Haya majadiliano juu ya CV ya Mnyika na Nnauye ingekuwa really valid kama sasa wangekuwa wapo katika kinyang'anyiro fulani ambacho wana niya ya kugombea. Na umuhimu huo ungekuwa tu ni moja ya kipengele cha vipengele...
Naomba kama hutajali unijibu... Hizi discussions zanazoendelea juu ya CV zao na elimu kuna namna yoyote ambayo wananchi wananufaika? Take note tunajadili CV za watu ambao tayari nafasi zao zipo 'Defined' na haya majadiliano hayaongezi wala kupunguza kitu kwa hizo nafasi zao.... Pengine labda sioni na unieleweshe.
Maelezo yangu yalilenga jinsi CV ambavyo inatumika globally. Nikiwa mkweli kwenye hii discussion ya CV nitakuwa judgemental kitu nilikuwa nakikwepa. Lakini basi tuendelee.
1. Wanzilishi wa mjadala wa CV ni CCM(Nape) kwa lengo la kumdiscredit Mnyika. Ndiyo maana nao imelazimika CV??? zijadiliwe. Kwa nini CCM walileta mjadala huo ni kwa sababu viashiria vyao vya utendaji katika siasa za maji taka ni CV. Ndiyo maana kuna watu ndani ya CCM wana Phd ilihali hawana elimu hiyo. Kwa Mnyika ilikusudiwa kutoa picha ya mtu aliyedanganya elimu yake kwa hiyo alipata ubunge kwa udanganyifu na sisi humu JF tushadidie bila kupewa vigezo na visharia vya kumpima na kumhukumu Mnyika. Hizo ndizo siasa za maji taka. Yalimpata Salum A. Salum kuwa si Mtanzania, Bashe, Ulimwengu orodha ni ndefu.
Kwa hiyo kwa CCM ni majadiliano valid
2. Sisi tunaojadili ni wazi tunajadili kishabiki kupingana bila hoja na lengo. Hapa nasisitiza majadiliano haya ni muhimu kukabiliana upande mwingine; na ni afya kwa wanaJF kuwa "informed" na information siyo lazima iwe accurate, valid na achieving kwenye mazingira haya.
3. Tunawajadili CV zao pamoja na kuwa wako kwenye nafasi zao kwa sababu upande mmoja ulitaka kutujulisha kuwa Mnyika ni muongo kadanganya elimu hafai. Siyo kuwa hoja za Mnyika zina mapungufu gani.
Mimi ni muumini wa JF CV yangu ni ya M&E kwenye utendaji (performance). Cha kwanza naangalia malengo target/objective; mbinu/strategies, resources/rasilimali na matokeo kufikia malengo. Cha pili naangalia kitu kinaitwa crisis management uongozi na usimamizi wa mkanganyiko.
Kifupi CCM wana mikanganyiko mingi ambayo wanafanya kila njia kuisimamia/kumanage. Wana lengo la kuonyesha jitihada zao lakini kwa kuwapaka matope wengine. Wanazo resources kwa mikakati hiyo hata kama hawatathmini kabla matokeo yatakuwaje.
Mnyika naweza kusema kifupi anafanya anachokiamini kwa rasilimali aliyonayo kwa lengo la kwenda kinyume na yanayofanywa na CCM. Hapo kuna mgongano lazima hoja hata za CV ziletwe public.
Mimi naona ni healthy informed discussions; tunanufaika sana na hizi discussion tunaokuwa na access nazo. Wananchi wengi hawana access ya hizi discussion ingawa sisi tuna majukumu ya kuwashirikisha na kinachoendelea kwenye hizi discussions ili tuwa"equip" kufanya maamuzi kuhusu wanayoambiwa na wanayoshirikishwa. Kwa sababu wananchi hata kama hana elimu lakini ana uwezo (IQ) ya kupima hata kwa hisia.
Sina uhakika kama nimekuelewesha ila naamini discussion ya CV ya Mnyika kwangu mimi imenifundisha mengi yenye faida. Kwa mfano wote wameonyesha walivyojitahidi kukamata elimu hata kama ni bora elimu. Wote wameji"expose" na kulinganishwa kiutendaji. Na wote wamesimamia malengo yao kwenye taasisi zao.
Imenipa fursa adhimu kubaini mikakati mufilisi ya CCM kwa watu binafsi wacha Mnyika orodha ni ndefu. Kwa mtazamo tu nimeona kama mikakati hiyo imeimarisha sana upande uliotuhumiwa na watu binafsi walioshambuliwa. Ingawa lazima nikiri labda nao CCM wamepata return ya adventure yao.
Ukitaka tija katika suala hili itategemea mtu binafsi ana uelewa upi unaompa tools za uchambuzi zipi kwa lengo gani? Kwa hiyo hata wewe ukiona hazina tija potezea, mimi kwangu ni input muhimu ninayoipata bure juu ya wrong or rght strategies kuhusu Siasa za maji taka