1. Kawe: Namuonea huruma sana Halima Mdee (Gwajima hapendwi lakini ndio mbunge mtarajiwa)
2. Vunjo: Kimei sio mwanasiasa ila alienda pale kwa kuelekezwa tu upinzani unapitaje?
3. Moshi Mjini: Jimbo kongwe la upinzani. Mwenyewe jimbo lake kafa(Ndessamburo) upinzani unapitia wapi?
4. Hai: Mbowe ni kama kashatolewa lakini kwa sababu mpira ni dk 90 anaona bora amalize tu
5. Arusha Mjini: Maskini Lema anapambana na aliekuwa rais wa mkowa wake anajua kila kitu kuhusu Arusha.
6. Iringa Mjini: Msigwa amekuwa mwiba sana bungeni kwaio anatakiwa asirudi kwa vyovyote vile.
7. Mbeya Mjini: Sugu anapambana na Naibu Spika. Kiutawala tu bungeni nani mkubwa?
8. Tarime zote(Vijijini na Mjini) si rahisi lakini ni lazima wapinzani waachie hata kwa nguvu.
9. Kigoma mjini: ZZK ni mfame pale lakini anatakiwa mtu mpole wa kupiga makofi tu bungeni na kuimba mapambio.
Wapinzani watapita wasio jua kuongea sana na vijimbo vidogo vidogo tu.
Wekeni alama uzi huu halafu baada ya tarehe 28 mtaniambia kuwa mimi sio muongo. Mimi sina chama ila ukweli ndio huo.
.