Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Kabla hata ya kuyasikia majibu ya NASA kuhusu kauli ya kipumbavu aliyoitoa Uhuru Kenyatta kuwa eti hata Raila akishinda uchaguzi ndani ya miezi mitatu Jubilee wana uwezo wa kumwondoa madarakani [impeach] mimi nilihoji kuwa watamwondoa madarakani kwa kosa gani alilolifanya?
Rais, kwenye nchi za kidemokrasia [kama ambavyo Kenya inapenda kujipambanua] haondolewi madarakani kisa tu watu fulani hawampendi.
Ni lazima awe katenda makosa yanayohalalisha yeye kuondolewa madarakani.
Sasa huyo Uhuru anaropoka tu utadhani mnywa gongo [na si ajabu alikuwa kalewa].
Kwenye hii video hapa chini Moses Wetangula kajibu vizuri sana na kasema kile kile ambacho mimi nilikihoji awali...nacho ni utamuondoa rais Raila toka madarakani kwa kosa/ makosa gani?