GE2025 Majina haya ya Wabunge waliokatwa kwa visasi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwenye siasa kuna visasi vingi, chuki, husuda , usaliti, kiburi, jeuri , dharau, huko kumejaa huwa ni kutesa kwa zamu leo kwangu kesho kwako.
Wabunge hawa wameondolewa kwa chuki visasi na usaliti..Kuna baadhi waliojiharibia na kuna wengine chuki za waziwazi

1. Ummy Mwalimu - Rafiki wa JK , Samia na Januari..Urafiki wa Ummy uliisha baada ya Ummy kuona uwezo wa Samia ni mdogo kuongoza nchi kubwa kama Tz pili anaendesha nchi kilevi. Ameliwa kichwa kwa kisasi cha Mwenyekiti

2. Mrisho Gambo
Bila shaka Mrisho Gambo ni wabunge wachache ambao walikua wakiibua tuhuma nzito dhidi ubadhirifu wa fedha za umma , aliibua ufisadi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha hadi Dkt Pima aliyekua MKURUGENZI JIJI LS ARUSHS akala mvua ya mawe ya miaka 25 kabla hajakata rufaa, dunia inajua kuwa Dkt Pima aliiba hela zikaenda CCM kufanya kazi , ni kama sasa hivi zinavyoibws kutoka Halmashauri kugharamikia Ma Festival ya Mama siju Samia Connect nk. Lakini hapa mwishoni Gambo aliibua tuhuma za Ujenzi wa Jengo Jipy la Halmashauri kwa Vile Mchengerwa na Makonda ni Mtu na Ba Mkwe kulinda Heshima ya Mwenyekiti akaliwa kichwa kwa kisasi cha ndugu watatu waliounganishwa kwa damu na maji.

3. Luhaga Mpina
Huyu tunajua kabisa alivyokua mwiba katika kulinda maslahi ya nchi wakati wa Bunge Kibogoyo la Tulia Ackson, ingekua kipindi cha Samweli Sitta , Tume ingeundwa kuangalia suala la uingizaji wa Sukari maana kuna makampuni ya Simu hadi yaliagiza sukari, kwa vile Bi Tozo ametawalia na team Mtandao akienda kwenye kampuni anakuta majina ni yale yale team mtandao na Waziri wake ni mtiifu kwa Team Mtandao basi anakasirika anamuona Mpina ni mpiga kelele..Mwisho wa Siku Asset kama Mpina ikaliwa kichwa kwa visasi.

4. Januari Makamba
Hakuna dout yoyote kuwa huyu jamaa alikua threat katika uongoz wa Mwenyekiti wetu , kwa vile Januari alikua ameanza harakati mapema za kuutamani Urais aliona ndo muda muafaka wa kuanza kuunda team zake mwishowe akagombana na mwenye- kiti chake naye hakuchomoza hata nusu punje jina halikurudi, bila shaka mzee atakua ametengua kauli ya wazuri hawafi mapema.

5. Wabunge wa Mwanza na Musoma
Ilemela na Nyamagana ( Angel Mabula na Stanslau Mabula ) hawa wabunge walikua watiifu kwa Magufuli na walikua wazalendo ndo miongoni mwa wabunge ambao Magufuli alikua akiwapenda sana. Mabula yeye alianza kulia kichwa toka akiwa Waziri ni chuki bila sababu weka na Kaleman kule Geita -Chato.

Wabunge wa Musoma Mjini na Bunda Mjini ( Mathayo Manyinyi na Maboto ) hawa wana ugomvi mkubwa na Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Wasira , Wasira ana chuki na matajiri anajua matajiri wote ni wezi wanyonyaji?, waporaji .Hajui kuwa utajiri unatafutwa .Mambo ya mwaka 1890 anayaleta leo.

6. Fred Lowasa (Monduli)
Mbali na kuwa Fred Lowasa ni mlevi lakini ameondolewa kwa CHUKI ya Familia yake na JK..Utakumbuka wakati anahojiwa na Millard Ayo kwa yale mambo anayoyakumbuka kwa Mzee wake alisema kuwa mzee alikua loyalty anamuamini rafiki na Babake hajawai kumsaliti rafiki yake katika maisha yake ( Hii kauli ilimuudhi sana JK ) hivo amemsubiria huku kwenye maamuzi, JK ameendelea kumsalit Lowasa hata akiwa huko kaburini.

7. Emanuel Shangai (Ngorongoro)
Huyu ameondolewa kwa sababu ya kuwa na msimamo mkali kama wale wabunge wa mrengo wa kulia (wing right), yeye alipambana na kutetea maslah ya wananchi wa Ngorongoro wasihamishwe kwa nguvu kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera kwa vile utawala wa huu umezamiria kuwandoa wamasai kule Hifadhini na maeneo yao kupewa waarabu kwa ajili ya kujenga mahoteli na Mbunge wao alikua na wananchi sambamba Mwenyekiti akaona amle kichwa waziwazi.

8. Ole Sendeka
Huyu alikoswa kuuwawa kwa risasi na wasio julikana aliungana na Shangai wa Ngorongoro kuwatetea wa masai, mzee wa watu ameliwa kichwa mzima mzima kwa sababu ya chuki ya Mwenyekiti akimuona kuwa anamchelewesha mambo ya kula hela za waarabu walizowekeza kufukuza wamasai Hifadhi ya Ngorongoro, cha kusikitisha ni kwamba operation Msomera imesimama wakati huu kuelekea Uchaguzi Mkuu ila baada ya hapo wamasai watafukuzwa kama nyumbu.

9.Askofu Gwajina
Huyu sina haja ya kumuelezea sana .

Kwenye Siasa ni kuwa Macho kama upo choo cha Mlango wa Mbavu za mbwa (mlango wa kuamisha ) muda wowote mkono uwe tayari kuushikilia ili mtu akisukuma wewe ushindilie kwa nguvu.
Samia The Killer ni malikia wa visasi.
 
Kwenye siasa kuna visasi vingi, chuki, husuda , usaliti, kiburi, jeuri , dharau, huko kumejaa huwa ni kutesa kwa zamu leo kwangu kesho kwako.
Wabunge hawa wameondolewa kwa chuki visasi na usaliti..Kuna baadhi waliojiharibia na kuna wengine chuki za waziwazi

Kwenye Siasa ni kuwa Macho kama upo choo cha Mlango wa Mbavu za mbwa (mlango wa kuamisha ) muda wowote mkono uwe tayari kuushikilia ili mtu akisukuma wewe ushindilie kwa nguvu.
Mkuu Kozi Kodineta Course Coordinator, bandiko lako hili GE2025 - Majina haya ya Wabunge waliokatwa majina kwa Visasi vya Mwenyekiti limenigusa sana
Haya ni matokeo ya Watanzania kuukubali ujinga wa kuingiza siasa kwenye katiba ya nchi kwa kuchomekewa kifungu batili cha kulazimisha wagombea wadhaminiwe na chama cha siasa.

Ibara ya 5 ya katiba imetoa haki kwa kila Mtanzania kumchagua kiongozi unayempenda, na ibara ya 21 imetoa haki kwa kila Mtanzania kugombea bila shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa.

Hao wote waliokatwa na chama chao, kama ni vipenzi wa wananchi wao, walipaswa wasimame kama independent candidates na wangechaguliwa na wananchi wao.

Hiki kipengele cha mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni dhulma kubwa kwa Watanzania.

Kuna baadhi ya laana nchi yetu inazipata kutokana na dhulma kama hizi!.

Nimekuleta ili uone jinsi tulivyopigia kelele dhulma hii.

Huyu naye alipoanza tulikuwa na matumaini makubwa kuwa atatenda, kumbe ....
Naomba nisimalizie ...!

Ila Mungu Yupo!.

Paskali
 
Na kuna wagombea wamepitishwa kwa maslahi binafsi na sio ya nchi , kama WA Kinondoni, Kibamba na Kondoa
Mbunge wa Kibamba alishindwa kwenye kura za maoni . Tuache porojo zaisizo na maana. Ulitaka alieshindwa ndo ateuliwe?
 
Mkuu Kozi Kodineta Course Coordinator, bandiko lako hili GE2025 - Majina haya ya Wabunge waliokatwa majina kwa Visasi vya Mwenyekiti limenigusa sana
Haya ni matokeo ya Watanzania kuukubali ujinga wa kuingiza siasa kwenye katiba ya nchi kwa kuchomekewa kifungu batili cha kulazimisha wagombea wadhaminiwe na chama cha siasa.

Ibara ya 5 ya katiba imetoa haki kwa kila Mtanzania kumchagua kiongozi unayempenda, na ibara ya 21 imetoa haki kwa kila Mtanzania kugombea bila shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa.

Hao wote waliokatwa na chama chao, kama ni vipenzi wa wananchi wao, walipaswa wasimame kama independent candidates na wangechaguliwa na wananchi wao.

Hiki kipengele cha mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni dhulma kubwa kwa Watanzania.

Kuna baadhi ya laana nchi yetu inazipata kutokana na dhulma kama hizi!.

Nimekuleta ili uone jinsi tulivyopigia kelele dhulma hii.

Huyu naye alipoanza tulikuwa na matumaini makubwa kuwa atatenda, kumbe ....
Naomba nisimalizie ...!

Ila Mungu Yupo!.

Paskali
Mgombea binafsi
 
Haya ni baadhi ya mambo mazuri ya Rais Samia:

  1. Kufungua Tanzania kimataifa na kuongeza uwekezaji kupitia diplomasia ya kiuchumi.
  2. Kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati kama SGR, Bwawa la Julius Nyerere na uboreshaji wa viwanja vya ndege na bandari.
  3. Kusimamia elimu bila ada na kuongeza miundombinu ya shule, vyuo na ajira za walimu.
  4. Kuboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali, vituo vya afya na kupeleka vifaa tiba vya kisasa.
  5. Kusogeza huduma za maji na nishati vijijini na mijini ili wananchi wapate maisha bora.
  6. Kuimarisha mshikamano wa kitaifa kwa kuunganisha Watanzania bila kujali tofauti za kisiasa, kijamii au kidini.
  7. Kusikiliza wananchi kwa karibu na kuwaongoza kwa mtindo wa ushirikishwaji na uwazi.
Umebidi uiulize AI ikudanganye maana alichokifanya huyu bi chura hakionekani pia uwezo wenu wa kufikiri ni kisoda
 
Mkuu Kozi Kodineta Course Coordinator, bandiko lako hili GE2025 - Majina haya ya Wabunge waliokatwa majina kwa Visasi vya Mwenyekiti limenigusa sana
Haya ni matokeo ya Watanzania kuukubali ujinga wa kuingiza siasa kwenye katiba ya nchi kwa kuchomekewa kifungu batili cha kulazimisha wagombea wadhaminiwe na chama cha siasa.

Ibara ya 5 ya katiba imetoa haki kwa kila Mtanzania kumchagua kiongozi unayempenda, na ibara ya 21 imetoa haki kwa kila Mtanzania kugombea bila shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa.

Hao wote waliokatwa na chama chao, kama ni vipenzi wa wananchi wao, walipaswa wasimame kama independent candidates na wangechaguliwa na wananchi wao.

Hiki kipengele cha mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni dhulma kubwa kwa Watanzania.

Kuna baadhi ya laana nchi yetu inazipata kutokana na dhulma kama hizi!.

Nimekuleta ili uone jinsi tulivyopigia kelele dhulma hii.

Huyu naye alipoanza tulikuwa na matumaini makubwa kuwa atatenda, kumbe ....
Naomba nisimalizie ...!

Ila Mungu Yupo!.

Paskali

Nchi ya kipumbavu sana hii.
 
Uko sahihi kabisa. Na vyama vyote vya siasa havitaki mgombea huru. Mbunge anawakilisha chama, sio wananchi waliompigia kura.

Amandla...
 
Mkuu Kozi Kodineta Course Coordinator, bandiko lako hili GE2025 - Majina haya ya Wabunge waliokatwa majina kwa Visasi vya Mwenyekiti limenigusa sana
Haya ni matokeo ya Watanzania kuukubali ujinga wa kuingiza siasa kwenye katiba ya nchi kwa kuchomekewa kifungu batili cha kulazimisha wagombea wadhaminiwe na chama cha siasa.

Ibara ya 5 ya katiba imetoa haki kwa kila Mtanzania kumchagua kiongozi unayempenda, na ibara ya 21 imetoa haki kwa kila Mtanzania kugombea bila shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa.

Hao wote waliokatwa na chama chao, kama ni vipenzi wa wananchi wao, walipaswa wasimame kama independent candidates na wangechaguliwa na wananchi wao.

Hiki kipengele cha mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni dhulma kubwa kwa Watanzania.

Kuna baadhi ya laana nchi yetu inazipata kutokana na dhulma kama hizi!.

Nimekuleta ili uone jinsi tulivyopigia kelele dhulma hii.

Huyu naye alipoanza tulikuwa na matumaini makubwa kuwa atatenda, kumbe ....
Naomba nisimalizie ...!

Ila Mungu Yupo!.

Paskali
Watu wakitaka mabadiliko nyinyi mnakuwa mbele kuwapinga kisa ccm ifanye inavyotaka kwa kuogopa kukamatwa.
 
Babalevo ameachwa makusudi ili aliwe kichwa wakati watakapomtangaza Zito kua mbunge kama walivyokubaliana.
ACT wapate viti 5 na chaumma wajinga jinga 10 ili ionekane kulikua na uchaguzi.
Halafu baadaye mgombea urais kupitia chaumma atakua mkuu wa mkoa wa Arusha.
 
Mbunge wangu Ummy alifanya kosa gani? Nasikia fununu alikula fedha za Covid19 akiwa waziri afya na tetesi nyingine alikamatwa na mazungumzo ya kumsema Rais wangu mpendwa Samia. Ukweli ni upi?
 
Ila Kikwete Ni mtu mweusi Sana Kama chungu akicheka watu wanadhani Ni mtu kumbe ni shetani mkubwa yule mzee atakufa vibaya Sana huyu mzee

Hadi mtoto wa Lowassa? Mh!!
Hapo ndipo ninapomkubali Kikwete

Na katika marais wajanja,JK kwenye kupigania mambo yake yuko poa

Alimpanga Lowasa akapangika

Akamsaidia kushinda urais,kisha akamchinjia baharini

In history Lowasa ni looser,

Tutamkumbuka Kikwete kuliko Laigwanan

Kwani JK ni winner,no matter alitumia njia gani kushinda
 
Back
Top Bottom