'Majina' ya ndege zetu mpya za ATCL

'Majina' ya ndege zetu mpya za ATCL

Na hawategemei hata kuigusa maishani mwao

Ha ha ha MOTOCHINI acha hasira mkuu utapata maradhi bure! Hapa JF usione watu wanapinga mambo ukadhani ni watu wa hovyo kama unavyodhani. Wengine ni maafisa wakuu ndani ya serikali hii na mashirika yake. Na kama hata wakiponda hizo ndege ndio hao hao wanazipanda tena kwa pesa za kulipiwa na serikali hiyo hiyo ya Magufuli.
Hivyo tuliza mzuka.
 
Mimi natamani Ndege zipewe majina haya kwa ajili ya sifa na kuitangaza Tanzania

1. KARAFUU
2 Tanzanite
 
Upinzani wa Tz ni moja pinzani za kipumbav dunian
 
At the end of the day, ndege zipo na naamini zitafanya vizuri. Kukiwa na juhudi za dhati hata Airbus A380 na Boeing B747-8 zitakuwepo tu.
Kwanini juhudi na rasilimali zisihamie kwenye madawa na madawati? You people fail to amaze me!!

Huwa hamuelewi kabisa panapokua na rasilimali haba zinapaswa kuelekezwa penye tija na mantiki zaidi. Na kwa serikali basi pia penye manufaa zaidi kwa wengi.

Sasa ni wazi umaskini unatamalaki kwa kushindwa kuchagua vipaumbele!!
 
Mimi natamani Ndege zipewe majina haya kwa ajili ya sifa na kuitangaza Tanzania

1. KARAFUU
2 Tanzanite
Sifa gani kununua ndege huku wanaombaomba madawati?

Huko wilaya ya Hai kuna kituko. Madawati yamezidi madarasa? Changanya na zako.
 
Hizi ndege jamani sio sawa na bure kwa kuanzia ni sawa kabisa kumbukeni Rais ana miezi kadhaa tu...ataleta kitu Airbus
 
Nilichogundua kuhusu Watanzania wengi, wengi ambao hawajawahi kusafiri sana nchi za watu ndio wanaosimulia sana vitu vya huko. Pia wale ambao hawajawahi kuingia pale Airport na wala hawajui hata taratibu za 'check-in' na hata kupanda ndege ndogo za watu wawili au 12 ndio wanaobeza sana hizi ndege. Na ndio maana kuna mtu alianzisha uzi humu kuhoji watu warefu watapandaje ndege hizi. Jibu ni rahisi tu kwamba hawajui chochote kuhusu usafiri wa ndege ndo maana wao kila kitu ni kubeza tu.
 
Back
Top Bottom