Nilikorofishana kidogo na mpenzi wangu nikagoma kula nikaondoka ile narudi namkuta kavaa khanga imeandikwa 'ukisusa wenzio wala',jamani hivi haki kweli kuvaa khanga kama hii maana sio mara yake ya kwanza kuna safari flani hivi nilisafiri kwa dharura sikumuaga niliporudi nikamkuta kavaa khanga imeandikwa 'ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani',.na kuna siku niliacha hadi kwenda kazini niliamka nikakuta kanivalia khanga imeandikwa 'ukitoka wenzako wanaingia'.jamani hivi maneno ya kwenye khanga hayana mipaka?