Majina ya Kiafrika mbioni kutoweka

Majina ya Kiafrika mbioni kutoweka

Emu niambie nini maana ya majina,Trump,Frank,Fredy,William,Paul,Pascal,Charles,Charlie,Zephania,Gerlad,James,Steven,Robert?????
Haya ni majina ya watu ambayo yana asili na maana tofauti, kulingana na tamaduni mbalimbali. Hapa chini ni ufafanuzi wa majina kadhaa:

1. Trump: Jina hili limekuwa maarufu kutokana na rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump. Jina lenyewe linaweza kumaanisha "triumph" au ushindi.

2. Frank: Asili yake ni kutoka kwa neno la Kilatini "Franciscus," ambalo lina maana ya "mtu huru."

3. Fredy (au Freddy): Ni kifupi cha jina "Frederick," lenye asili ya Kijerumani, likimaanisha "mtawala wa amani."

4. William: Jina la asili ya Kijerumani, likimaanisha "mpiganaji wa nguvu" au "mlinzi mwenye mapenzi."

5. Paul: Lina asili ya Kilatini, likimaanisha "mdogo" au "mnyenyekevu." (Ukimsoma Paul kwenye agano jipya utaelwa kwanini jamaa alikuwa vile jina lina kawaida ya kuambukiza mwenendo na tabia za mmiliki wa jina)

6. Pascal: Lina asili ya Kifaransa na Kilatini, likiwa linahusiana na neno "Pascha," likimaanisha "Pasaka" au "sherehe ya kupita au kuvuka kama unasomaga Biblia pitia kitabu cha kutoka utaelewa Vizuri."

7. Charles: Lina asili ya Kijerumani, likimaanisha "mtu huru" au "mtawala."

8. Charlie: Kawaida ni kifupi cha Charles, lakini pia hutumika kama jina kamili. Lina maana ya "mtu huru."

9. Zephania: Ni jina la Kiebrania, lenye maana ya "Mungu ameficha" au "Mungu amelinda."(Soma kitabu cha Sefania katika Biblia utaelewa vizuri)

10. Gerald: Lina asili ya Kijerumani, likimaanisha "mtawala mwenye nguvu" au "mtawala wa upanga."

11. James: Ni jina la Kiingereza lenye asili ya Kiebrania, sawa na "Jacob," likimaanisha "aliyeshikilia kisigino" au "mfuatiliaji." au king'ang'anizi (ukisoma Kitabu cha Mwanzo katika Biblia) utaelewa vizuri Yakobo alikuwa king'anganizi Tangu tumbo bado akang'ang'ania mpaka akabarikiwa na malaika hiyo haitoshi alimkazia Baba Mkwe mpaka akampa kipenzi cha moyo wake kwa kufanya kazi miaka 14 kwa ujumla.

12. Steven (au Stephen): Lina asili ya Kigiriki, likimaanisha "taji" au "mshindi."

13. Robert: Lina asili ya Kijerumani, likimaanisha "anayeng'ara kwa utukufu" au "anayejulikana."

Haya majina mara nyingi yanaweza kuwa na tafsiri na maana zinazotofautiana kidogo kulingana na utamaduni na matumizi ya Eneo husika.

Kama unamajina mengine unayohitaji kupata maana zake nakuomba sana usishindwe kuni quote karibu.
 
Majina ya kiafrika yataisha hata saizi karibia mengine yameanza kupotea kwa sababu hizi
1. kuna makabila ukishaita jina la ukoo wale wachawi walioko kwenye ukoo wenu inakuwa umewapa njia ya kuloga kwa urahisi sababu ya jina la ukoo analijua zaidi sasa kupunguza huu mlolongo watu wakaamua kuhamia kuita majina ya dini
 
Ni ngumu , nyaraka nyingi za serikali zipo kwa kizungu, ndo waje walazimishe watu watumie majina ya kiswahili
Kwani nyaraka za India au Rwanda au Israel haziko kwa kizungu. Umewahi kuona Mhindi anaitwa Mwighwano, au Lusinde ? Sisi ni watumwa, wajinga, washamba na limbukeni wa majina. Nimewasikia wanashangaa unapomuita mtoto jina la asili la kibantu " he, hee, jina gani hilo. Ningekuwa na uwezo ningecharaza viboko hawa binadamu weusi wasiojiamini.
 
Ndugu wanaJF,
Kufikia mwisho wa karne ya 21, majina kama Masawe, Otieno, Gwamaka, Kamugisha, Masanja n.k yatafutika nchini kwetu.

Imekuwa nadra mno kukuta mtanzania mwenye majina matatu, yote yenye asili ya kabila lake, au hata ya makabila ya hapa Tanzania au Afrika kwa ujumla.

Ubantu unaisha. Unailoti unaisha.

Watu wa pwani walishapotezwa kitambo. Wao wengi wao wana majina ya kiarabu tupu.
Wakina Mohammed Said. Hata Surname za kiafrika walishaacha.

Watu wa bara ndiyo walikuwa badobado, lakini nao sasa watoto wao ni wakina Brian McDonald, Humphrey Jr. Scott au Natasha-Rose Leonard.

Hata wazungu, wachina, wahindi na waarabu wanatushangaa sana.

Wao hawana huu ujinga.

Hakuna mzungu anaitwa Manka, hakuna muarabu anaitwa Mabula wala mchina anayeitwa Mahenge.

Ngugi wa Thiong'o huyaita haya majina colonial tags.
Yeye aliachana na colonial tag yake 'James' akabaki na Ngugi wa Thiong'o.

Je, waafrika tumeshindwa kuthamini majina ya tamaduni zetu na kuachana na majina ya kigeni?
Hata ungejiita jina la weupe mweusi huna maana,, mwisho wa mambo yote rangi yako nzuri sana nyeusi,, ndiyo utambulisho wa hadhi, heshima, thamani na utu wako. Ninaringa kuwa mweusi, ninajivunia kuwa na majina yote matano ya kibantu.
 
NI kweli mkuu nachotaka kumaanisha ni kwamba sisi hata hii lugha ya kiswahili ni kama tumeikubali shingo upande
 
Majina ya kiafrika yataisha hata saizi karibia mengine yameanza kupotea kwa sababu hizi
1. kuna makabila ukishaita jina la ukoo wale wachawi walioko kwenye ukoo wenu inakuwa umewapa njia ya kuloga kwa urahisi sababu ya jina la ukoo analijua zaidi sasa kupunguza huu mlolongo watu wakaamua kuhamia kuita majina ya dini
Hakuna uhusiano wa kulogwa na kukataa majina ya kibantu. Kama ni uchawi mbona wana majina ya kizungu na kiarabu na bado wanaanguka mapepo na kulogwa. Narudia majina ya kizungu tunayaita kwa ushamba, na kulazimishwa na dini tu.
 
Hivi kweli mleta mada hata wewe leo upate mtoto umuite jina kama kimweri, nzagamba,mateso,kinjekitile..asee kwangu Big no
 
Katika jambo jema ambalo dikteta Mobutu alifanya ni kuamuru wakongo kutumia majina yao ya asili na kuachana na za kizungu. Sisi hapa tusipokuwa makini tutakuwa hatuna hayo majina. Pia lugha zetu za asili kwa miaka ijayo zitatoweka. Pamoja na kwamba tunapaswa kuulinda umoja wetu wa kitaifa ila tupambane kuzitunza lugha zetu.
 
Kwanza nianze mimi kujilaumu kwa kutumia ID ya kizungu ya Anonymous Caller.

Naombeni msamaa.
Kwa mapungufu haya nimepoteza sifa ya kulalamika..ila naunga mkono hoja.

Naomba nishauri kwamba kama tumefeli kuacha kutumia majina ya kizungu basi tutumie majina ya nje yenye maana inayoeleweka.

Mfano wenzetu Wa-zimbabwe hutumia majina haya;

Suceess, Method, Talent, ocean, Future, Prince, Perfect, wisdom, Gift
 
Urithi wa kwanza uliobora kwa mtoto ni jina...

Wewe mwite Mashaka, Masumbuko, Gwandumi, Mayala au Anyosise, Kamala au Rugaba au Manka hakuna Shida.

Mwingine atamwita Happy au Joy,Marry, Joshua sawa tu...

Ila kumbuka Urithi ulio bora wa kwanza ni jina.
Tatizo limekwenda hadi kwenye majina ya ukoo ...unakuta mtz anajina la ukoo greyson au livingstone... majina ya ukoo ya heshimike ...kanuni inatakiwa kila unapo taja jina la pili basi liwe ni jina la ukoo halisi siyo majina ya kiarabu au kizungu
 
Hata ungejiita jina la weupe mweusi huna maana,, mwisho wa mambo yote rangi yako nzuri sana nyeusi,, ndiyo utambulisho wa hadhi, heshima, thamani na utu wako. Ninaringa kuwa mweusi, ninajivunia kuwa na majina yote matano ya kibantu.
Una bahati nzuri sana mkuu.

Wengine tulipewa majina ya kizungu na wazazi, tumesomea na kuyatumia mpaka tunajitambua na kuanza kuchanganua mambo kwa mapana zaidi.
Sasa tupo katika mchakato wa kufanya marekebisho.
 
Ndugu wanaJF,
Kufikia mwisho wa karne ya 21, majina kama Masawe, Otieno, Gwamaka, Kamugisha, Masanja n.k yatafutika nchini kwetu.

Imekuwa nadra mno kukuta mtanzania mwenye majina matatu, yote yenye asili ya kabila lake, au hata ya makabila ya hapa Tanzania au Afrika kwa ujumla.

Ubantu unaisha. Unailoti unaisha.

Watu wa pwani walishapotezwa kitambo. Wao wengi wao wana majina ya kiarabu tupu.
Wakina Mohammed Said. Hata Surname za kiafrika walishaacha.

Watu wa bara ndiyo walikuwa badobado, lakini nao sasa watoto wao ni wakina Brian McDonald, Humphrey Jr. Scott au Natasha-Rose Leonard.

Hata wazungu, wachina, wahindi na waarabu wanatushangaa sana.

Wao hawana huu ujinga.

Hakuna mzungu anaitwa Manka, hakuna muarabu anaitwa Mabula wala mchina anayeitwa Mahenge.

Ngugi wa Thiong'o huyaita haya majina colonial tags.
Yeye aliachana na colonial tag yake 'James' akabaki na Ngugi wa Thiong'o.

Je, waafrika tumeshindwa kuthamini majina ya tamaduni zetu na kuachana na majina ya kigeni?
Huo ulimbukeni na ujinga wa kukumbatia majina ya wakolomi uko tu huku kwetu. Katika nchi ya Afrika ya kusin na sehenu kubwa nchi ya Botswana na Eswatini watu wanajulikana na kuandikishwa kwa majina yao ya asili zao,
 
Hivi kweli mleta mada hata wewe leo upate mtoto umuite jina kama kimweri, nzagamba,mateso,kinjekitile..asee kwangu Big no
Mtumwa huwaza kama mtawala wake anavyotaka. Walichoweza watawala wa kizungu, kiarabu na dini zao ni kutubadili kabisa mtazamo. Nikosoma Quran na Biblia sioni amrisho la kututaka tutumie majina yao. Huu ni ujanja wa kututawala kifikra.
 
Back
Top Bottom