mie naenda na rodri....hamna mizengwe, matarajio mara nyingi huleta huzuni. Rodri kwa misimu miwili kakiwasha sana. Sema tofauti ni mwamba Rodri ni kiungo na Vini ni mshambuliaji.
Mara nyingi washambuliaji ndio wanaibuka juu kupewa tuzo haswa kwa sababu ya kufunga.
Mabeki na viungo ni wachache sana waliopata hizi tuzo ukilinganisha na washambuliaji.
Rudisheni kumbukumbu nyuma miezi michache iliyopita kwenye euro2024 kule ujerumani mtakumbuka kazi aliyopiga Rodri na Spain National team. Anastahili mazee.