Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

We ni mjinga Sana kwani Mwanza haina Bandari ?

Mbeya haina Bandari ?

Kigoma haina Bandari ?

Rukwa haiana Bandari ?

Wewe kwako Bandari ni nini!
Wewe ndio mjinga,tunaongelea Bandari za Bahari,sio Bandari za Maziwa.Bandari za Bahari zinaunganisha Majiji ya Dunia nzima.Wewe wasema Bandari za maziwa,zinazounganisha mikoa na miji ya nchi jirani.Hizo Bandari za Maziwa,ulisikia zikipokea shehena za mafuta ya magari na mitambo,au kupokea vichwa vya train kutoka Ulaya.
Au hizo Bandari za Maziwa,ulisikia,wakisafirisha kwenda soko la Dunia,mazao ya biashara kama kahawa,pamba,katani nk

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
We jamaa naona umekazania port city,kwani kati ya Nairobi na Mombasa lipi ni jiji kubwa!!! Mbona Nairobi ambayo sio port city imeiacha mbali Mombasa!! Sijakuelewa kabisa
Sio kweli,Mombasa kuwa na Bandari,imeiacha nyuma sana Nairobi,Nairobi haiwezi kujiendesha bila kutegemea Mombasa,kwa mafuta ya magari,mafuta ya mitambo,kusafirisha bidhaa,kupokea bidhaa nk

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Majiji ni Dar na Tanga(Port City),Jiji lenye Bandari ya Bahari,ndio Jiji.Miji yote inategemea Port City ,kupokea bidhaa na kusafirisha

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Mkuu inatakiwa Mwanza, Arusha, Mbeya na dodoma zikose sifa ya kua jiji na kupewa mikoa yenye port kama Lindi au Mtwara
 
Mkuu nimesoma sana replies zako.
Hapo ulicho tetea ni port city tu kwahiyo serikali ifanye namna city zisizo na bandari ya bahari zitaifishwe sifa ya kua jiji.
Ninachomaanisha,Majiji yenye Bandari za Bahari,Port City,ndio ziwe namba moja.Kwasababu majiji yote yanategemea haya majiji yenye Bandari za Bahari,kukuza uchumi wao,kwa kusafirisha bidhaa na kupokea bidhaa.Kwa mfano mafuta ya magari,yana umuhimu wa kwanza,bila kupitia Bandari za Bahari,ingekuwa shida kubwa,na vile vile kupokea bidhaa na kusafirisha mazao kwenye masoko ya kimataifa ingekuwa tabu.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Ninachomaanisha,Majiji yenye Bandari za Bahari,Port City,ndio ziwe namba moja.Kwasababu majiji yote yanategemea haya majiji yenye Bandari za Bahari,kukuza uchumi wao,kwa kusafirisha bidhaa na kupokea bidhaa.Kwa mfano mafuta ya magari,yana umuhimu wa kwanza,bila kupitia Bandari za Bahari,ingekuwa shida kubwa,na vile vile kupokea bidhaa na kusafirisha mazao kwenye masoko ya kimataifa ingekuwa tabu.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Lakini na majiji mengine yanaumuhimu sana katika kuchangia mapato ya Taifa.
Ukiitoa Dar ambayo ni port city kwa kuchangia mapato Tanga haingii ndani zaidi ya majiji hayo mengine unayo zalau
 
Yeye anaongelea Bandari ya bahari tu.
Mfahamishe,mimi naongelea Bandari za kimataifa,za Bahari.Bandari hizi ndio zinaunganisha Majiji yote ya Dunia.Aliyeko Jiji la Mwanza,Arusha,Mbeya,Dodoma,hawezi kupokea bidhaa kutoka nje,kuanzia mafuta,magari,vifaa vya ujenzi vya nje,bila kupitia Bandari za majiji ya Bandari(Port city?) Na pia hawezi kusafirisha mazao ya kibiashara, katika soko la kimataifa bila kupitia Bandari za Majiji ,za Bahari sio maziwa.

Hapa hadi waje watalamu wa haya mambo maana nahisi nikibishana sana nitaharibu.
Ngoja wataalamu waje.
 
Lakini na majiji mengine yanaumuhimu sana katika kuchangia mapato ya Taifa.
Ukiitoa Dar ambayo ni port city kwa kuchangia mapato Tanga haingii ndani zaidi ya majiji hayo mengine unayo zalau
Tanga inachangia sana pato la Taifa kupitia Bandari ya kusafirisha mazao nje na kupokea bidhaa kutoka nje,Bandari za kushusha mafuta ya magari na mitambo,ukichukuwa Bandari inayoshusha mafuta ya kampuni moja tu,ni mapato ya majiji yote yasio na Bandari,wakati kampuni tofauti zinazoshusha mafuta..Hapo hatujagusa maingizo ya mpaka,baina ya Tanzania na Kenya.Na bado kuna bomba la mafuta,linakuja kutoka Uganda,DRC,Sudani ya kusini.Hatujaingiza mapato ya mazao biashara,kama katani(white gold,green gold).

Ila Bandari isiwe kigezo mkuu maana kuna kwenye uchangiaji pato la taifa Mwanza ipo vizuri zaidi ya Tanga
 
Ila Bandari isiwe kigezo mkuu maana kuna kwenye uchangiaji pato la taifa Mwanza ipo vizuri zaidi ya Tanga
Tanga ni zaidi,lazima ujuwe Jiji la Tanga,ni wilaya ya Tanga,katika mkoa wa Tanga.Wilaya zilizobakia sio Jiji.Ni wilaya moja tu ndio Jiji,katika mkoa wa Tanga,ni wilaya ya Tanga,sio mkoa mzima wa Tanga ni Jiji.Kwa hiyo ukisikia mapato ya jiji la Tanga,ni wilaya ya Tanga,sio mkoa mzima.Hapo hakujajumlishwa mapato ya wilaya nyingine.Wengi hufikiria Jiji ni mkoa mzima wa Tanga.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Buhongwa hadi mjini Kati kuna barabara ngapi?

Kwangu mimi barabara kama haijawa separated katikati huwezi ita ni dual carriage ni utopolo tuu as usual na huwa hazipendezi.

Ndio maana hata Arusha ina barabara kali kuliko kijiji kikubwa cha Mwanza..Mbeya na Mwanza kuna tofauti gani hasa?

By the way barabara zitajengwa kabla ya 2025
Hahaaa
Umesha anza chuki zako mzee na mwanza
Inshort mwanza inakupa muhaho na mtero
Hiyo barabara ya buhongwa to cty center ndo pekee one way zingine ni 3way na 4way
Afu usifananishe mbeya ,arusha na mwanza
We huoni hata ziara za rais zinafanyikia wapi sana?
Huoni miradi mikubwa iliyozinduliwa na iliyoko tayar?
Unauliza mwanza kuna nn hahahaa
Kuna dhahabu,samaki,reli ya kisasa,jpm bridge hivi vyote havipo mbeya na arusha.
 
Weka picha za current achana na hizo za kitambo za ku google.

Kwani huo uwanja umekamilika? Si bado unaendelea kujengwa? Watu wa Mbeya kamwe hawawezi kulamba matako ya mtu maana kwa Viwango vya maisha tuko juu ya huko kwenu
Umekamilika bhana
Acha porojo zako
 
Kama hauko Dom,Dar na Arusha huna cha kuizingua Mbeya.

Mbeya kuna vyuo vikuu na koleji/kampani takribani 10 ,huwezi kuta kwenye kijiji cha Mwanza
Vyuo si maendeleo
Nyie mlionanvyo vingi vinawasaidiaje maana havisomeshi wana mbeya tu ni tz yote pengine hata wazawa wa mbeya hawasomei huko
 
Hii hapa ni orodha ya Miji mizuri Tanzania.
1-Dar es Salaam (Mzizima)
Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani.

Ni km² 1,800 pamoja na visiwa vidogo 8 na eneo la bahari kati ya pwani na visiwa hivi. Eneo la nchi kavu pekee ni km² 1,393.

Kuna wilaya tano: Kinondoni (wakazi 1,775,049), Ilala (wakazi 1,220,611) na Temeke (wakazi 1,368,881) ambazo zimeongezewa Kigamboni na Ubungo. Kila moja inaangaliwa kama mji. Takwimu hizi ni za mwaka 2012, kwa ujumla idadi ya wakazi ilikuwa 4,364,541.

Wakazi asili wa eneo la mkoa walikuwa Wazaramo pamoja na makabila madogo kama vile Wandengereko na Wakwere. Kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji kuna makabila yote ya Tanzania.

2-Mwanza (Rocky city)
Jiji la Mwanza ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mwanza. Mji upo kando la ziwa Viktoria Nyanza Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 378,327 (ukijumlisha wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na sehemu za Wilaya ya Ilemela).

3-Arusha (A city)
Arusha ni jiji la kaskazini mwa Tanzania na makao makuu ya Mkoa wa Arusha. Kiutawala eneo la jiji la Arusha ni sawa na eneo la Wilaya ya Arusha Mjini. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 416,442

4-Dodoma (Idodomya)
Ilitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973, lakini mnamo tarehe 26 Aprili 2018 katika maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano John Magufuli aliupandisha hadhi na kutangaza rasmi kuwa Dodoma ni Jiji. Serikali ya awamu ya tano ilihamia rasmi jijini Dodoma mwaka 2016.

Jiji hili pia ni makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na eneo lake linahesabiwa kama Wilaya ya Dodoma .

Eneo la mji liko mita 1135 juu ya usawa wa bahari UB. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji wa Dodoma ulikuwa na wakazi wapatao 410,956 waishio humo.

5-Mbeya (Green city)
Mbeya ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Tanzania. Idadi ya wakazi imehesabiwa kuwa 385,279 katika sensa ya mwaka 2012. Wengine 300,000 hivi wanaishi katika mazingira karibu na Mbeya mjini.

Kiasili Mbeya ilikuwa eneo la Wasafwa. Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa Wasafwa pamoja na makabila ya Wanyakyusa kutoka wilaya za Rungwe na Kyela, Wanyiha kutoka Mbozi, Wandali kutoka Ileje na Wakinga kutoka Makete.

Tazama zaidi video ya mandhari ya majiji hayo.

Karibu sana Mbeya sisi huku tuna upendo wa dhati hatuna unafki kabisa na ukituzingua tunakuzingua vilevile utani asili yetu.😅😅
 
Hizo ni kelele za kunyanyua mabega juu,huko kumejaa maskini afu sijui mnaongea nini.Mwaka 2019 Mauzo ya mazao ya horticulture kutoka Arusha,Njombe,Iringa na Mbeya yalikuwa namba 3 kuingiza pesa nyingi za kigeni nyuma ya dhahabu na utalii .Sasa dhahabu inatoka kwa makampuni makubwa wanufaika ni wachache,the same kwenye utalii.

Wakati mazo ya horticulture yanatoka kwa wakulima wadogo wadogo ,pesa zinawanufaisha moja kwa moja matokeo yake huko Lake zone watu wanajipiga kifua wakati wanazidi kuwa maskini.Ndio maana lake zone haitakaa iache kuongoza kwenye umaskini Tzn hii.
Numbers dont lie
Screenshot_20210613-232943_Twitter.jpg
 
Back
Top Bottom