Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

Kama hauko Dom,Dar na Arusha huna cha kuizingua Mbeya.

Mbeya kuna vyuo vikuu na koleji/kampani takribani 10 ,huwezi kuta kwenye kijiji cha Mwanza
Uwe unasoma na kuelewa nilichoandika, unajibu Kama umepasuka kichwa.

Nakwambia lete city plan , sewage stystem, Transport network ya jiji.

Unakuwa mshamba wa maghorofa na Vyuo eti ndio uzuri wa miji.

Nyie mbona washamba Sana.
 
Hii hapa ni orodha ya Miji mizuri Tanzania.
1-Dar es Salaam (Mzizima)
Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani.

Ni km² 1,800 pamoja na visiwa vidogo 8 na eneo la bahari kati ya pwani na visiwa hivi. Eneo la nchi kavu pekee ni km² 1,393.

Kuna wilaya tano: Kinondoni (wakazi 1,775,049), Ilala (wakazi 1,220,611) na Temeke (wakazi 1,368,881) ambazo zimeongezewa Kigamboni na Ubungo. Kila moja inaangaliwa kama mji. Takwimu hizi ni za mwaka 2012, kwa ujumla idadi ya wakazi ilikuwa 4,364,541.

Wakazi asili wa eneo la mkoa walikuwa Wazaramo pamoja na makabila madogo kama vile Wandengereko na Wakwere. Kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji kuna makabila yote ya Tanzania.

2-Mwanza (Rocky city)
Jiji la Mwanza ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mwanza. Mji upo kando la ziwa Viktoria Nyanza Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 378,327 (ukijumlisha wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na sehemu za Wilaya ya Ilemela).

3-Arusha (A city)
Arusha ni jiji la kaskazini mwa Tanzania na makao makuu ya Mkoa wa Arusha. Kiutawala eneo la jiji la Arusha ni sawa na eneo la Wilaya ya Arusha Mjini. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 416,442

4-Dodoma (Idodomya)
Ilitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973, lakini mnamo tarehe 26 Aprili 2018 katika maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano John Magufuli aliupandisha hadhi na kutangaza rasmi kuwa Dodoma ni Jiji. Serikali ya awamu ya tano ilihamia rasmi jijini Dodoma mwaka 2016.

Jiji hili pia ni makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na eneo lake linahesabiwa kama Wilaya ya Dodoma .

Eneo la mji liko mita 1135 juu ya usawa wa bahari UB. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji wa Dodoma ulikuwa na wakazi wapatao 410,956 waishio humo.

5-Mbeya (Green city)
Mbeya ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Tanzania. Idadi ya wakazi imehesabiwa kuwa 385,279 katika sensa ya mwaka 2012. Wengine 300,000 hivi wanaishi katika mazingira karibu na Mbeya mjini.

Kiasili Mbeya ilikuwa eneo la Wasafwa. Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa Wasafwa pamoja na makabila ya Wanyakyusa kutoka wilaya za Rungwe na Kyela, Wanyiha kutoka Mbozi, Wandali kutoka Ileje na Wakinga kutoka Makete.

Tazama zaidi video ya mandhari ya majiji hayo.


MOROTOWN na DODOMA wapi pametulia?
 
Tanzania nzima hakuna barabara iliyopita juu kileleni mlimani kama hii.. ipo mbeya
afu bado uko juu watu wacheza mashindano ya magri(drift)
njo tar 20/6 uone drift zitavuopigwaView attachment 1818228View attachment 1818229
295ca95969a659ac4482818a5dd9c4dd.jpg
View attachment 1818230
 
Uwe unasoma na kuelewa nilichoandika, unajibu Kama umepasuka kichwa.

Nakwambia lete city plan , sewage stystem, Transport network ya jiji.

Unakuwa mshamba wa maghorofa na Vyuo eti ndio uzuri wa miji.

Nyie mbona washamba Sana.
Tayari masterplan ya jiji iliandaliwa na ilipitishwa na wizara ya ardhi na inaendelea kutekelezwa
 
Mkuu Mwanza ni heavy weight City Mbeya ni pazuri ila Lock City ni Noma pia mzunguko wa hela katika ya Mbeya na Mwanza ni tofauti Mwanza lile ziwa linatema sangara si mchezo na kuuzwa viwandani, pia mikoa inayozunguka ina madhahabu ya kutosha na matajiri wote wanaenda kuwekeza Mwanza yaani Geita,Shinyanga, Mara, Simiyu, kiujumla uchumi wa Mbeya ni kilimo cha mpunga, mahindi na viazi mviringo tukisema madini ule mgodi wa Chunya ni wa kawaida tu.
Hizo ni kelele za kunyanyua mabega juu,huko kumejaa maskini afu sijui mnaongea nini.Mwaka 2019 Mauzo ya mazao ya horticulture kutoka Arusha,Njombe,Iringa na Mbeya yalikuwa namba 3 kuingiza pesa nyingi za kigeni nyuma ya dhahabu na utalii .Sasa dhahabu inatoka kwa makampuni makubwa wanufaika ni wachache,the same kwenye utalii.

Wakati mazo ya horticulture yanatoka kwa wakulima wadogo wadogo ,pesa zinawanufaisha moja kwa moja matokeo yake huko Lake zone watu wanajipiga kifua wakati wanazidi kuwa maskini.Ndio maana lake zone haitakaa iache kuongoza kwenye umaskini Tzn hii.
 
Tayari masterplan ya jiji iliandaliwa na ilipitishwa na wizara ya ardhi na inaendelea kutekelezwa
Hivi unaelewa unachokijibu kweli wewe...

Zile slams zilizojaa mbeya huzioni ?

Huoni machinga kila sehemu ?

Au hujui Mpango Miji ni Hadi suala la machinga kushughulikiwa na wakae wanapostahili. Hii akili ya kudhani mipango miji Ni kuwa na maghorofa marefu na Barabara ni upumbavu umewajaa viongoz sampuli yako.


Nasikitika hujui lolote na huna exposure ya kuzurura miji kadhaa nje ya Tanzania , naamini ungekuja kufuta Mambo mengi unayoandika humu.
 
Wajinga hao wamezaliwa na kukulia Dar hakuna wakijuacho.

Wengine Wana picha za 2014 na kipindi kile wanadanganywa eti ooh Mbeya hakuruhusiwi majengo marefu sijui tetemeko sijui maji na blaa blaa kibao

Kwa taarifa yao Mbeya ya sasa imeendelea na ni Jiji kubwa kuna kila kitu kinachopatikana kwenye majiji mengine.

Tuna changamoto ya barabara tuu ambayo nayo inamalizwa kabla ya 2025

1 Dar
2 Mwanza
3 Mbeya
4 Arusha
5 Dom


Dom inakua kwa kasi, baada ya miaka kadhaa mbele itamfunika Arusha, na Arusha kushuka hadi nafasi ya 5.


Mbeya pazuri sana, ile green ya pale na waterfalls dah
 
ndani ya kona za mkoa mbeya
 
Mwaka 2021 bado unajivunia lift ?

Nimetoka tanga mwaka jana November nimeona Nyumba za nyasi na tope tanga mjini Tena jijini.

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Wewe hukuja Tanga Jiji,umeishia vijijini,kwanza Kama ni Tanga Jiji,hata ingekuweko nyumba,sio ya nyasi ungesema ya makuti,ndio wanatumia kwenye Bar na Mahoteli,baadhi sana,kama vivutio vya utalii,na kupunguza joto.Wewe hujafika Tanga Port City.
Port City,ndio inabeba maendeleo ya majiji mengine,huwezi ku import mafuta ya magari na mitambo(viwanda),kutoka kokote duniani,bila kupitia Port City.
Tanga Port City kuna Bandari kubwa za mafuta kutoka nje,ukifika hapo,jinsi kulivyojengwa,na jinsi inavyoingiza pato la Taifa kwa kodi,na bado Bandari za kawaida zinazosafirisha bidhaa nje na kuingiza nchini,ambazo hizo bidhaa huko unakoita majiji,wanategemea mafuta ya magari na Bidhaa nyingine,zishushwe kutoka Port City,ndio wao wapate,utaona,huko kote hakufai.Port City,sio mchezo

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Point yako ni Nini Sasa mbona uko kinyume na mada

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Siko kinyume na Mada.Port city Huwezi kulinganisha na majiji yasio na Bandari za Bahari(Port City).Hayo majiji mengine yote,maendeleo yao,yanategemea Port City(Dar,Tanga).Kama mafuta ya magari na mitambo,bila kwenda kuchukuwa Dar au Tanga,hao majiji mengine,hayawezi kuwa na maendeleo.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom