Elections 2010 Majimbo 21 yatakayochukuliwa na CHADEMA kabla ya oct 31

Fanfa

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2009
Posts
1,830
Reaction score
2,878
Ndg wan JF,
Kulingana na tathimini ya mwenendo mzima wa kampeni za uchaguzi kwa takribani siku 40, wapiga kura wameonyesha dhahiri kuwa CHADEMA itashinda katika majimbo yafuatayo; Hizi sio hisia zangu bali ni hali halisi ya upepo wa kisiasa katika majimbo yafuatayo.

1. Kiteto
2. Karatu
3. Bukombe
4. Iringa mjini
5. Ubungo
6. Kawe
7. Vunjo
8. Kigoma Mjini
9. Kigoma Kaskazini
10. Maswa Mashariki
11. Nyamagana
12. Hai
13. Busanda
14. Mbulu
15. Tarime
16. Arusha Mjini
17. Meatu
18. Ngorongoro
19. Kibaha
20. Singida (jimbo la Tundu Lissu)
21. Bukoba mjini

Ushauri wangu kwa team ya kampeni ya CHADEMA iweke mikakati dhabiti ya kulinda kura katika majimbo haya kwa gharama yoyote maana CCM wanajua hilo na mkizembea sauti ya wananchi itapokonywa na CCM kwa kuiba kura.

Pia Dr. Slaa kama itawezekana apite tena kwa awamu ya pili katika majimbo haya KUKAZIA HUKUMU YA WANANCHI dhidi ya CCM.

Kama kuna watu wamefanya tathimini katika maeneo mengine wanaweza kuongeza katika list hii.

Ningeshauri tutoe tathimini kulingana na hali halisi ya kisiasa katika maeneo husika badala ya ushabiki.





 
Kama hawataiba,Njombe Magharibi hali ni mbaya kwa CCM,baada ya kuchakachua matokeo ya kura za maoni,wapigakura wamemfuata Nyimbo baada ya kuhamia Chadema.
 
Mkuu mbozi magharibi kuna kijana anaeitwa Silinde wa Chadema anachukua jimbo bila wasi wasi wowote.
 
Mimi huwa sihesabu vifaranga kwa kuangalia idadi ya mayai... napenda zaidi kulinda hayo mayai ili yaanguliwe yote... kwa kuhesabu vifaranga na tuna mwezi mzima wa kampeni ni ngumu sana

Cha maana ni kuendeleza kampeni ili mbunge sahihi (bila kujali chama) ashinde
 
Fanfa;
You mean haya ndiyo majimbo pekee yaliyo na wagombea wa Chadema?
Ningekupa zawadi ila sikupi, umeniudhi sana una kasoro ya kutofikisha ujumbe kwa jamii kama ulivyoukusudia wewe mwenyewe. hata hivy nimeshakusamehe ila ningekushauri kichwa cha thread yako uki-editi ili kisomeke hivi: MAJIMBO YA UCHAGUZI 21 AMBAYO TAYARI YAMESHACHUKULIWA NA CHAMA KITAKACHOTAWALA BAADA YA TAREHE 31 OKTOBA, halafu unayataja. Huhitaji kutaja jina la chama, ukitaja majimbo tu wapiga kura tayari watakuwa wanaelewa unamaanisha chama gani. Wanaelewa vizuri sana kuwa ni kipi chama chao baada ya uchaguzi
 

Wee kweli ni fanfa, yaani umeacha majimbo kibao kwa mfano anakotoka makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. S. Arfi au humfahamu??? Sumbawanga mjini, Mbozi, Mbeya mjini, Kawe, na orodha inaendelea....
 

Nashukuru kwa kunisamehe. Sina maana kuwa ndo majimbo pekee bali kulingana na tathimini tuliyofanya. Tunahitaji tathimini kutoka kila pembe ya nchi na kazi hii huwezi fanya mtu mmoja au wawili. Hivyo naomba utujuze kwa yale ambayo hatujapata tathimini halisi.

 
Mkuu mbozi magharibi kuna kijana anaeitwa Silinde wa Chadema anachukua jimbo bila wasi wasi wowote.

Tunashukuru mkuu kwa taarifa. Tunaomba uzidi kutupa tathimini ya sehemu zingine
 
Mbeya vijijini naskia lishachukuliwa na CHADEMA, yaani hakuna ubishi hapo!
 
Ninaafiki na hiyo tathmini kwa asilimia sitini hivi. Hesabu zangu zinaweka majimbo 81 kuwa yanaelekea Chadema na mengineyo 26 ni "too close to call"

Majimbo yote ya Dar, Siha ni baadhi tu ya majimbo ambayo huenda yakaangukia Chadema. Huko Siha kuna Injinia mmoja anaitwa Humphrey Tuni nasikia amemkalia pabaya Mhe. Aggrey Mwanri ila siwezi kuthibitisha maana huko sijafika taarifa hizo ni "hearsay"

Jimbo la 18. Ngorongoro sina uhakika kwa sababu taarifa nilizonazo mgombea wa Chadema pamoja alikuwa ni mbunge wa zamani wa hapo katika miaka ya 1985- 1990 Bw. Parkipuny wanasema hakubaliki sana wakidai kutokana na silika yake ambayo siwezi kuiandika humu kwa sababu ni hisia tu. Hata hivyo Parkipuny is very strong ukilinganisha na huyo mpinzani wake wa CCM ambaye anashutumiwa kwa kutotetea Mwarabu mwindaji kuondolewa Loliondo. Parkipuny anakumbukwa kwa kumwondoa Ole Saibul (marehemu sasa) kwa kile kilchoitwa kuwatekeleza wamasai wa ngorongoro. Hiyo "is a hot button campaign issue" kwenye tarafa ya ngorongoro ambako serikali imekusudia kuondoa kilimo cha bustani kwenye mbuga ya hifadhi. Wagombea wote wawili "they are busy assigning blame on the matter rather than assuming responsibility."

Yule mgombea wa CCM hapo Ngorongoro anaitwa Saningo Telele (an immediate) MP hakubaliki sana haswa kwenye kata yake ya ngorongoro wanadai he is " too snobbish and too weak" Kama hilo linatosha kumsarambatisha tutajua baada ya D-Day. Na huyu Parkipuny kama akiweza kuwashawishi kata ya Ngorongoro basi jimbo limekwenda Chadema maana huko kwenye kata nyinginezo "it is anybody's game"
 
Hamuwafahamu CCM kwenye ballot box. Muulize Dr Mvungi aliyegombea Urais kwa tiketi ya NCCR mwaka ule. Hakuiona hata kura aloojipigia yeye mwenyewe pale Chuo.
 
hivi wanaoshabikia ccm ni watanzania?
 
Taadhari isije ikawa kama tasmini ya mwaka 2005 kusema upinzania utapata majimbo 100, na kuzomwea kote kina Hawa Ghasia na Makweta mwisho wake wakaja kushinda, naomba tusidanganyike na wingi wa watu kwenye mikutano ina bidii tuwahamasishe wajitokezo hiyo siku ya kupiga kura na wajitahidi kuzilinda ndio ushindi ytapatikana
 
Hivi Moshi kwa Pesa Ndesa vipi? Hakuna mpinzani mkuu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…