Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Wakuu heshima mbele,
Yafuatayo ni mahojiano kati ya Rais Kikwete na Mwandishi wa BBC Bw. Omar Mutasa huko Afrika Kusini ambako Rais Kikwete alikuwa anaendelea na ziara yake ya Kiserikali.


BBC: Suala la Umeme Mheshimiwa Rais Kikwete ungependa kulizungumzia nini?

Rais Kikwete: Tatizo la umeme kimsingi ni suala la ukame tu. Kwa sababu mabwawa yetu ya kuzalisha umeme yanayotoa umeme karibu MW600 sasa hivi yanatoa umeme kidogo sana. Maji pungufu ndio maana kuna tatizo hilo.

BBC:Mheshimiwa, hili suala si la leo wala si la jana limekuwepo kwa muda mrefu, kwanini serikali haina njia mbadala ya kuweza kutatua suala hili? Tanzania ina raslimali nyingi mheshimiwa Kikwete!

Rais Kikwete: Kwanza, serikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe, unajua unajua hivyo, Kwa sababu (kicheko) ingekuwa na uwezo wa kufanya mvua inyeshe mabwawa yale yangejaa.
Ni kweli kuwa Tanzania inazo raslimali za kutosha na katika kipindi hiki - toka wakati ule - sisi tulipoingia tumekuta suala la Ukame na mwaka 2007 tukapata matatizo ya kwanza.Baada ya pale tukafanya uamuzi kwamba sasa tuanze kuwekeza katika vyanzo vingine; tuongeze uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo vingine. Tuongeze uzalishaji wa umeme kutoka vya vya kutumia gesi asilia twende kwenye makaa ya mawe. Kutoka vyanzo vya gesi asilia tayari tuna mtambo pale Ubungo, na toka mwaka 2009 mpaka sasa tumeshaongeza MW145, itakapofika Disemba tutakuwa tumeongeza MW160 nyingine. Tutakuwa tumeongeza MW300 siyo kidogo.

BBC: Mhe. Kikwete Mmoja katika wabunge Bw. John Mnyika ambaye ni Mbunge wa upinzani ambaye ni Waziri Kivuli wa Nishati amekuwa akilalamika na kwamba amewahi kusema kwamba hili tatizo ni tatizo linalowahusu Watanzania wote na amesema mje pamoja na kuona vipi mtakavyotatua tatizo hili. Na sasa hivi Bungeni wamesimamisha mswada, wa kutoa bajeti ya nishati ya Tanzania. Wewe unachukulia vipi matamshi kama haya kutoka kwa Wabunge?

Rais Kikwete: Mimi nasema hivi yeye si Mbunge atoe maarifa yake tu; anayo maarifa gani na anapendekeza kitu gani. Kwa sababu toka Uhuru mabwawa tuliyotengeneza ni Kidatu MW200, Mtera MW80, Kihansi MW 165 mimi nilipokuwa Waziri wa Nishati, pale Pangani tumeongeza.Sasa ufikirie kwamba toka Uhuru tumeweza kuzalisha umeme wa MW600, lakini toka 2009 mpaka Disemba mwaka huu tutakuwa tumeongeza MW300! Ni jitihada kubwa.
Mimi nasema kwamba usipozitambua hizo ni kwamba wewe mwenyewe siyo mkweli.Sasa ni hivi, unajua hii mitambo ya umeme si mitambo unaenda kununua kama unavyonunua jaketi lako hili. Ni kwamba ukitaka mitambo ya umeme, lazima uweke order wakutengenezee. Huu mtambo unaofika mwaka huu Disemba order tuliweka mwezi wa Juni mwaka jana. Inachukua muda huo kutengeneza. Sasa ingekuwa mnaenda kutafuta mitumba, mitumba ya mitambo tu ya kununua iko mingi kweli. Tukasema hatuwezi kufanya hivyo.Mimi nasema hivi, kitu kikubwa ni kuwa na subira. Tumefanya jitihada kubwa. Ni lazima watu watambue kuwa tumefanya jitihada kubwa katika miaka hii toka 2009 mpaka sasa hivi 2011 Disemba tutakuwa tumeongeza MW300 kulinganisha na MW600 ambazo tumeziongeza katika miaka yote hii. Nasema ni lazima watu watambue hivi. Sasa kama kuna mtu ana maarifa ya haraka zaidi nasema mtu atoe maarifa hayo na sisi kama yapo tutayafanyia kazi.

BBC: Kuna njia kama umeme wa jua, umeme wa kutokea ardhini wa mvuke, kwanini serikali haitafuti njia mbadala kuzalisha umeme kwa njia hizo?

Rais Kikwete: Nasema hivi, hata umeme wa jua lazima ujenge, umeme wa mvuke lazima ujenge, si kitu cha mwezi mmoja. Nasema huo ndio ukweli wenyewe na wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - “unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo” - tungeweza kufanya hivyo.Sisi sasa hivi kwa mfano tunajiandaa kuzalisha umeme wa kutumia Upepo, pale Singida. Tuna mwaka wa tatu sasa tuna mipango na Wakorea wa Kusini, umeme haujakuwepo. Kwa hiyo nasema hayo ni maelezo rahisi. Wanasema “mbona jua lipo?” katengeneze umeme wa jua kama jua lipo! (kicheko).

BBC: Watanzania wamekuwa wakisema (mwisho kabisa) kwamba Tanesco ingebinafsishwa ili waweze kupata makampuni kufanya kazi hiyo ya umeme?

Rais Kikwete: Aah! Kwani ukitaifisha kesho ndio utapata mitambo kesho? Nasema hivi ni vizuri kuelewa tu - kwanza tatizo la msingi - ni maji kukauka kwenye mabwawa. Maji yasingekauka kwenye mabwawa tatizo hili halipo. Maji yamekauka kwenye mabwawa kwa sababu ya ukame. Hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzuia ukame usiwepo. Sasa hiki ndicho kiini cha tatizo. Sasa nasema sisi jitihada ambayo tumeifanya ni kupunguza sasa kutegemea umeme unaotakana na nguvu ya maji.Toka mwaka 2009 tumewekeza adi Disemba 2011 tutakuwa tumeongeza MW 310, yenyewe hiyo ni hitihada kubwa, ni vizuri ukaitambua jitihada hiyo. Kulikoni kusema kitu tu nasema hatakam huna majawabu rahisi utuambie tu.

MWISHO.
 


Miaka ya 80 (1980s)hatukuwa na megawati 600, uko wapi weyee? Nilichkueleza mimi ni jumla ya miaka themanini (80 Years)

Hakuna wakati wowote ambapo umeme umetutosha Tanzania na kabla hatujawa Tanzania. mpaka leo ni asilimia chini ya 15 inayopata umeme, Kikwete anakuambia atahakikisha ifike 50% kabla hajaondoka na hapo namuamini kwani anafanya kweli.

Megawati mia zinakuja mwezi huu na wa nane zilitiwa order June 2010. Wewe inaonesha uko "out of touch kabisa" bora ukae kimya tu maana huna hoja una viroja.
 
Hapana mkuu wangu unakosea sana na maelezo ya JK yanaonyesha ufinyu wake wa kufikiri..
labda nikueleze vizuri na kwa uhfasaha ambao JK anaukwepa.
Hadi kufikia miaka ya 80 uwezo wetu ktk kuzalsha umeme (vyanzo) ulikuwa zaidi ya MW 3,000 na sii 600 isipokuwa tulikuwa tukitumia MW 600 ambazo Tanesco walizitumia ktk usambazaji..

sasa JK anachozungumzia ni kuongezeka kwa generators kuzalisha MW 300 zaidi hali generator hizo zinatumia Gas! chanzo cha nguvu za umeme kinachotokana na gas ndicho muhimu zaidi ya mikataba ya wawekezaji wa Generators ambao wanatuumiza ktk malipo. Ujenzi wa gas ya Songos ili itumike kuzalisha umeme sio mkakati wa JK ameukuta. Hydro dams kazikuta na hata Kiwira hkaikuta lakini kashindwa ku zikarabati kwa njia moja ama nyingine kiasi kwamba demand ya Umeme imeongezeka lakini yeye anaendelea kujaza Magenerator..Vynzo vinakufa kama viwanda vya Nyerere na imefikia hadi vyanzo hivyo haviwezi tena kuzalisha zaidi ya tuseme MW 900 (generating capacity)..

Ni sawa na wewe kununua jiko la Umeme hali unajua kabisa kijijini kwenu hakuna Umeme, kisha unanunua generator wakati unajua hakuna Diesel..matatizo ni kuchukua maamuzi rahisi bila kuzingatia kwanza vyanzo vya kitu unachotaka kutumia. Na ndio sisi tunasema matatizo yetu ni ya kujitakia.

Toka JK ameingia madarakani anajua fika mwalimu alitumia MW 600 kwa sababu ndio ilikuwa mahitaji yetu wakati huo na kazi kubwa ilikuwa kusambaza umeme huo hadi vijijini, miji yote mikubwa yenye umeme haikupatwa na adha hizi za mgao, leo JK kenda sambaza umeme kwenye machimbo ya madini na kuita wawekezaji wa viwanda hali akijua fika hatuna vyanzo vya kutosheleza mahitaji hayo huoni kama huu ni Ujinga mkubwa!.. Mkuu wangu hata sisi wa uswahilini huwezi kualika watu kwenye Hitma wakati unajua fika huna gunia la mchele..maswala ya Sunna hayawezi kuondoa ukweli kwamba umewaweka watu njaa...

Ni majuzi tu ktk sakata la Dowans, niliwahi kusema wazi kwamba hata kama tutawachukua Diowans na hizo MW100 hazitoshi kulingana na mahitaji yetu kwa nini tuingie mkataba na shirika hili ama tukubali ufisadi wao kwa sababu ya shida wakati tunajua fika MW 100 haziwezi kuondoa tatizo la mgao hata kidogo..Lakini wamelazimisha kununuliwa kwa mtambo huo wakati wakijua fika kwamba tatizo kubwa ni uwezo wa bomba ya gas kuhudumia mitambo iliyopo.

Kwa hiyo mkuu wangu JK anachokifanya ni kununua mashangigi hali hatuna barabara na wewe unamsifia kwa kuongeza mashangingi zaidi ukashindwa kufikiria gharama za mafuta, maintanance na kadhalika..haya ndio yanatupata leo hii mkuu wangu Umeme umewekwa juu ya mawe!
 

Hapo ndio umechemsha kabisa sina haja hata ya kumalizia kusoma mada yako. Mie naongelea jumla ya miaka 80 wewe unanipeleka 1980 ambapo hata chakula ilikuwa shida, kaya moja kilo moja kwa wiki ya sukari. Usinikumbushe.
 

Faiza,

Name us 5 major accomplishments done by 4th Government, and these accomplishments are project that they innitiated, planned and invest to the completion. Just 5 major projects!
 
Nchi inazidi kukumbwa na GIZA mtu anaendelea kusema JITIHADA KUBWA JITIHADA KUBWA!
 
Hapo ndio umechemsha kabisa sina haja hata ya kumalizia kusoma mada yako. Mie naongelea jumla ya miaka 80 wewe unanipeleka 1980 ambapo hata chakula ilikuwa shida, kaya moja kilo moja kwa wiki ya sukari. Usinikumbushe.
Sasa unaposema jumla ya miaka 80 unahesabu kitu gani? maanake nashindwa kukuelewa kwani hatujawa na Uhuru kwa miaka hiyo na hata ukizungumzia ukoloni inahusu vipi na uongozi wa JK?.

Na maajabu unakubali miaka ya 80 ambayo hatukuwa na chakula sijui kaya moja kilo moja kwa wiki lakini haya ya kukosa Umeme huyaoni tena una utetezi mkubwa wakati shida ni kubwa kuliko miaka 80 iliypita!. Wapi zamani mkuu...maanake mimi nakubali shida za miaka ya 80 lakini wewe unatetea ongezeko la umeme kwa miaka 80 wakati wananchi wanalia shida kuliko hata zile za miaka ya 80's au miaka 80 iliyopita. Kama hujichanganyi kitu gani mkuu wangu...

najua kweli JK ameweka mkataba na Warussi kujenga hydropower ya Mw 700 huko Iringa, lakini hii pia sio ujanja ikiwa yeye mwenyewe anakiri kwamba mvua hazileti yeye, na kwa nini asiende na geothermal au upepo? tukisema sisi mnasema tunamchukia JK. I mean mkuu wangu JK ktk utetezi wake hata angesema swala la ukosefu wa umeme tunalifanyia uchunguzi na zipo sababu akataja matatizo ya IPTL, Songos na kuwajaza ujinga wao kuliko kusingizia mvua kisha anakuwa mkali kwa ujinga na aibu alotuachia na zaidi ya yote JK anazidi kuweka mikataba ya ujenzi wa Dams kuzalisha umeme akitegemea mvua za Mungu...
Tena basi nasiki na Brazil nao wanapewa mradi wa 2bn kujenga nini - dam..
 
Kweli kama tuna machozi, basi tujililie wenyewe. Hamna wa kumlaumu mwenzake tujilaumu wenyewe
 
Ubabaishaji tu... tangu alipokuwa Waziri wa Nishati ni miaka mingapi imepita? Ukame ulikuwepo tangu 1974, 1984, 1994 nk... hata wangekuwa na mikakati imara tangu mwaka 2000 tu, kusingekuwa na tatizo la umeme mwaka 2011. Kwani mitambo ya umeme inahitajia karne nzima kutengenezwa? Asitubabaishe hapa!!!!!!!!!!!! Afrika Kusini walikuwa na tatizo la ghafla na wakalimaliza chini ya miezi miwili.
Halafu ufisadi wa mitambo ya Dowan, kama hiyo isingekuwa DEAL si angalau ingepunguza shida hizi?
Chad wameweza kutia taa za barabarani zinazotumia nguvu za jua katika mji mzima wa Abeche, na nusu ya mji wa Ndjamena kwa chini ya miezi sita! Sasa huu muda anaozungumza adhania watu wajinga? Ubaya wa Kikwete ni kuwa haoni haya kusema uongo. Badala ya kukiri uzembe na makosa aona afadhali aongopee. haoni kuwa tabia ya uongo ni tabia za kihuni za barabarani na kwamba unapokuwa kiongozi inabidi uepuke tabia hizo, au bado adhania yeye ni check bob?
 
Nasema hivi, ahadi zimekuwa nyingi na sisi tuko gizani. Hatutaki visingizio, miaka yote hiyo mmetawala ninyi CCM sasa leo unawaletea lawama wenzio as if you were not part of the system.
 
Hakuna kauli ya rais mkwele inayoniudhi na kunichefua siku nzima inayosema "serikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe". Kwa maoni yangu binafsi kauli hiyo ndiyo inayopambanua waziwazi uwezo mdogo wa kikwete. Siju kama kuna chizi anayeweza kutamka maneno ya ajabu kama hayo.
 

Naona hujasoma vizuri post yangu, lakini nilifundishwa kuwa "Mwalim bora huwa hachoki kuelekeza" soma:

Miaka 40 ya Muingereza jumlisha miaka 20 ya Nyerere jumlisha miaka 10 ya Mwinyi jumlisha miaka 10 ya mkapa: awamu hizo zote zina jumla ya miaka 80. Jee, umefaham?

Na katika hiyo miaka 80 Kikwete kakuta jumla ya megawati 600 za umeme toka tulizorithi kwa mkoloni mpaka yeye anachukuwa nchi. Jee, umeelewa?

Sasa yeye Kikwete kwa muda wake mfupi, Kisha leta megawati 200 tayari, Kisha saini mikataba tofauti ya megawati zaidi ya 500 tayari. Kwa hiyo, Kikwete kawekeza kwenye umeme zaidi ya awamu zoooooote zilizowekeza kwenye umeme alioukuta. Umeelewa au hujaelewa?
 
Nasema hivi,huu ukame kama ndio sababu basi tumelogwa wabongo!
 
personally nimemuelewa Mr. President sasa kama chadema wana alternatives hebu wauweke hapa tupime.
 
akijibu swali la omar mutasa wa bbc kuhusu kwanini hazitumiki njia mbadala wa kuzalisha umeme badala ya kutegemea maji ?
Kikwete alisema" umeme wa jua au mvuke siyo kitu cha mwezi mmoja au miwili " ameshasaau kuwa umeme wa mgao umeanza una zaidi
ya miaka 15. amefunika ufafanuzi wa swali la mtangazaji kwa kushindwa kufafanua juhudi za serikali ya ccm kuhusu njia mbadala za kuzalisha
umeme kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.majibu yake kwa BBC yamedhiirisha kuwa serikali haina comprehensive plan ya kutatua tatizo la umeme.
 
Rais wetu anajigamba na anafanya kosa kubwa sana kujisifia alichokifanya tofauti na wenzake waliomtangulia. Ni dalili ya kutokujiamini na kujitilia mashaka uwezo wake na inaelekea kana kwamba anataka apewe tukuzo na sifa wakati bado yupo madarakani kwa kazi ambayo matunda yake hayaonekani.

Nikirudi kwenye hizi megawati zake 300, sehemu kubwa ni kuwa tumejenga viwanda vya kufua umeme, lakini mitambo ya kuzalisha umeme si yetu. Pale Ubungo panapozalishwa mw 104, kuna IPTL (sina uhakika kama wanachangia sehemu), Symbion na sasa Jacobsen ambao mradi wao wa Dola milioni 125 za Kimarekani, sisi tumetoa asilimia 15 (15%) tuu kwa mradi mzima, na sehemu iliyobakia ni mikopo na ni Jacobsen na si Tanesco ndio inawezekana wakawa wamiliki wa mitambo.

Kuna hili jambo la umeme wa thermal na hiki kipande ni very interesting ukizingatia kuwa ni habari ya miaka miwili iliyopita na Tanesco hawajabadilisha walichoandika kwenye webusaiti yao. KIpande hiki, kinaonyesha mapungufu kwa vituo vinavyozalisha umeme kwa kutumia mafuta, na hovyo tukirudi kwemye majibu ya kudai mvuoa ndio chanzo, je hizi megawati nyingine zisizozalishwa kutokana na uchakavu wa mitambo ni nani alaumiwe?


Ama jedwali hili


na hili



na hii ambayo bado haijakamilika na iko chini ya wafadhili


So there goes mahesabu ya awamu yetu imefanya haya, in comparison to yaliyofanywa na awamu ya kwanza na ya pili.

 
Tunataka umeme no more bla bla bla! Mnyika alipowaambia watangaze swala la umeme janga la kitaifa walimuona mpayukaji. Nadhani majibu wameyapata kwwenye bajeti na bado...Time will tell!!
 
Ukisoma vizuri between lines utagundua kuwa umeme anaofikiria Mh. rais ni umeme wa nguvu za maji tu.
 
kama unaelewa na kutafakari hii diologue utagundua hii issue imempanikisha,ata majibu yake yapaniki paniki,tulia kaa na wataalam tatua tatizo,kama mkuu wa kaya huwezi toa jibu eti hutengenezi mvua,so,ukame ukiendelea zaid miaka10 twafunga nchi!uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…