Majina, misemo na maneno kwenye khanga

Majina, misemo na maneno kwenye khanga

maradhi yote ugua ila kuchacha usiombe
Maskini hafilisiki,
Pesa huna,nguvu huna hata mkwara?
 
Mwenye wivu ajinyonge
hii ni kawaida yetu sijui nyie malimbukeni
mimi ndo shina wengine wote matawi
utamaliza gesi kwa kupika mifupa
Mtu mzima ovyo!
Jicho hilo mimi nina wangu
mtaa wa pili mtanikoma..
asie kujua nani kama wewe ni mmbea
Yako unayakalia yawezio midomo juu
kama unataka kumjua mume mwenzio mwache mkeo
chokochoko za jirani hazinitoi ndani..
tusikosane tufikirie watoto
Mtamaliza kuni kwa kukaanga mawe
Ushuzi dawa yake mate
huruma ninayo bahati sina
wewe peleleza na wala hutaniweza
wembamba wa reli treni inapita

ongezea mengine
 
Sa Sweetie hizo Khanga utapoanza kuninunulia ndo ntajua maneno yake.
 
Fitina na pelelezi ni sumu ya penzi
Dhuluma si njema
Mama nipe radhi kuishi na watu kazi
CCM NO.1
Penye udhia penyeza rupia
 
..................................... (hiki ni kitenge jamani, hakina maneno..eti!? :lol🙂
 
Tenda wema mara mia,adui akijua, umeumia.

Kama unaweza mtie kama mumeo umzuie.

Mbuzi kala mkeka,wambea mtakalia nini?.

Usisafirie nyota ya mwenzio.

Utamu wa wali matandu,uzuri wa kiuno chach*ndu.

Raha ya nanga baharini,mtoni utatoka na tope.

Mjinga akierevuka,mwerevu uko matatani.

Utamu wa mtwangio kutwanga,raha ya wanaume,mapanga nshhaaaa....!!!
Niendelee....?
 
nimekukubali madame.. dahh, Uzuri wa kiuno chachandu.!!!
 
Tenda wema mara mia,adui akijua, umeumia.

Kama unaweza mtie kama mumeo umzuie.

Mbuzi kala mkeka,wambea mtakalia nini?.

Usisafirie nyota ya mwenzio.

Utamu wa wali matandu,uzuri wa kiuno chach*ndu.

Raha ya nanga baharini,mtoni utatoka na tope.

Mjinga akierevuka,mwerevu uko matatani.

Utamu wa mtwangio kutwanga,raha ya wanaume,mapanga nshhaaaa....!!!
Niendelee....?
Madame B raha ya nanga baharini...nimekukubali endelea

Sikuhadae rangi,tamu ya chai sukari
Chakumbimbi ukimuona muogope
Sijafunzwa kula ndizi sukari
Macho yanacheka, moyo unalia
unalo limekuganda
 
Last edited by a moderator:
1.Mpaka Kieleweke
2.Hapa kazi tu kula kwenu
3.Kula CCM Kura CHADEMA
 
Back
Top Bottom