Majibu yangu kwa Thadei Ole Mushi alivyouliza, nini kimempata Ndugai?

Majibu yangu kwa Thadei Ole Mushi alivyouliza, nini kimempata Ndugai?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Naheshimu mawazo yako Thadei Ole Mushi,nilijua utatutajia nini kimempata Ndugai lakini umeishia kupamba pambo maua,kupiga maneno na kutuletea maajabu ya Bongo,bongo sihami.Unasema awamu ya tano imeishia kununua wapinzani na kukopa Trillion 29,ninukuu ya Mzee Mwinyi sijui kama nainukuu sawa sawa "tukichukua miaka yetu 30 yeye Rais Magufuli amefanya zaidi yetu sisi wote" hii ni busara kubwa kwako Thadei Ole Mushi,Sina haja ya kutaja Mambo makubwa aliyofanya Rais Magufuli maana kila Mtanzania anajua.

Thadei umesema wenye akili uwa hawashangai kwa nini deni la Taifa linaongezeka,wao ujikita kuangalia kwa nini tumekopa na matumizi sahihi ya mkopo wenyewe,hapa umesema vyema na mfano wa matumizi sahihi ni Awamu ya tano,jua linajua,mvua inajua,mbingu na ardhi zinajua lakini Thadei umejisifia sana kuwa kukopa sio tatizo kwa sababu Marekani imekopa,Uingereza imekopa na China imekopa,Sasa nikufungue akili Thadei Ole Mushi,

Sikatai kuwa na Marekani wanadaiwa but tujiulize Marekani bado inadai nchi nyingi mabilioni ya madeni pia China inaidai karibu bara zima la Africa

Swali.
Sisi Tanzania tunawadai nchi gani?
Ili tufidie Kama China inavyo daiwa madeni bilioni USA 100 afu inadai USA TIRIONI 100

tusijilinganishe na USA ambayo inadai madeni fedha nyingi kuliko wanavyodaiwa

Muulizeni Ole China japo inadaiwa but inadai madeni kiasi gani duniani na Africa?
China ndo waliishikilia bandari ya Singapore kwa miaka 30 kwa kuidai, China ndo wameshika mateka uwanja wa Kampala kwa kudai madeni
China inaidai Kenya mabilioni ya shilingi.

SWALI
Sisi Tanzania tunawadai nchi gani?
na Tirioni ngapi?
Tunadaiwa Tirioni 70, Sasa sisi tunadai nchi nyingine Tirioni ngapi

Endeleeni kujilinganisha na madeni ya marekani na China ambao wao wanadai zaidi kuliko wanavyodaiwa ipo siku nchi itapigwa mnada,namsupport Ndugai ila siungi mkono tozo,Tanzania ni tajiri tukutane 2025.
 
... akiba ya mafuta aliyojiwekea US akiamua kui-release sokoni thamani yake ni mara mia ya madeni yote anayodaiwa ambayo ni pungufu mara mia ya yale anayodai. Halafu utasikia "nguchiro" nao wakijitapa "hata Marekani inadaiwa"; ni kichekesho hasa!
 
Ole anailinganisha Tanzania na Marekani na China, muuluze swali moja tu: wenzetu wanaweza kugeuza mchanga/ udongo kuwa machine je sisi Tanzania tunaweza?

Kutumia karibia theluthi moja ya bajeti ya nchi kulipia mikopo sio jambo zuri hata kidogo. Maana yake itafika hatua tutashindwa kutumia makusanyo ya kodi kwa kutoa huduma badala yake tutaishia kuhudumia deni tu.
 
Halafu kama walikua sahihi kukopa,kwanini walitaka iwe siri nakuwadanganya watanganyika kuwa miladi yote inajengwa napesa zandani? Je kwa maana hii ndomana nape akasema miladi yote na pesa zilizokopwa zichunguzwe ili ijulikane kama pesa yote ilokopwa inaendana na miladi iliopo?
 
Sasa hivi ni vitisho ,mwacheni mama aongoze nchi kwa Uhuru mbona Magufuli haku songwasongwa na akina Ndugai
 
Ole anailinganisha Tanzania na Marekani na China, muuluze swali moja tu: wenzetu wanaweza kugeuza mchanga/ udongo kuwa machine je sisi Tanzania tunaweza?

Kutumia karibia theluthi moja ya bajeti ya nchi kulipia mikopo sio jambo zuri hata kidogo. Maana yake itafika hatua tutashindwa kutumia makusanyo ya kodi kwa kutoa huduma badala yake tutaishia kuhudumia deni tu.
Duh nalo neno
 
Mtu anachukua mkopo wa miaka 20 angali yeye anakaa madarakani miaka 10 unafikiri anayeingia madarakani atalipa ya mwenzake
Kama hujui kitu sio lazima uchangie , ina maana hili la mkopo wa miaka 20 leo ndio umelisikia?!!kuna mikopo ambayo ilichukuliwa enzi za mkapa leo hii ndio ime mature na ni jukumu la serikali hii ya awamu ya 6, kuilipa!!una fikiria hizo karibia bilioni 600, zinazolipwa kila mwezi ku service deni la taifa, ni madeni ya jana?!!na huyo jiwe aliyekuwa anachukua mkopo wenye masharti ya ki biashara ya kuanza kulipa riba ndani ya miezi 6 wakati mradi huo kuja tu kukamilika ni miaka 5, hizo ndio akili??mikopo mingi ya IMF, WB, AFDB, huwa ni ya muda mrefu kulipa.
 
Sawa wewe unayejua ndio utuambie sasa nani atakaye kuja kulilipa ile deni baada ya hiyo miaka 20 maana kila atakayeingia atakopa lake
 
Sawa wewe unayejua ndio utuambie sasa nani atakaye kuja kulilipa ile deni baada ya hiyo miaka 20 maana kila atakayeingia atakopa lake
Ndio maana nimekwambia kwani hilo deni ana kopa rais? hizo trilioni 22, alizokopa meko, si serikali zinazofuata ndio zitalilipa!!, deni la taifa nyie kopeni tu linachanganywa na kuwa moja tu, ila likifikia kiwango fulani, mnaambiwa sasa hamuwezi kukopesheka, hapo ndio balaaa!!!na ndiko tunapo elekea ni suala la muda tu.
 
Sawa wewe unayejua ndio utuambie sasa nani atakaye kuja kulilipa ile deni baada ya hiyo miaka 20 maana kila atakayeingia atakopa lake
Mbona amekuelewesha vizuri kabisa.Tatizo ni nini?Ukiona rais anakopa na deni lilipwe baada ya miaka 20 huyo ana akili kwa sababu kiuchumi mradi ulioombwewa mkopo ni budi uanze kufanya kazi na ikiwezekana ujilipie wenyewe hilo deni.Huyo mtu wenu ambaye alikuwa anasema kuwa tunatumia fedha zetu za ndani wakati ndiye aliyekopa kuliko wengine wote.Kwa ujuaji wake amechukua mikopo ya kibiashara yenye masharti magumu na marejesho baada ya muda mfupi.Unakuta deni limeanza kulipwa wakati mradi hata nusu haujafika.
 
Pro Magufuli mlikuwa mnajitamba humu mnajenga kwa fedha za ndani, kumbe mlikuwa mnakopa.Mama kaja kusema ukweli mnaanza kulialia humu.
 
Back
Top Bottom