City Owl
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 3,475
- 7,571
Ndugu wanaJF,
Kufikia mwisho wa karne ya 21, majina kama Masawe, Otieno, Gwamaka, Kamugisha, Masanja n.k yatafutika nchini kwetu.
Imekuwa nadra mno kukuta mtanzania mwenye majina matatu, yote yenye asili ya kabila lake, au hata ya makabila ya hapa Tanzania au Afrika kwa ujumla.
Ubantu unaisha. Unailoti unaisha.
Watu wa pwani walishapotezwa kitambo. Wao wengi wao wana majina ya kiarabu tupu. Wakina Mohammed Said. Hata Surname za kiafrika walishaacha.
Watu wa bara ndiyo walikuwa badobado, lakini nao sasa watoto wao ni wakina Brian McDonald, Humphrey Jr. Scott au Natasha-Rose Leonard.
Hata wazungu, Wachina, Wahindi na Waarabu wanatushangaa sana.
Wao hawana huu ujinga.
Hakuna mzungu anaitwa Manka, hakuna muarabu anaitwa Mabula wala mchina anayeitwa Mahenge.
Ngugi wa Thiong'o huyaita haya majina colonial tags.
Yeye aliachana na colonial tag yake 'James' akabaki na Ngugi wa Thiong'o.
Je, Waafrika tumeshindwa kuthamini majina ya tamaduni zetu na kuachana na majina ya kigeni?