Majina ya vinywaji vyetu vya asili

Majina ya vinywaji vyetu vya asili

Mkuu kunyumba kuzuri sana, wakati huo no tv, jioni tunashinda kwenye ngoma, mitaa ya mateka, makambi, kimolo, matogoro na kule luhila, mkuu asikwambie mtu kuna ngoma hiyo inaitwa kambindi, wacha bana, ikifika kuanzia mwezi wa sita komunio ya kwanza na vipaimara sherehe kila nyumba hahaa acha mkuu kitoweo mkuu wa meza.
Sasa kuna madogoli ............ yaani hapa madogoli hapa KINDI........... ukienda kile kilabu cha Manzese na Lizaboni (wenyewe tulikuwa tunaita melini) we acha kabisa. Na ukienda kule msamala karibu na yale machinjio............. yaani hapa KINDI, ULANZI na upande wa pili kuna UBENDE, MAVAMBANGOMA, MBULIKA WEEEEEEEEE............
 
We ngalikihinja mwana wa yani? ummanyile na msongela? ah pale namatuhi ndo pa bomani bwana, ummanyile na mbema?
Nimmanyi sana Msongela (Zenda) alikuwa dereva wa loli (isuzu, rangi ya bluu) la kijiji cha Namatuhi and the only usafiri wa uhakika by then. Tulikuwa tunatoka kisiwani na kuvuka zile daraja saba za mto mmoja kufuata pombe na muziki pale ukumbi wa kijiji...........weeeeeeeeeee
 
Mkuu kimsingi gongo (au chang'aa, piwa, machozi ya simba) sio pombe ya asili kwetu. Gongo ni pombe ya mvuke (spirit) na sidhani kama kuna kabila (hapa Tanzania) lenye asili ya kutengeneza hizi pombe za mvuke!
Pombe za kiasili (au kienyeji) zinatokana na mazao (yenye wanga/sukari) yanayopatikana mahali husika.
Swali langu ni Je, wamasai (na makabila ya wafugaji) wana pombe za kienyeji/asili? Gongo hapana hii asili yake si umasaini, japo inatumika sana kwa wamasai.
Hii Gongo si ndo Konyaji ya kiwandani ?
 
Boha inapatikana Tanga inatengenezwa kwa miwa, Wanzuki- Kanda ya ziwa, nafikiri tende ni sawa na Gongo, Mapuya, Kangara-Mwanza; Pingu- Dar, vipi hivi Chibuku sio ya kienyeji?
 
Hii Gongo si ndo Konyaji ya kiwandani ?
Ni kweli, lakini nadhani hii inaitwa gongo kwa vile in the same container............the alcohol content of upper part is different from that of the bottom, and sometime you might take in only alcohol...........
 
Hii Gongo si ndo Konyaji ya kiwandani ?

yeah, ila tofauti yake kubwa ni kwamba ile ya kiwandani wanapima alcoholic contents, ila hii yetu hakuna kupima - unaweza kuwa unakunywa then unamwambia mama muuza "mbona unanizimia taa?" watu wanakushangaa huyu jamaa vp loo kumbe macho yameshapofuka.

ukipata mpishi mzuri - basi yawaka ka mafuta ya taa.
 
Ni kweli, lakini nadhani hii inaitwa gongo kwa vile in the same container............the alcohol content of upper part is different from that of the bottom, and sometime you might take in only alcohol...........

yeah, ila tofauti yake kubwa ni kwamba ile ya kiwandani wanapima alcoholic contents, ila hii yetu hakuna kupima - unaweza kuwa unakunywa then unamwambia mama muuza "mbona unanizimia taa?" watu wanakushangaa huyu jamaa vp loo kumbe macho yameshapofuka.

ukipata mpishi mzuri - basi yawaka ka mafuta ya taa.

Tatizo kubwa sana la gongo sio kiwango cha 'alcohol' pekee, ila kuna wakati inakua na kiwango kikubwa sana cha methonal (hii ni aina ya 'alcohol' ambayo ni sumu - haifai kwa matumizi ya binadamu). Ingekua ni wingi wa ethanol ('alcohol' inayonyweka na wanadamu) sio tatizo sana, regardless of the inconsistency in the volume of alcohol.
 
Majina ya pombe zetu za asili:

Dengelua – Hii inapatikana kule upareni
Mbege – Hii ina[patikana kule Moshi uchagani
Ulanzi – Kule Iringa
Ulaka – Nasikia inapatikana Morogoro
Boha – sina uhakiaka inapatikana wapi
Kindi – Hii nayo naomba msaada sijui asili yake ni wapi
Wanzuki – Hii ni new technology nasikia ina gesi kushinda hata Bia
Chimpumu – Hii nayo nasikia inapatikana mikoa ya kusini
Tende – Hii inapatikana wisiwa vya karafuuZanziberi
Gongo – Hii ina majina mengi ajabu, Kachaso, machozi ya Simba, Uzo, Chang'aa, na haijulikani asili yake ni wapi

Nyingine mtajazia……………………..

Wazuki ni pombe inayotengenezwa kutumia Asali, ni tamu kama Redis kwa wale wanywaji - inapatikana sehemu za Tabora zaidi na kanda ya ziwa.

Hii wazuki kabla hujaenda kunywa lazima uhakikisha umefunga suluari kwa chini kwa kutumia kamba za viatu vyako, kama huna kamba basi lazima uchomekee ndani ya soksi ili kukinga zahma.

Hiki kinywaji kina sifa moja tu ya kulegeza bolti za kule makao makuu kadri unavyozidi kukipata, sasa bila kujijua utaanza kuharibu mazingira ya sehemu husika - na ndiyo maana unatakiwa kuwa umefunga suruari kuzuia mafuriko.

Kama we ni mgeni wa pombe hii nakushauri usitumie, na kama utataka kutumia basi uliza wenyeji wakupe masharti yake ili uwe salama.
 
Wa kunyumba kabisa veve bwelai Pa lipaya unywai mkangafu
Wakuu kule kwetu mpitimbi songea kuna kilaji babu kubwa kinaitwa myakaya, inatengenezwa kwa mihogo haha, kuna msabe hii inapatikana iringa vijijini, pyua au gongo bin chang'aa inatokana na sehemu na sehemu, wakati naishi maeneo ya shamsi pale arusha kuna washkaji zangu wa matejoo waliniambia pyua ya pale inamchanganyiko wa hatari, kuna molases humo, mapapai, vidonge vya klorokwini yaani noma tupu
 
Naona unamsaidia mkuu jiwe kutafsiri
Kwa wasiojua 'kiingereza'😀!

"Wewe Ngalikihinja ni mtoto wa nani (ni ukoo gani)? Unamfahamu hata Msongela! Pale Namatuhi ndio kwetu bwana, unamfahamu na Mbema?"
 
Back
Top Bottom