Majibu ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka mbele ya Baraza la Maadili

Majibu ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka mbele ya Baraza la Maadili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka alisomewa mshtaka manne katika Baraza la Maadili kutokana na malalamiko manne ya kukiuka maadili ya Viongozi wa Umma ambapo ameyakana yote

Kikao cha Baraza la Maadili liliketi chini ya Mwenyekiti wa Baraza, Jaji Mstaafu Rose Temba, upande wa mlalamikaji umewakilishwa na Mawakili wa Serikali, Emma Gellan na Hassan Mayunga ambapo hitimisho lilipatikana jana Oktoba 17, 2024.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Honoratus Ishengoma amesema “Baraza limesikiliza utetezi wake (Prof. Sedoyeka), Mwenyekiti amesema baada ya kusikiliza pande zote mbili, litafanya hitimisho na ushauri utapelekwa kunakohusika.”

Pia soma
~
Prof. Eliamini Sedoyeka asomewa tuhuma nne kwenye Baraza la Maadili, azikana zote
~ Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yawasilisha malalamiko kuhusu Prof. Eliamini M. Sedoyeka

MAJIBU YA PROFESA HAYA HAPA
1. Tuhuma ya kuwa na ukaribu na Bw. Hakimu Ndatama na uhamisho wake kurudi IAA pindi mimi niliporejea kuwa Mkuu wa Chuo

Uhamisho wa Bw. Ndatama kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ulifuata taratibu zote za kisheria na kufuatia mahitaji ya kikazi, Chuo kiliandika kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuomba Bw. Ndatama arejeshwe. Hili la kuomba arejeshwe lilifanyika kabla hata ya mimi kurejea IAA kutokana na mahitaji ya kikazi.

2. Tuhuma kuhusu Uteuzi wa Bw. Hakimu Ndatama kuwa Mkuu wa Sehemu

Kuhusu tuhuma ya kutekeleza uteuzi wa Bw. Hakimu Ndatama na mgongano wa maslahi, napenda kueleza kuwa uteuzi huu ulikuwa na msingi mzuri unaozingatia uwezo na ufanisi wake katika utekelezaji wa
majukumu yake.

Nilizingatia sifa za Bw. Ndatama na uwezo wake wa kuchangia maendeleo ya IAA. Nikiwa na dhamira ya kulinda maslahi ya taasisi na kuhakikisha tunapata watu wenye uwezo wa kuchangia katika malengo yetu ya taasisi. Bw. Ndatama si ndugu yangu, si kabila langu, si dini yangu, si rafiki yangu na wala hakuna chochote kinachoniunganisha naye. Sina maslahi naye kwa namna yoyote ile.

3. Zabuni ya Viti na Meza vya Wanafunzi kwa Kampasi ya Babati

Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, Na. 7 ya mwaka 2013), inampa mamlaka Afisa Masuuli kukataa kuendelea na zabuni ama kurejesha zabuni kwenye Bodi ya Zabuni.

Vifungu hivyo vimefafanua kwamba atakapofanya hivyo ataeleza sababu na kupata idhini ya Bodi ya zabuni (Tender Board). Ninaweka wazi msimamo wangu kwamba nilifuata taratibu zote na sikuvunja sheria bali
nilikuwa nikitekeleza majukumu yangu kwa mujibu wa Sheria.

Kama kiongozi mwaminifu kwa nchi yangu, nimekuwa makini kuhakikisha taasisi inapata bidhaa bora kwa njia za uwazi na kwa gharama nafuu kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.

Katika mazingira yote ya manunuzi ya umma, dhamira yangu kama Afisa Masuuli ni kuongeza wigo wa ushindani kwa lengo la kupata thamani halisi ya pesa za Umma (value for money). Hivyo nimekuwa na msimamo wa uwazi na kuzingatia taratibu zinazotakiwa, kwa lengo la kulinda maslahi ya
taifa na kuimarisha taasisi ili iweze kufikia malengo yake ya kutoa elimu bora kwa jamii.

4. Tuhuma kuhusu Uhamisho wa Ndani wa Mtumishi Bw. Robert Mwitango

Kwa ujumla uhamisho wa ndani wa watumishi hufanywa kwa lengo la kuboresha ufanisi wa kiutendaji wa taasisi.

Katika Mwaka wa 2023/2024 Idara ya Maktaba ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo zile ambazo kwa uhalisia wake zilihitaji msaada wa karibu wa kitengo cha Manunuzi ya Umma, kama Stock taking, Asset Verification” na Ununuzi mkubwa wa vitabu kwa mkupuo.

Nilipotathmini ukubwa wa majukumu hayo, unyeti wake na namna yanavyohitaji utaalamu wa manunuzi ya umma, niliamua mtumishi mmoja afanyiwe uhamisho wa ndani kutoka kitengo cha Manunuzi kwenda Idara ya Maktaba.
 
atajua hajui mana walikula kichwa ule ukatibu mkuu wake sasa wanahangaika naye sijui uhamisho sijui nini mbona kuna mafigisu makubwa sana zaidi ya haya huko sirikalini? watu wakihamishiwa sehemu nyingine hasa makatibu wakuu mawaziri na wakuu wa taasisi na mashirika ya umma ni kawaida sana kuhama na watu wao kuanzia madereva secretary etc na wengine hadi mahawara zao, sasa huyu wanavyomwandama nasikia harufu ya siasa chafu hapa.
 
Sio lazima ufurahi, kama huna cha maana unacho deliver una msaada gani?
Je amepunguziwa mshahara?

Au kwa vile ameondolewa kwenye kuiba?
Ww umejuaje Hana Cha maana anacho deliver? What if anazuia ufisadi wa prof asipige madili...
Prof ana hoja ya kujibu acha kumtetea...hapa iundwe timu huru kwenda kuchunguza tuhuma zote za prof
 
Sio lazima ufurahi, kama huna cha maana unacho deliver una msaada gani?
Je amepunguziwa mshahara?

Au kwa vile ameondolewa kwenye kuiba?
Huwajui watawala ww..!!kukusingizia mfanyakazi wa chini kama unambania sehemu ni kugusa tu
 
Back
Top Bottom