Ndugu Jf-Doctors, mimi nina mchumba ninayetarajia kumwoa. Kwa maelezo yake, yeye bado bikra. Jana tulikwenda katika hospitali ya wilaya kupima HIV. Mimi nilionekana NEGATIVE, lakini majibu yake yeye yalinichanganya. Kipimo cha Determine kilionyesha POSITIVE, lakini Uni-gold ilionyesha NEGATIVE. Leo asubuhi tukaenda kwenye VCT kupima tena na majibu yakawa yaleyale. Tukaenda hospitali ya rufaa ili tupate kipimo cha ELISA au WESTERN BLOT lakini wakasema vipimo hivyo hawana. Je, jibu sahihi ni lipi au tufanyeje?