Uchaguzi 2020 Majimbo haya yanatakiwa kwa gharama yoyote na CCM

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
1. Kawe: Namuonea huruma sana Halima Mdee (Gwajima hapendwi lakini ndio mbunge mtarajiwa)

2. Vunjo: Kimei sio mwanasiasa ila alienda pale kwa kuelekezwa tu upinzani unapitaje?

3. Moshi Mjini: Jimbo kongwe la upinzani. Mwenye jimbo lake kafa(Ndessamburo) upinzani unapitia wapi?

4. Hai: Mbowe ni kama kashatolewa lakini kwa sababu mpira ni dk 90 anaona bora amalize tu

5. Arusha Mjini: Maskini Lema anapambana na aliekuwa Rais wa mkoa wake anajua kila kitu kuhusu Arusha.

6. Iringa Mjini: Msigwa amekuwa mwiba sana bungeni kwahiyo anatakiwa asirudi kwa vyovyote vile.

7. Mbeya Mjini: Sugu anapambana na Naibu Spika. Kiutawala tu bungeni nani mkubwa?

8. Tarime zote(Vijijini na Mjini) si rahisi lakini ni lazima wapinzani waachie hata kwa nguvu.

9. Kigoma mjini: ZZK ni mfame pale lakini anatakiwa mtu mpole wa kupiga makofi tu bungeni na kuimba mapambio.

Wapinzani watapita wasiojua kuongea sana na vijimbo vidogo vidogo tu.

Wekeni alama uzi huu halafu baada ya tarehe 28 mtaniambia kuwa mimi sio muongo. Mimi sina chama ila ukweli ndio huo.
 
Naona umeandika hapa kujifurahisha tu. Mahera anatoka jasho hajui awasaidie kwa njia gani, wapiga kura hawataki tena ule ujinga wa zamani mnawaibia kura halafu wanakaa kimya, mwaka huu mtaisoma namba.
 
Mwenyekiti tu hana uhakika na kibarua chake ndiyo itakuwa hao wengine.

Mwizi anaibia usiku yani huwezi kuiba mbele ya macho ya watu huko Arusha Lema ni kama anajua hadi mpinzani wake anachokiwaza ameanika kila mpango wa siri wa hao jamaa kuhusu wizi wa kura.
 
Shime watanzania tusicheze na maisha yetu. Tuipige chini CCM kila mahala. Huyu dikteta akirudi ikulu tena tumekwisha!

Mange Kimambi aliwahi kutuonya kipindi kile kwamba atatushika pabaya. Na kweli tumeumizwa Sana.
 
Sisiemu watakua wamesuka wapiga kura hewa wakutosha huko.

Huku kwetu wapiga kula hewa wapo wengi balaa, inasikitisha sana.
 

7. Mbeya mjini: Sugu anapambana na naibu spika. Kiutawala tu bungeni nani mkubwa?
Kigoma mjini: ZZK ni mfame pale lakini anatakiwa mtu mpole wa kupiga makofi tu bungeni na kuimba mapambio.
👇👇ZITTO AKIWA ANAIMBA MAPAMBIO😁😁😁


Iringa mjini: Msigwa amekuwa mwiba sana bungeni kwaio anatakiwa asirudi kwa vyovyote vile.
👇👇MSIGWA AKIWA MWIBA😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…