Katika elimu kuna mambo mawili ambayo bado hayajawa sambaba. Kuna elimu ambayo msomaji angependa awe na vyeti vizuri, na labda toka katika vyuo vikuu vyenye majina makubwa Duniani na elimu ingine ni ile isiyojali sana vyeti ila inampa msomaji ujuzi/uwezo wa kutenda ipasavyo, mara nyingi huwa hajali kama anapata cheti toka chuo chanye jina au la.
Kuna mifano na mazuri katika yote mawili.
Watu wanaosoma na kupenda elimu ya kwanza ya vyeti, ni watu wanaoamini vyeti vyao na shule/vyuo walivyosoma vitawafanyia wepesi katika mambo yao. Watu wa aina hii ya elimu ni watu wanaotegemea kuajiariwa, watu hawa ni watu ambao wapo tayari kwa lolote ili wapate vyeti vyao, hawa huwa watii hata kwa mamlaka dhalimu ili wapate vyeti vyao, ni sawa na wasemao "Tumikia kafiri upate mradi". Pia katika kundi hili wanakuwepo pia wanazuoni na watafiti mbalimbali, kwani moja ya sifa ya mtafiti au mwanazuoni ni machapisho (publications) na majina ya vyuo au journals ni muhimu.
Katika sehemu hii ya pili niwatu wanataka elimu pasi kujali vyeti au jina la chuo ili waweze kufanya mambo yao. Wengi wa watu wa elimu ya aina hii ni watu wanakuja kujiajiri wenyewe, ni watu wenye kudhubutu(risk taking) kufanya mambo. Ni watu ambao wanasoma ili waje kujiajiari wenyewe, hivyo pindi wawapo katika masomo yao wakijiona wanauwezo wa kufanya yale watakayo huwaacha shule na kufanya mambo yao. Katika kundi hili kuna majina mengi ya watu waliofanya makubwa sana Duniani. Bill Gates alikuwa mwanafunzi mwenye uwezo mkubwa lakini alipoanzisha Microsoft aliacha chuo na kuendelea na Microsoft yake, Steve Jobs akiwa na Steve Woznak walitengeza Maknistosh lakini Jobs aliacha chuo akandeleza ndoto yake na kutengeza kampuni kubwa ya Apple, Mark Zuckerberg alikuwa mwanafunzi mweney uwezo sana lakini aliacha chuo akajihusisha na facebook.
Katika elimu hii nataka kuwaangalia Nape Nnauye wa CCM na John Mnyika wa CHADEMA. Kwa taarifa zilizowekwa hapa mtandaoni na watu wengine ambazo Nape hajajitokeza kuzipinga ni kuwa alipata daraja la nne pts 29 (Div 4 pts 29) lakini badae alijiendeleza hadi akapata shahada ya uzamili katika utawala (M.A. Public Administration) hapa anaonesha ni muumini wa elimu ya vyeti, na yawezakana hakuwa mwanafunzi mzuri sana lakini alijitahidi na akatumia njia yeyote ile ili apate vyeti ili kufaniukisha ndoto yake. Binafsi sijui kama alifanyaje hadi akapata shahada ya uzamili, sijui alikuwa mwanafunzi wa namna gani chuoni, lakini anayo shahada ya uzamili kutoka katika chuo kikuu cha Mzumbe.
John Mnyika kwa taarifa alizoziweka mwenyewe hapa kwenye mtandao anaonesha ni mwanafunzi mwenye uwezo wa kusoma chuo chochote Duniani ila anangukia katika kundi la watu wanaotaka elimu ili waweze kujiajiri, ndio mana alidhubutu kupinga ´baadhi ya mambo aliyaona haypo sawa, uamuzi ambao ulipelekea kufukuzwa chuo. Lakini alipoona ana uwezo wa kusimamia ayatakayo akaona hana haja ya kulamba uongozi wa chuo miguu ili arudishwé kumalizia shahada yake. Katika shuguli zake za siasa ameonesha uwezo mkubwa wa kusimamia anayoamini, tumeona hata uwezo wake bungeni, anaangukia katika kundi lakini Mark Zuckerberg,Bill Gates na wengine wengi.
Naona kuna tofauti kati ya wawili hawa.