Majibu ya CCM Mdahalo wa Odemba: Tunasikitishwa na jinsi alivyoupotosha umma, tumeshangazwa na machozi yake!

Majibu ya CCM Mdahalo wa Odemba: Tunasikitishwa na jinsi alivyoupotosha umma, tumeshangazwa na machozi yake!

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu kutoshiriki kwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenye mdahalo ulioandaliwa na Kituo cha Televisheni cha Star Tv, na kuratibiwa na Ndugu Edwin Odemba tarehe 31 Agosti, 2024.

CCM inautaarifu umma kuwa Katibu Mkuu hakukimbia wala hakudharau mdahalo huo. Balozi Nchimbi alifanya kila jitihada za mawasiliano na muaandaji na tunasikitishwa na jinsi alivyoupotosha umma.

Tarehe 10 Agosti 2024 mtangazaji wa Kituo cha Televisheni, Star Tv, Ndugu Edwin Odemba alimtafuta Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (sms) akimuomba Katibu Mkuu ashiriki mdahalo huo wa viongozi wa vyama vya siasa uliopangwa kufanyika Jumamosi, tarehe 31 Agosti 2024.

Katibu Mkuu alimjulisha kuwa masuala ya vyombo vya habari yanaratibiwa na Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla hivyo awasiliane naye na akampa namba ya simu ya mkononi ya Ndugu Makalla.

Kwa sababu ambazo Odemba anaweza kuzieleza mwenyewe, katika kipindi cha takriban wiki tatu, hakufanya mawasiliano au kumtafuta Ndugu Makalla kama alivyoelekezwa na kushauriwa na Katibu Mkuu Balozi Nchimbi.

Baada ya kuhisi kwamba nafasi ya Katibu Mkuu inaweza kuwa ngumu kupatikana kutokana na majukumu yake ya kazi za chama, Ndugu Odemba alimtafuta tena Balozi Nchimbi akiomba amuandae mwakilishi huku matangazo ya mdahalo huo yakiendelea kumtaja Katibu Mkuu wa CCM kuwa ndiye atakayeshiriki. Badala yake Katibu Mkuu alimwelekeza Ndugu Odemba kutofanya lolote kabla ya kupata mawasiliano na Sekretarieti ya Chama.

Kimsingi Ndugu Odemba alitaka wananchi wadanganywe kuwa CCM kupitia kwa Katibu Mkuu ilikuwa imethibitisha kushiriki katika mdahalo huo jambo ambalo si sahihi.

Katika mazingira ya kustaajabisha tumeshangazwa na machozi ya Ndugu Odemba aliyotoa jana akielekeza lawama kwa CCM na kwa Katibu Mkuu wakati alijua bayana kwamba alikuwa hajapata uthibitisho wowote wa CCM kushiriki ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba yeye mwenyewe alishajua kwamba alikuwa akiendelea kutangaza kuhusu mdahalo huo kama "promo" pasipo kupata ridhaa ya CCM.

Katibu Mkuu wa CCM ndiye Mwenyekiti wa Sekretarieti na siku nzima ya jana ambayo ndiyo siku Odemba alipanga kufanyika kwa mdahalo huo, kulikuwa na vikao vya maandalizi ya Kamati Kuu Maalum ambayo inafanyika leo tarehe 01 Septemba 2024, jambo ambalo kwa namna yoyote Katibu Mkuu asingeweza kuwapo katika mdahalo huo hata kama angekuwa amethibitisha awali.

Kushiriki kwenye mdahalo kunahitaji mashauriano na maafikiano kati ya waandaji na waalikwa.

Tunaweza kutamka bayana na kwa uhakika kwamba Katibu Mkuu hakuwa ametoa uthibitisho wa kuhudhuria mdahalo huo. Hakukuwa na makubaliano yoyote rasmi ya yeye au mwakilishi wake kuhudhuria katika shughuli hiyo. Mwisho, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Nchimbi yupo tayari kwa midahalo, majadiliano na makongamano yanayolenga kujenga umoja wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa kadiri ya taratibu zilizopo na ratiba yake ya kazi inavyoruhusu.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

1725190150817.png


1725190194087.png


Pia soma
- Kuelekea 2025 - Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa: Nchimbi kaingia mitini, wengine wagoma kushiriki!
 
Huyo Nchimbi na sisiem hata wakipewa wao nafasi ya kupanga ratiba ya mdahalo bado wataukimbia tu.

Hivi unaenda kwenye mdahalo kuwakilisha kambi ya mashetani yenye kila aina ya uovu, unategemea uongee nini zaidi ya kujiaibisha? Wasitufanye sie maboya, Nchimbi kafanya calculations kaona anaenda kujivua nguo mwenyewe akala kona, over.
 
Back
Top Bottom