FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Rais wetu anajigamba na anafanya kosa kubwa sana kujisifia alichokifanya tofauti na wenzake waliomtangulia. Ni dalili ya kutokujiamini na kujitilia mashaka uwezo wake na inaelekea kana kwamba anataka apewe tukuzo na sifa wakati bado yupo madarakani kwa kazi ambayo matunda yake hayaonekani.
Nikirudi kwenye hizi megawati zake 300, sehemu kubwa ni kuwa tumejenga viwanda vya kufua umeme, lakini mitambo ya kuzalisha umeme si yetu. Pale Ubungo panapozalishwa mw 104, kuna IPTL (sina uhakika kama wanachangia sehemu), Symbion na sasa Jacobsen ambao mradi wao wa Dola milioni 125 za Kimarekani, sisi tumetoa asilimia 15 (15%) tuu kwa mradi mzima, na sehemu iliyobakia ni mikopo na ni Jacobsen na si Tanesco ndio inawezekana wakawa wamiliki wa mitambo.
Kuna hili jambo la umeme wa thermal na hiki kipande ni very interesting ukizingatia kuwa ni habari ya miaka miwili iliyopita na Tanesco hawajabadilisha walichoandika kwenye webusaiti yao. KIpande hiki, kinaonyesha mapungufu kwa vituo vinavyozalisha umeme kwa kutumia mafuta, na hovyo tukirudi kwemye majibu ya kudai mvuoa ndio chanzo, je hizi megawati nyingine zisizozalishwa kutokana na uchakavu wa mitambo ni nani alaumiwe?
Ama jedwali hili
na hili
na hii ambayo bado haijakamilika na iko chini ya wafadhili
So there goes mahesabu ya awamu yetu imefanya haya, in comparison to yaliyofanywa na awamu ya kwanza na ya pili.
Habari uliyoiweka pamoja na takwimu za Tanesco zinakusuta. Au kusoma takwimu zinakupiga chenga? Mikataba ya umeme wakati wa Kikwete ni over 2,000MW. kama ulivyoonyesha katika jedwali la Tanesco ni nani aliyefanya zaidi yake katika awamu zote zilizopita? Hakuna hata uchanganye na mkoloni.