Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Katika kuendelea kuwafanya Watanzania ni wajinga na watu wasiojua chochote, nimewasikia Makamu Mwenyekiti wa CCM Stephen Wassira na Mwenezi wao Amos Makalla wakidai kuwa, yalishafanyika mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi hivyo hoja ya No Reform No Election haina mashiko.
Wassira na Makalla wanasema haya wakati Watanzania wote tunatambua hayo maigizo ya kujifanya wanarekebishwa Sheria za Demokrasia na Uchaguzi yalifanyika kuwahaa Watanzania kuanzia mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwanzoni mwa mwaka 2024.
Wassira na Makalla wanasema hayo huku Watanzania tukiwa tunatambua kuwa pamoja na Maigizo hayo yaliyofanywa na CCM na watu wao kujifanya wanatengeneza Tume Huru ya Uchaguzi, katika zoezi la uchaguzi lililofanyika baada ya mabadiliko hayo ya mazingaombwe ( Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024) tulishuhudia Wagombea wa vyama vya Upinzani karibu asilimia 95 (Hasa CHADEMA) kuenguliwa.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa mujibu wa taarifa za Viongozi wa CHADEMA, Wagombea wao zaidi ya 9000 walienguliwa kwenye uchsguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwezi Novemba 2024.
Napenda kuwaambia Amos Makalla na Stephen Wassira. Sehemu pekee ambayo kama CCM wangekuwa na akili walipaswa kuwaonesha Watanzania kuwa kuna reforms zimefanyika, ni kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka jana 2024.
Kwa ule uchafuzi uliofanyika kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwezi Novemba mwaka jana, Watanzania wote tunaoipenda nchi yetu na tunaojitambua, tunakubaliana na CHADEMA kuhusu NO REFORM NO ELECTION.
Rai yangu kwenu. Ni heri nchi hii tusiwe tena na chaguzi na pesa za kufanyia uchaguzi tukanunulie madawa hospitali na kupeleka huduma bora za kijamii kwa Watanzania kuliko kupoteza hela za walipa kodi wa taifa hili kufanya maigizo ya kuwachezea Watanzania as if wao ni watoto wadogo wasiojitambua. Hii ni kwa sababu nchi hii hakuna uchaguzi ila kuna uchafuzi. Hakuna kiongozi anaywpatikana nchi hii kwa kupigiwa kura halali na Wananchi. Viongozi wote wanaopatikana kupitia chaguzi ni wale ambao CCM kupitia Tume na Wakurugenzi wao wa Halmashauri wanaamua wawe Viongozi na sio kura halali za Wananchi.
Kama CCM na Serikali yake mlishindwa kutuonesha maana ya chaguzi huru na za haki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba, 2024. Basi hakuna mabadiliko ya Sheria tutakayoyaamini Watanzania. Sote tutasema kwa sauti moja NO REFORM NO ELECTION.