Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

sisi akina mwinika zeze kwetu sio jiji?
 
Kwann unasema hvyo, japo sijawahi kuishi moro zaidi ya kupita tu na one day trips na kurudi dar.

Tupe experiences tuachane na comments za JF.
Kwa sasa kuna changamoto kdg hasa miundombinu kama vile barabara na majengo. Nafikiri kuna haja ya mamlaka husika kufanya uboreshaji zaidi ili mji uvutie zaidi kama ilivyokua mwanzo..
 
Maisha ya mtandaoni tofauti na uhalisia watu wapo fake Sana kila kitu ila ukweli Tanga City ni mji mzuri Sana mgeni ukija utapenda kuishi bandari sahiv inafanya kazi masaa yote inapokea meli kubwa zaidi tofauti na miaka ya nyuma watu wameongezeka Sana .tanga kuna fursa nyingi sana hasa za viwandani .Siipi sifa tanga zisozostahili ila nawakaribisha Sana muje muone Jiji ambalo lina barabara zinazounganisha mitaa yote mjini kwa kiwango cha lami na taa za barabarni hakuna jiji lenye sifa hii pia huduma ya maji safi tanga City hakuna jiji linalofikia huduma kma sewage system tanga ni kubwa hii toka mjerumani na nyengine zimeboreshwa .Tanga kuna ongezeko kubwa la watu tofauti na awali pia halmashauri ya Jiji la tanga imeibuka kidedea kwenye ukusanyaji mapato Tanzania mwezi ulopita wa pili walipewa tuzo hiyo ,pia ni jiji ambalo limepangiliwa vizuri kuliko majiji yote Tanzania kimiundombinu .mzunguko wa pesa Tanga umeongezeka Sana tofauti na awali kama ulifika tanga miaka ya nyuma kuanzia 2020 au 2019 sikupindi kuiponda kuhusu mzunguko wa pesa .. Karibuni Tanga City muone uhalisia msidanganyane mitandaoni ukija ukae ufanye survey mwenyewe nina uhakika utaelewa nini nilimasnisha alafu hayo magofu ya mjerumani yamepigwa service yote hadi reli inafanya kazi kubeba mizigo . Narudia tena Tanga hakuna magofu tena kama mwanzo halmashauri ina watu makini sahivi na wazalendo kwa ambao hamkuja muda mrefu mkija mtashangaa Sana . Viwanda vya saruji vinazidi ongezeka kama Huaxin popote Tanzania hawa wachina unapata bidhaa zao ukienda pale kiwandani mwao utakuta magari makubwa zaidi ya 200 kila siku yanatoa mizigo mikubwa mno kutoka nchi mbali mbali Bandari ya Tanga inazidi kufanyiwa marekebisho ya hali ya juu sana vitendea kazi vimeongezwa na bandari kupanuliwa Tanga ndiyo Jiji ambalo limepanga hadi maeneo yapi ya viwanda na maeneo yapi ya makazi huwezi jenga hovyo hovyo mjini kati kulikuwa na nyumba za hovyo sahiv wameuza wenyeji wamepisha wawekezaji hakuna nyumba za makuti tena .watu wanauza kwa mamilioni wanaruhusu wawekezaji wapya .Hakuna Jiji lenye miundombinu bora ya majitaka na maji safi ambayo mtumiaji huweza kunywa moja kwa moja bila kuchemsha pia huduma ambayo inamuwezesha kila mtu kupata huduma kwa wakati barabara kila hatua kadhaa Tanga hakutakuja tokea foleni Tanga kuna sehemu kuna lami hata hazitumiki vituo vya afya vimeongezwa Sana Pongezi kwa halmashauri ya Jiji na Mheshimiwa Ummy hakika amesaidia Sana Tanga City. Tanga hakuna magorafa mengi wala makubwa sana kama DSM ila ina miundombinu mizuri na bora Sana Karibuni muone uhalisia ulivyo msipotoshwe jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
View attachment 2139742View attachment 2139744View attachment 2139743View attachment 2139745
 
Sawa tumekusikia tutafika Tanga.

#MaendeleoHayanaChama
 
Asante Mkuu kwa nyongeza natumaini wadau wataona fursa katika jiji hilo la Tanga.
 
Miji yote ni hovyo imechafuliwa na wamachinga na miundo mbinu kama barabara za wapita njia hakuna kabisa.

This entire country is just one pile of a fucking shith0le.
Yet you live in that shit hole? Then you are the shit itself
 
Nawakumbusha Tanga City kuna kiwanda cha kutengeneza vocha za mitandao ya simu tena cha kimataifa East Africa hakuna ukanda wetu wa Africa sub Saharan nadhan kama vipo vingine basi Nigeria na South Africa pekee Tanzania kipo Tanga City
 
Nawakumbusha ujio mwengine wa kiwanda kikubwa cha utengenezaji wa kadi za kibenki kimbo mbioni kuanza kazi hapa Jiji la tanga ni cha kimataifa pia
 
Nawakumbusha Mradi wa Bomba la mafuta umeanza hapa Jiji la tanga maeneo ya chongoleani
 
Mradi wa uboreshaji wa bandari ya Tanga kwa awamu ya pili wa ujenzi wa gati la kwanza na pili umefikia katika asilimia 26 ambapo matarajia ya kukamilika kwake ni Oktoba ,16,2022.
 
Mhandis Kipalo alisema mradi huo utaleta manufaa kwa wananchi na wafanyabiashara katika kuongeza ufanisi wa bandari kutoka tani laki saba na nusu hadi milioni tatu ambapo uwezo wa bandari utaongezeka na kufanyika haraka tofauti na mwanzoni.
 
Nawakumbusha Tanga City kuna kiwanda cha kutengeneza vocha za mitandao ya simu tena cha kimataifa East Africa hakuna ukanda wetu wa Africa sub Saharan nadhan kama vipo vingine basi Nigeria na South Africa pekee Tanzania kipo Tanga City
Kumbe vocha zinatengeneza Tanga.
 
Mhandis Kipalo alisema mradi huo utaleta manufaa kwa wananchi na wafanyabiashara katika kuongeza ufanisi wa bandari kutoka tani laki saba na nusu hadi milioni tatu ambapo uwezo wa bandari utaongezeka na kufanyika haraka tofauti na mwanzoni.
Asante kwa kutujuza kumbe Tanga mambo ni 🔥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…