Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

Tanga inachangia sana pato la Taifa kupitia Bandari ya kusafirisha mazao nje na kupokea bidhaa kutoka nje,Bandari za kushusha mafuta ya magari na mitambo,ukichukuwa Bandari inayoshusha mafuta ya kampuni moja tu,ni mapato ya majiji yote yasio na Bandari,wakati kampuni tofauti zinazoshusha mafuta..Hapo hatujagusa maingizo ya mpaka,baina ya Tanzania na Kenya.Na bado kuna bomba la mafuta,linakuja kutoka Uganda,DRC,Sudani ya kusini.Hatujaingiza mapato ya mazao biashara,kama katani(white gold,green gold).

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Acha porojo wewe ,Tanga ni kama kivuko tuu,uliwahi ona wapi mkoa wa Tanga uko top 5 ya kuchangia GDP ya Taifa?
 
Tanga ni zaidi,lazima ujuwe Jiji la Tanga,ni wilaya ya Tanga,katika mkoa wa Tanga.Wilaya zilizobakia sio Jiji.Ni wilaya moja tu ndio Jiji,katika mkoa wa Tanga,ni wilaya ya Tanga,sio mkoa mzima wa Tanga ni Jiji.Kwa hiyo ukisikia mapato ya jiji la Tanga,ni wilaya ya Tanga,sio mkoa mzima.Hapo hakujajumlishwa mapato ya wilaya nyingine.Wengi hufikiria Jiji ni mkoa mzima wa Tanga.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Hii nchi imejaa watu wenye mihemko na wajinga mko radhi kubisha hadi Takwimu sahihi zilizopo ila mkashadidia hisia zenu binafsi

Umeambiwa Mkoa wa Tanga haipo hata top 5 ya mikoa inayochangia zaidi Pato la Taifa unabisha,humu ndani kuna uzi utafute uusome.
 
Hii hapa ni orodha ya Miji mizuri Tanzania.
1-Dar es Salaam (Mzizima)
Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani.

Ni km² 1,800 pamoja na visiwa vidogo 8 na eneo la bahari kati ya pwani na visiwa hivi. Eneo la nchi kavu pekee ni km² 1,393.

Kuna wilaya tano: Kinondoni (wakazi 1,775,049), Ilala (wakazi 1,220,611) na Temeke (wakazi 1,368,881) ambazo zimeongezewa Kigamboni na Ubungo. Kila moja inaangaliwa kama mji. Takwimu hizi ni za mwaka 2012, kwa ujumla idadi ya wakazi ilikuwa 4,364,541.

Wakazi asili wa eneo la mkoa walikuwa Wazaramo pamoja na makabila madogo kama vile Wandengereko na Wakwere. Kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji kuna makabila yote ya Tanzania.

2-Mwanza (Rocky city)
Jiji la Mwanza ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mwanza. Mji upo kando la ziwa Viktoria Nyanza Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 378,327 (ukijumlisha wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na sehemu za Wilaya ya Ilemela).

3-Arusha (A city)
Arusha ni jiji la kaskazini mwa Tanzania na makao makuu ya Mkoa wa Arusha. Kiutawala eneo la jiji la Arusha ni sawa na eneo la Wilaya ya Arusha Mjini. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 416,442

4-Dodoma (Idodomya)
Ilitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973, lakini mnamo tarehe 26 Aprili 2018 katika maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano John Magufuli aliupandisha hadhi na kutangaza rasmi kuwa Dodoma ni Jiji. Serikali ya awamu ya tano ilihamia rasmi jijini Dodoma mwaka 2016.

Jiji hili pia ni makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na eneo lake linahesabiwa kama Wilaya ya Dodoma .

Eneo la mji liko mita 1135 juu ya usawa wa bahari UB. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji wa Dodoma ulikuwa na wakazi wapatao 410,956 waishio humo.

5-Mbeya (Green city)
Mbeya ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Tanzania. Idadi ya wakazi imehesabiwa kuwa 385,279 katika sensa ya mwaka 2012. Wengine 300,000 hivi wanaishi katika mazingira karibu na Mbeya mjini.

Kiasili Mbeya ilikuwa eneo la Wasafwa. Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa Wasafwa pamoja na makabila ya Wanyakyusa kutoka wilaya za Rungwe na Kyela, Wanyiha kutoka Mbozi, Wandali kutoka Ileje na Wakinga kutoka Makete.

Tazama zaidi video ya mandhari ya majiji hayo.

Toa mwanza aisee,ipo wap moshi
 
Yan Mwanza Ni ya Tano kwa umaskini Tanzania Halafu hiwe nzuri [emoji23][emoji23] na Moshi utasemaje Ambayo hipo kilimanjaro[emoji23]
images%20(1).jpg
 
Kuna beach gani nzuri...?!
Kuwe na beach kwani kuna ziwa au bahari? Mwanza kungekuwa na beach nzuri si mungeongoza kwa utalii wa beach kama Zanzibar?

Hakuna kitu huko cha maana,kwa mfano siwezi funga safari kuja Mwanza kwa sababu sina cha maana kuja kuangalia.

Mara mia niende Dom nitazunguka hata Mji kuona ikulu, barabara za mzunguko,projects nyingi za kupanga Mji nk

Bora niende hata Mbeya ni drive ile road ya kuelekea Chunya nione zile Kona kali na mandhari ya kuvutia ya mlima kawetele na Mbeya.
 
Hahaaa
Umesha anza chuki zako mzee na mwanza
Inshort mwanza inakupa muhaho na mtero
Hiyo barabara ya buhongwa to cty center ndo pekee one way zingine ni 3way na 4way
Afu usifananishe mbeya ,arusha na mwanza
We huoni hata ziara za rais zinafanyikia wapi sana?
Huoni miradi mikubwa iliyozinduliwa na iliyoko tayar?
Unauliza mwanza kuna nn hahahaa
Kuna dhahabu,samaki,reli ya kisasa,jpm bridge hivi vyote havipo mbeya na arusha.
Weka barabara kama za Arusha Acha porojo za kipuuzi
 
Mkuu Mwanza ni heavy weight City Mbeya ni pazuri ila Lock City ni Noma pia mzunguko wa hela katika ya Mbeya na Mwanza ni tofauti Mwanza lile ziwa linatema sangara si mchezo na kuuzwa viwandani, pia mikoa inayozunguka ina madhahabu ya kutosha na matajiri wote wanaenda kuwekeza Mwanza yaani Geita,Shinyanga, Mara, Simiyu, kiujumla uchumi wa Mbeya ni kilimo cha mpunga, mahindi na viazi mviringo tukisema madini ule mgodi wa Chunya ni wa kawaida tu.
Lock?wat[emoji23]
 
Umekamilika bhana
Acha porojo zako
Huelewi kitu acha makelele,kama umekamilika mitambo ya mkandarasi inafanya nini pale?

Serikali bado inaweka tabaka la runway nyingine na kuondoa la zamani au kufanya overlay maana wajenzi wa awali walijenga chini ya Kiwango.

Pili wanamalizia ujenzi wa maeneo ya parking za ndege,kufunga radar,kujenga cold Room,VIP lounge na Kazi zingine ndogo ndogo.

Uwe unafuatilia bajeti za kisekta zinaposomwa na mawaziri husika sio kupayuka wakati huna data
 
Vyuo si maendeleo
Nyie mlionanvyo vingi vinawasaidiaje maana havisomeshi wana mbeya tu ni tz yote pengine hata wazawa wa mbeya hawasomei huko
Vinavuta huduma na biashara zingine kuanzishwa,vinaongeza mzunguko wa pesa jijini na vinaleta hadhi ya Jiji kwamba ni la kitaaluma.

Mwisho tunapata varieties za watoto wakali kutoka pande zote za Nchi
 
Shida ya jiji la mbeya halipendezi katikati ya mjini nyumba zimejengwa Kwa tofali mbichi halafu hazijapigwa plasta. Katika miji mingi niliyotembea Tanzania mbeya ndio jiji pekee tatikati ya mji nyumba zimejengwa Kwa tope
Acha porojo mkuu kwani kama tofari mbichi hazifanyi nyumba kuanguka tatizo lako nini?

Pili aliyekwambia Mbeya ya zamani bado iko vilevile ni nani?

Na kinachofanya wengi kupuuza ni ufinyu wa miundombinu ya barabara ambayo nayo itakuwa worked before 2025 ,dual carriage road zitajengwa na bypass 2 na kuzidi kuboresha za mitaani kwa hiyo hiyo picha itabadilika.

Mwisho Yale mashamba ya chuo cha kilimo Uyole yakichukuliwa na Jiji/Manispaa ya Uyole na kuendelezwa kimakazi ,Mbeya itakuwa vizuri kuliko Miji Mingi ya Tzn hii.
 
Nilichogundua wewe jamaa una chuki kali sana,kama una uwezo wa kujipima pia una ukabila sana,sasa shida umeanzaje kuwashambulia Mbeya kwa ukabila,huu umeanzishwa kama mjadala tu,lakini maneno ni makali mno kuhusu Mbeya tu,wamekukosea nini mzee,hata vigezo vya mji kupandishwa hadhi huvijui kwa vigezo vyako ni makabila,najua utakuwa povu pole sana
Achana na mjinga huyo anakupotezea time kumjibu
 
Huelewi kitu acha makelele,kama umekamilika mitambo ya mkandarasi inafanya nini pale?

Serikali bado inaweka tabaka la runway nyingine na kuondoa la zamani au kufanya overlay maana wajenzi wa awali walijenga chini ya Kiwango.

Pili wanamalizia ujenzi wa maeneo ya parking za ndege,kufunga radar,kujenga cold Room,VIP lounge na Kazi zingine ndogo ndogo.

Uwe unafuatilia bajeti za kisekta zinaposomwa na mawaziri husika sio kupayuka wakati huna data
Uwanja unatumia miaka 10 kujengwa?
Bas tungesema hata ni international airport kwamba kuna buildings kali za maana zinajengwa.
Cha ajabu ni jengo mfano wa kichuguu haha
Mnafurahisha na hicho kijiji chenu aisee
 
Vinavuta huduma na biashara zingine kuanzishwa,vinaongeza mzunguko wa pesa jijini na vinaleta hadhi ya Jiji kwamba ni la kitaaluma.

Mwisho tunapata varieties za watoto wakali kutoka pande zote za Nchi
Hebu taja huduma vilizo vutwa mbeya kukaifanya itishe kuliko majiji mengine
Mnafika hadi hatua za kujisifia vyuo kwakwel dawa imewaingia na ukitoa TEKU na MUST vingine ni branches na collages haya hivyo vyuo vingi vipo wap?
 
Acha porojo mkuu kwani kama tofari mbichi hazifanyi nyumba kuanguka tatizo lako nini?

Pili aliyekwambia Mbeya ya zamani bado iko vilevile ni nani?

Na kinachofanya wengi kupuuza ni ufinyu wa miundombinu ya barabara ambayo nayo itakuwa worked before 2025 ,dual carriage road zitajengwa na bypass 2 na kuzidi kuboresha za mitaani kwa hiyo hiyo picha itabadilika.

Mwisho Yale mashamba ya chuo cha kilimo Uyole yakichukuliwa na Jiji/Manispaa ya Uyole na kuendelezwa kimakazi ,Mbeya itakuwa vizuri kuliko Miji Mingi ya Tzn hii.
Eti mbeya ya zaman na ya sasa hahaa
Kwan kuna majiji gani yaliyo ya zaman na sio ya sasa
Unavyo ongea utadhania utafikiria majiji mengije ni ya zaman na mbeya ni ya kisasa
Dual carriage my foot serikali haiwez jenga huu mradi kwenye kjj cha mbeya
 
Kwenu wapi mkuu tupime Kama kumeizidi Mbeya kimaendeleo. Mbeya imeendelea katika sekta nyingi kuanzia elimu mpaka michezo. Tusiendekeze chuki Mbeya ni jiji la mfano nchi hii Kwa maendeleo ya kweli.

Ni Mbeya penye shule nzuri, uchumi mzuri Kwa wakazi wake, ni Mbeya kwenye Tim nyingi za soka. Haya Mambo unayakuta wapi kwingine Tanzania hii?
View attachment 1817471

Mbeya City
View attachment 1817472

Mount Loleza - Unaosifia eti kivutio

View attachment 1817474

HIzi ndizo mandhari za Mbeya, nitakuja niwwaambie kwa nini Mbeya patabaki na ujima wake ukipewa Ceremonial Title. Watu wa Mbeya noma sana. Hawataki mawazo ya watu wasiokuwa wa kwao kama vile watu wasio wa Mbeya wanavyopata tabu kuwaongoza hawa watu. Ubishi wa kishamba, ubinafsi na ukablia ndiko mahala pake. Maendeleo yanahitaji kuchanganya fahamu na maarifa. Kaeni na mlima loleza wenu eti ndio kivutio cha jiji. Duh!.
 
Back
Top Bottom