabaki kuwa kuna watu ambao walikuwa hawawezi kabisa masomo ya darasani na matokeo yao ni average lakini kwenye utendaji ni wazuri huku wengine utendaji unaendana kabisa na ufaulu wao huo afifu. Na hali bado kuna wale ambao hufaulu sana darasani na utendaji ukawa mbovu ama ukawa mkubwa ukaendana kabisa na ufaulu huo.

Tukiacha hayo... Nape anafanya kazi nzuri sana aliyopewa aifanye CCM, achilia mbali kuwa siasa zake ni za taka. He is really good in 'Gutter Politics'. Na hali piya Mnyika anafanya kazi nzuri sana aliyopewa kufanya na Chadema achilia mbali kuwa aidha si mtaalam wa Siasa za Maji taka ama hajiusishi na siasa za maji taka kama Nape.

They are both Great at what they do... Swali linabaki hizo CV zinavyoendelea kuleta mlolongo wa majadiliano nani ana benefit siku ya mwisho? Mnyika/Nape/CCM/CDM ama Wananchi?
 
Elimu ya kuunga unga kama ya Nape ni lack of confidence ktk maisha. Nape na masters yake inamsaidia nini wakati yeye ni opportunistic, sawa na mwanamke anayetaka kuolewa akijua kwamba akiolewa tu shida zake zote zimeisha. Mnyika anajielewa na anafahamu anachokifanya
 
1. nimejifunza kuwa kama una elimu ya kuunga -unga kama yangu basi usithubutu hata siku moja kuhoji elimu ya mtu mwingine maana nitaumbuka, tena mbaya zaidi ukapotea njia na kuhoji ya mtu ambaye ni genius.

2. Si lazima ujilazimishe kuwa na degree, masters na hata PHD eti tu watu wakuone umesoma la hasha kinachotakiwa unajiuliza je masters au phd nayoitaka kusoma naihitaji kwa kazi zangu? na kama kichwani unajiona nina ujuvi sawa na hiyo degree kuna haja gani tena ya kukaa darasani kufundishwa vitu ambavyo unavijua na unavifanyika kazi?

3. Watu wenye upeo wa juu huwa hawakai na kuangalia elimu ya mtu mwingine ikoje bali wanachoangalia ni jinsi mtu huyu anavyo-deliver. (perfomance)

4. Watu wenye upeo mkubwa ki-akili hawana majivuno - kwa mafano hapa JF ukiuliza ni nani aliyepata point 7 ya A tisa o'level sidhani utapata hata wa tu 10. Lakini wengine ndiyo tumejua juzi tu kwamba kumbe mnyike si mtu wa kawaida kichwani, sasa inakuwa tofauti na mtu mwenye upeo mdogo lazima mtaa mzima mtamjua kwamba kamaliza chuo.
 
mhuu! katika karne hii jambo la elimu, zaidi sana kwetu sisi watanzania ni muhimu kuliona kwa uzito wake. hawa viongozi wetu wasijiridhishe na mafanikio ya kina bill gates na jobs. hao wapo! lakini waweza kuta ni mmoja kati ya milioni moja. viongozi wa watu, kwa maana ya kisiasa au kiserikali, wahakikishe wamepata elimu ya darasani ya kutosha. upeo wa hoja za mmyika zingeboreka zaidi kama elimu yake ingetimia.
 
Tunachotakiwa kufanya kama jamii inayomzunguka John Mnyika siyo kumzodoa na kumshambulia kwa matusi bali kumpa moyo na nguvu ili arudi shule na kumaliza degree yake ya kwanza.Nina uhakika kama hatafanyiwa hujuma na chuo kikuu John Myika anauwezo mkubwa wa kufaulu.

Ningemsihi sana mdogo wangu Mnyika pamoja na wito alionao wa kujenga Taifa lake bado bila elimu ya darasani inahitajika.Hata jioni aweza kujisomea na akamaliza degree yake.

Viongozi waChadema wanapaswa kumpunguzia kazi kijana wao ili amalize shule yake.Na siyo Mnyika tu vijana wote ambao hawajamaliza shule zao au walimaliza form four wakati ni huu wa kurudi shule na kuendelea na masomo yao.Elimu kwanza siasa baadaye.
we una kiwango gani cha elimu, kama una Masters Degree basi tuombe IQ test wewe na Mnyika ili tuhakikishe kwamba elimu lazima uwe na vyeti.
 
Tunachotakiwa kufanya kama jamii inayomzunguka John Mnyika siyo kumzodoa na kumshambulia kwa matusi bali kumpa moyo na nguvu ili arudi shule na kumaliza degree yake ya kwanza.Nina uhakika kama hatafanyiwa hujuma na chuo kikuu John Myika anauwezo mkubwa wa kufaulu.

Ningemsihi sana mdogo wangu Mnyika pamoja na wito alionao wa kujenga Taifa lake bado bila elimu ya darasani inahitajika.Hata jioni aweza kujisomea na akamaliza degree yake.

Viongozi waChadema wanapaswa kumpunguzia kazi kijana wao ili amalize shule yake.Na siyo Mnyika tu vijana wote ambao hawajamaliza shule zao au walimaliza form four wakati ni huu wa kurudi shule na kuendelea na masomo yao.Elimu kwanza siasa baadaye.

Watu wanasoma ili waelimike. Anayetakiwa kurudi shule ni Nape siyo Mnyika. Hapa wewe umebeba kasumba ya kukosa karatasi (cheti). Mimi sioni umuhimu wa karatasi kama hata ukiwa nalo na bado unaweza ukawa pumbalised.
 
Ame upo na mimi.Hata akijiunga na College yoyote ile as long as amemaliza degree yake.Uwezo anao na nia anayo.
Mnyika umeshapewa link ,punguza kazi zako nenda shule jamii yako bado inahitaji uende shule.
 
Kumekuwepo na mjadala mkubwa kwenye social medias kuhusiana na Elimu ya Katibu wa Uenezi wa CCM- NAPE MOSES NNAUYE na Mkurugenzi wa Uenezi wa CDM-JOHN MNYIKA.,mjadala ambao ni mpana na unazalisha maswali na hoja nyingi vichwani mwa watu.

Nikiwa naufuatilia kwa makini mjadala huo, nimeipitia maoni ya mmoja wa great thinkers kwa jina la mtanzania na ametoa ushauri ambao nadhani ni ushauri bora unaotoa mafunzo ya msingi katika kuzifanyia tathimini CV hizo za viongozi hao waandamizi wa vyama vikubwa vya siasa hapa nchi.

Hao watu wanaosemwa kwenye MTANZANIA hawafai kufananishwa na NAPE NNAUYE hata kidbuogo....
Yeah alijaribu kurudia mara mbile mtihani wa form four... lakini yeye alikuwa na GODFATHER na CCM-CULT nyuma yake

Wewe beba CHETI CHAKO CHA FORM FOUR DIVISION TWO Uombe Scholarship za kwenda INDIA utasikia Majibu yake

Please Misichanganye Machungwa na Machenza...
 
Hapa yapo mawazo ya msingi na michango yenye kulenga kujenga..,wapo ambao wanaona mfumo wa kuelekeza akili na kuthamini cheti si mfumo nzuri kuweza kupata mtu mwenye uwezo na kumtumia katika mikakati ya maendeleo ya jamii yetu.,lakini swali moja la msingi la kujiuliza ni kuwa kama si kwa cheti ni njia ipi ya mbadala ambayo tunaweza kupima na kujiridhisha kuwa mtu husika anaop uwezo wa kutosha wa kumudu majukumu na wajibu atakaopangiwa kwa kazi husika bila ya kuangalia na kufuatilia CV yake ya Kielimu (tukimaanisha Vyeti..)..?
 
1. nimejifunza kuwa kama una elimu ya kuunga -unga kama yangu basi usithubutu hata siku moja kuhoji elimu ya mtu mwingine maana nitaumbuka, tena mbaya zaidi ukapotea njia na kuhoji ya mtu ambaye ni genius...

Fuso, hapa mimi ndiyo nahisi kuwa wengi tumeingia Mkenge. Personally siamini kuwa Nnauye Jr ni mjinga kiasi kwamba afikiri kuwa aulize na kufukunyua elimu ya Mnyika alafu akadhani raia watatulia tu na kutoku chokoa yake.

Hizi ndizo Siasa za Nape, hana soni wala hatikisiki... Matokeo yake kuwa wazi hata kama kafeli kuliko aliye mchokoa ambae matokeo yake ni 'outstanding' nahisi haimpi shida kabisa Nnauye!

Nadhani hii yote ni ku-divert watu kutojadili masuala yaliyo msingi kwa jamii na kuanza kujadili elimu ya Nnauye na Mnyika. Hili likipita atakuja tu na lingine... He is good at it. Siyo kwamba nampongeza, ila ndiyo ukweli wenyewe (per my observation and understanding).
 
Tunachotakiwa kufanya kama jamii inayomzunguka John Mnyika siyo kumzodoa na kumshambulia kwa matusi bali kumpa moyo na nguvu ili arudi shule na kumaliza degree yake ya kwanza.Nina uhakika kama hatafanyiwa hujuma na chuo kikuu John Myika anauwezo mkubwa wa kufaulu.

Ningemsihi sana mdogo wangu Mnyika pamoja na wito alionao wa kujenga Taifa lake bado bila elimu ya darasani inahitajika.Hata jioni aweza kujisomea na akamaliza degree yake.

Viongozi waChadema wanapaswa kumpunguzia kazi kijana wao ili amalize shule yake.Na siyo Mnyika tu vijana wote ambao hawajamaliza shule zao au walimaliza form four wakati ni huu wa kurudi shule na kuendelea na masomo yao.Elimu kwanza siasa baadaye.
Hizo ratiba za kuomba chama kimpunguzie kazi ni wazo lako, ila tayari ameshatoa msimamo wake juu ya kuendelea na masomo yake.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
nina shaka sana na elimu ya nape,huwezi kupata digrii ukiwa kiongozi wa ccm na masters(nape)phd(nchimbi)katika awamu ya d.haifu halafu nika-relax eti ni za halali!!there is something stinky behind their certificates.
 
Hapa yapo mawazo ya msingi na michango yenye kulenga kujenga..,wapo ambao wanaona mfumo wa kuelekeza akili na kuthamini cheti si mfumo nzuri kuweza kupata mtu mwenye uwezo na kumtumia katika mikakati ya maendeleo ya jamii yetu.,lakini swali moja la msingi la kujiuliza ni kuwa kama si kwa cheti ni njia ipi ya mbadala ambayo tunaweza kupima na kujiridhisha kuwa mtu husika anaop uwezo wa kutosha wa kumudu majukumu na wajibu atakaopangiwa kwa kazi husika bila ya kuangalia na kufuatilia CV yake ya Kielimu (tukimaanisha Vyeti..)..?
nchi zilizoendelea zimeweka mfumo wa kuwapata watu hawa, kuwaendeleza kielimu kwa manufaa ya taifa husika. wengi wao wanakuwa kwenye maabala ya technologia, viwanda vya siraha na mitandao ya kijasusi nk

Mtoto mwenye kipaji cha pekee huwa anajulikana mapema na anakuwa mikononi kwa serikali - serikali ndio itaamua impeleke nyanja ipi kutokana na mahitaji ya taifa.

kuna kipindi mwalimu alifikiria kuanzisha kijiji cha sayansi na technologia lengo likiwa ni kuanza kuwatafuta na kuwaendeleza watu hawa kwa manufaa ya taifa. Akina myika walitakuwa kuwa hazina ya nchi kwani wenye uwezo kama wake wapo wachache.
 
They are both Great at what they do... Swali linabaki hizo CV zinavyoendelea kuleta mlolongo wa majadiliano nani ana benefit siku ya mwisho? Mnyika/Nape/CCM/CDM ama Wananchi?

Sehemu ya kwanza ya swali lako ni rahisi kulijibu linajibu sehemu ya pili ya swali lako.

CV kama CV ina sehemu kuu nne umuhimu unaongezaka kwenda chini

1. Taarifa za kuzaliwa (Mambo binafsi) inasaidia kufuatilia historia ya nasaba ya mtu. 5%

2. Hobby, ushiriki kwenye taasisi kwa uanachama au kukaribishwa kutoa mada 5%

3. Elimu: Inaonyesha jinsi ulivyoipata na misingi ya ubongo ulivyohinikishwa kukabili mazingira 25% Mara chache sana (labda Tanzania pekee duniani) vyeti vya elimu vinahitajika kama sehemu ya CV.

4. Uzoefu na mafanikio 65% (Experience and deliverablea) Hizi zinagawanyika kwa specialisation na faida kwa jamii.

Ili uweza ukawekwa kwenye kigezo cha ubora CV yako kwenye vigezo hivyo nilazima isipungue 70% Ukiondoa 1 na 2 hapo juu utashindanisha 3 na 4 ambazo peke yake zina score ya 75%

3 hapo juu kama umesoma vyuo vya kutambulika zinaamua kiwango cha chini kabisa cha mshahara. 4 ina over ride tatu kwa sababu deliverables na aina ya kazi ni standard. Cha msingi 4 inaainisha wapi mhusika atatoa results/matokeo yanayotarajiwa.

Huwezi kufanya vizuri kwenye 4 kama huna background nzuri kwenye 4. Miaka yetu mtu wa darasa la nane alifaa sana kuwa DC wa siku hizi. Siasa wakati huo ilikuwa mchezo wa wahuni ambao hawakuwa na nafasi kwenye kazi za tija. Nalizungumzia hivyo kwa sababu kitaifa tumereverse utendaji wa kisiasa umekuwa tija na uzalishaji/production kwenye nyanja zote muhimu ni utwana. Matokeo yake hatuna uzalishaji wa tija (Kijamii, kiuchumi).

Nape vs Mnyika CV. Tukiangalia namba 3 hapo juu tumpe Nape 20% kwenye namba 3 na Mnyika tumpe 17.5%
Kwenye namba 4 tunalie kazi za tija kwa kwa maana nani amemtendea mwananchi/taifa kitu kinachopimika chenye tija?

Mnyika atachukua 55% na Nape 35% kwa kuwa very fair kwa kigezo kimoja baada ya kingine. Kwa score kadi ya Nape itasoma 55% na ya Mnyika 72.5%. Tukijulisha na sehemu ya 1 na 2 Score ya Nape itafikia 65% na Mnyika 82.5%.

Hii inadhirishwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge ambapo Nape alipata nafasi ya tatu kwa wagombea wa CCM na Mnyika kama tujuavyo

Nawasilisha kwa mawazo mbadala
 
Nimependa analysis yako Mimibaba,

But nahisi hujanipata vema... Sisemi kuwa CV hazina umuhimu; Ina umuhimu saana.

Haya majadiliano juu ya CV ya Mnyika na Nnauye ingekuwa really valid kama sasa wangekuwa wapo katika kinyang'anyiro fulani ambacho wana niya ya kugombea. Na umuhimu huo ungekuwa tu ni moja ya kipengele cha vipengele...

Naomba kama hutajali unijibu... Hizi discussions zanazoendelea juu ya CV zao na elimu kuna namna yoyote ambayo wananchi wananufaika? Take note tunajadili CV za watu ambao tayari nafasi zao zipo 'Defined' na haya majadiliano hayaongezi wala kupunguza kitu kwa hizo nafasi zao.... Pengine labda sioni na unieleweshe.
 
Last edited by a moderator:
Kumekuwepo na mjadala mkubwa kwenye social medias kuhusiana na Elimu ya Katibu wa Uenezi wa CCM- NAPE MOSES NNAUYE na Mkurugenzi wa Uenezi wa CDM-JOHN MNYIKA.,mjadala ambao ni mpana na unazalisha maswali na hoja nyingi vichwani mwa watu.

Nikiwa naufuatilia kwa makini mjadala huo, nimeipitia maoni ya mmoja wa great thinkers kwa jina la mtanzania na ametoa ushauri ambao nadhani ni ushauri bora unaotoa mafunzo ya msingi katika kuzifanyia tathimini CV hizo za viongozi hao waandamizi wa vyama vikubwa vya siasa hapa nchi.

Katika elimu kuna mambo mawili ambayo bado hayajawa sambaba. Kuna elimu ambayo msomaji angependa awe na vyeti vizuri, na labda toka katika vyuo vikuu vyenye majina makubwa Duniani na elimu ingine ni ile isiyojali sana vyeti ila inampa msomaji ujuzi/uwezo wa kutenda ipasavyo, mara nyingi huwa hajali kama anapata cheti toka chuo chanye jina au la.
Kuna mifano na mazuri katika yote mawili.
Watu wanaosoma na kupenda elimu ya kwanza ya vyeti, ni watu wanaoamini vyeti vyao na shule/vyuo walivyosoma vitawafanyia wepesi katika mambo yao. Watu wa aina hii ya elimu ni watu wanaotegemea kuajiariwa, watu hawa ni watu ambao wapo tayari kwa lolote ili wapate vyeti vyao, hawa huwa watii hata kwa mamlaka dhalimu ili wapate vyeti vyao, ni sawa na wasemao "Tumikia kafiri upate mradi". Pia katika kundi hili wanakuwepo pia wanazuoni na watafiti mbalimbali, kwani moja ya sifa ya mtafiti au mwanazuoni ni machapisho (publications) na majina ya vyuo au journals ni muhimu.

Katika sehemu hii ya pili niwatu wanataka elimu pasi kujali vyeti au jina la chuo ili waweze kufanya mambo yao. Wengi wa watu wa elimu ya aina hii ni watu wanakuja kujiajiri wenyewe, ni watu wenye kudhubutu(risk taking) kufanya mambo. Ni watu ambao wanasoma ili waje kujiajiari wenyewe, hivyo pindi wawapo katika masomo yao wakijiona wanauwezo wa kufanya yale watakayo huwaacha shule na kufanya mambo yao. Katika kundi hili kuna majina mengi ya watu waliofanya makubwa sana Duniani. Bill Gates alikuwa mwanafunzi mwenye uwezo mkubwa lakini alipoanzisha Microsoft aliacha chuo na kuendelea na Microsoft yake, Steve Jobs akiwa na Steve Woznak walitengeza Maknistosh lakini Jobs aliacha chuo akandeleza ndoto yake na kutengeza kampuni kubwa ya Apple, Mark Zuckerberg alikuwa mwanafunzi mweney uwezo sana lakini aliacha chuo akajihusisha na facebook.

Katika elimu hii nataka kuwaangalia Nape Nnauye wa CCM na John Mnyika wa CHADEMA. Kwa taarifa zilizowekwa hapa mtandaoni na watu wengine ambazo Nape hajajitokeza kuzipinga ni kuwa alipata daraja la nne pts 29 (Div 4 pts 29) lakini badae alijiendeleza hadi akapata shahada ya uzamili katika utawala (M.A. Public Administration) hapa anaonesha ni muumini wa elimu ya vyeti, na yawezakana hakuwa mwanafunzi mzuri sana lakini alijitahidi na akatumia njia yeyote ile ili apate vyeti ili kufaniukisha ndoto yake. Binafsi sijui kama alifanyaje hadi akapata shahada ya uzamili, sijui alikuwa mwanafunzi wa namna gani chuoni, lakini anayo shahada ya uzamili kutoka katika chuo kikuu cha Mzumbe.
John Mnyika kwa taarifa alizoziweka mwenyewe hapa kwenye mtandao anaonesha ni mwanafunzi mwenye uwezo wa kusoma chuo chochote Duniani ila anangukia katika kundi la watu wanaotaka elimu ili waweze kujiajiri, ndio mana alidhubutu kupinga ´baadhi ya mambo aliyaona haypo sawa, uamuzi ambao ulipelekea kufukuzwa chuo. Lakini alipoona ana uwezo wa kusimamia ayatakayo akaona hana haja ya kulamba uongozi wa chuo miguu ili arudishwé kumalizia shahada yake. Katika shuguli zake za siasa ameonesha uwezo mkubwa wa kusimamia anayoamini, tumeona hata uwezo wake bungeni, anaangukia katika kundi lakini Mark Zuckerberg,Bill Gates na wengine wengi.

Naona kuna tofauti kati ya wawili hawa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mtu hawezi kusoma ili afurahishe watu ama kujaza vyeti kwenye droo...wakati ana maono na malengo yake kuhusu maisha yake. Mnyika ni wazi anao uwezo wa kusoma na kupata hayo madegree mnayotaka muyaone au ana uwezo wa kununua vyeti awaoneshe kama walivyofanya wengine.....Lakini ameamua kuchagua kufanya yanayomfaa kutokana na kipaji chake, anapata nguvu kufanya na anasimamia hayo.

Halafu mtu tu, anatoka nje anamwambia eti kasome, kamalize shule....si vibaya,lakini kuna mahala Mnyika anapaona, Nape hapaoni au haelewi....

Kama mmesoma maelezo yake vizuri khs MNYIKA kupiga shule anasema "Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho"

Katika MNYIKA na NAPE unaweza kuona mwenye elimu nani.....vyeti au kuhudhuria madarasa mengi siyo kuelimika....

"Tangu mwaka 2012 na 2013, nimekuwa kwenye mtanziko mwingine na viongozi wangu ndani ya chama wanafahamu; niliomba kuachia majukumu mengine yote katika chama ili nibaki na ubunge peke yake niweze kuwatumikia wananchi wakati huo huo niendelee na masomo zaidi ya elimu ya juu katika fani inayoendana na kazi ninayoifanya ya sasa na matarajio yangu ya baadaye.

Hata hivyo, kwa mwelekeo huu wa Serikali na CCM leo nieleze tu kwamba nikifanya hivyo itakuwa faida zaidi kwa watawala tunapoelekea mwaka 2015; hivyo, nimeamua kama nilivyoamua mwaka 2005; kwamba nitarejea masomoni baada ya CCM kuondoka madarakani na Tanzania kupata Serikali mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho" John Mnyika
 
Tunachotakiwa kufanya kama jamii inayomzunguka John Mnyika siyo kumzodoa na kumshambulia kwa matusi bali kumpa moyo na nguvu ili arudi shule na kumaliza degree yake ya kwanza.Nina uhakika kama hatafanyiwa hujuma na chuo kikuu John Myika anauwezo mkubwa wa kufaulu.

Ningemsihi sana mdogo wangu Mnyika pamoja na wito alionao wa kujenga Taifa lake bado bila elimu ya darasani inahitajika.Hata jioni aweza kujisomea na akamaliza degree yake.

Viongozi waChadema wanapaswa kumpunguzia kazi kijana wao ili amalize shule yake.Na siyo Mnyika tu vijana wote ambao hawajamaliza shule zao au walimaliza form four wakati ni huu wa kurudi shule na kuendelea na masomo yao.Elimu kwanza siasa baadaye.

mnyika hawez kurudi udsm, bcoz udsm wamekaa kipro ccm. myika piga kazi nafasi ya kusoma ipo tu.
 
hao watu wanaosemwa kwenye mtanzania hawafai kufananishwa na nape nnauye hata kidbuogo....
Yeah alijaribu kurudia mara mbile mtihani wa form four... Lakini yeye alikuwa na godfather na ccm-cult nyuma yake

wewe beba cheti chako cha form four division two uombe scholarship za kwenda india utasikia majibu yake

please misichanganye machungwa na machenza...

kweli ukiwa na mnene wa kukupush na ukapatakachuo kachuo ka kishkaji indiaunatoka,vigievyo utabaki hivyo2.
 
Back
Top Bottom