GE2025 Majina haya ya Wabunge waliokatwa kwa visasi

GE2025 Majina haya ya Wabunge waliokatwa kwa visasi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mkuu Kozi Kodineta Course Coordinator, bandiko lako hili GE2025 - Majina haya ya Wabunge waliokatwa majina kwa Visasi vya Mwenyekiti limenigusa sana
Haya ni matokeo ya Watanzania kuukubali ujinga wa kuingiza siasa kwenye katiba ya nchi kwa kuchomekewa kifungu batili cha kulazimisha wagombea wadhaminiwe na chama cha siasa.

Ibara ya 5 ya katiba imetoa haki kwa kila Mtanzania kumchagua kiongozi unayempenda, na ibara ya 21 imetoa haki kwa kila Mtanzania kugombea bila shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa.

Hao wote waliokatwa na chama chao, kama ni vipenzi wa wananchi wao, walipaswa wasimame kama independent candidates na wangechaguliwa na wananchi wao.

Hiki kipengele cha mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni dhulma kubwa kwa Watanzania.

Kuna baadhi ya laana nchi yetu inazipata kutokana na dhulma kama hizi!.

Nimekuleta ili uone jinsi tulivyopigia kelele dhulma hii.

Huyu naye alipoanza tulikuwa na matumaini makubwa kuwa atatenda, kumbe ....
Naomba nisimalizie ...!

Ila Mungu Yupo!.

Paskali
Bila shaka tunasubiria Katiba mpya
Maana vyama vyote mwaka huu Katiba Mpya imewekwa kwenye Ilani yao.
Ila najiuliza Katiba Mpya itaandikwa Yule Simba akiwa kwenye Korokoro kweli au ni kutaka kutuhadaa tuwape kura zetu halafu wasepe.
 
Wengine walikuwa watu magufuli. Hawakumuunga mkono samia anaingia
 
Mabula alifanya nini ni baada ya ridhwan kuwa naibu waziri wa ardhi na mabula kuwa waziri wa ardhi wakati huo ndio haikupita mda akaondolewa
 
Haya ni baadhi ya mambo mazuri ya Rais Samia:


  1. Kufungua Tanzania kimataifa na kuongeza uwekezaji kupitia diplomasia ya kiuchumi.
  2. Kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati kama SGR, Bwawa la Julius Nyerere na uboreshaji wa viwanja vya ndege na bandari.
  3. Kusimamia elimu bila ada na kuongeza miundombinu ya shule, vyuo na ajira za walimu.
  4. Kuboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali, vituo vya afya na kupeleka vifaa tiba vya kisasa.
  5. Kusogeza huduma za maji na nishati vijijini na mijini ili wananchi wapate maisha bora.
  6. Kuimarisha mshikamano wa kitaifa kwa kuunganisha Watanzania bila kujali tofauti za kisiasa, kijamii au kidini.
  7. Kusikiliza wananchi kwa karibu na kuwaongoza kwa mtindo wa ushirikishwaji na uwazi.
Kinacho niuma na kuniudhi ni jambo moja hayo yote uliyo yasema ndivyo yalivyo ila hayaongelewi sana kwenye media kulingana na ukubwa wake badala yake ni TBC PEKEE NDIO ANATEKELEZA JUKUMU HILI kwa kweli kafanya
 
Bila shaka tunasubiria Katiba mpya
Maana vyama vyote mwaka huu Katiba Mpya imewekwa kwenye Ilani yao.
Ila najiuliza Katiba Mpya itaandikwa Yule Simba akiwa kwenye Korokoro kweli au ni kutaka kutuhadaa tuwape kura zetu halafu wasepe

Bila shaka tunasubiria Katiba mpya
Maana vyama vyote mwaka huu Katiba Mpya imewekwa kwenye Ilani yao.
Ila najiuliza Katiba Mpya itaandikwa Yule Simba akiwa kwenye Korokoro kweli au ni kutaka kutuhadaa tuwape kura zetu halafu wasepe.
2027 itakuwa tushajua hatima yake
 
Back
Top Bottom