Majina ya Wachezaji Hawa Ni Burudani Tosha

Majina ya Wachezaji Hawa Ni Burudani Tosha

Nakumbuka sana best nilikuwa never miss....nilikuwa ball boy (naokota mipira na kurudisha uwanjani pale ushirika) nikiwa shule ya msingi. Ushirika walikuwa na kocha mmoja Dan Koroso alifundisha soka maridadi sana enzi za kina Bahatisha ndulute, Ofen Martin, Stephen Nyenge, Waziri Ally, Kaunda Mwakiptope, Venance Motto...dah kumbukumbu zinaanza kupotea. Nakumbuka katika msimu mzima wa ligi ni Yanga tu iliweza kuifunga ushirika goli moja, goli lililofungwa na Abeid Mziba kwa kichwa. Timu zote ama ziliambulia sare au ziliondoka na kichapo.

mm naumia sana kuona tuliua timu yetu ya ushirika hivi hivi. sijui ni lini tena tutaingiza timu kwenye ligi ya taifa ..............
nilikuwa nakaa Rau ila mpirani sikuwa naenda as baba alikuwa anasema mpira ni wa wavulana tu, so alikuwa anakwenda na mabraza pekee.
nakumbuka niliwah kuambulia kushuhudia mechi ya ushirika ikicheza na yanga uwanja wa CCP moshi. hi ilikuwa ni mechi ya ufunguzi wakati wa michezo ya majeshi kitaifa. sikumbuki mwaka vizuri ila ilikuwa kama mwezi mzima hivi timu zote za jeshi la polis na wananchi walipiga kambi CCP kulikuwa na michezo yote ilichezwa nafikir ilikuwa kama 1989 ama 1990 hivi. Ushirika wakati huo ni bonge la timu usipime.
 
Huyu Mziba kwa vichwa balaa, nasikia hata penalt alikuwa anatamani apige kwa kichwa
 
Huyu Abdalah Bori,anafanya kazi kwenye kampuni moja kwa sasa ambapo niko nae karibu sana aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa mcheza mpira nikamkatalia kabisa, nimeona anatajwa hapa, kumbe ni kweli. Maana yawezekana enzi hizo nilikuwa mtoto.
Ukamtake radhi kabisa Nyasirori
 
mm naumia sana kuona tuliua timu yetu ya ushirika hivi hivi. sijui ni lini tena tutaingiza timu kwenye ligi ya taifa ..............
nilikuwa nakaa Rau ila mpirani sikuwa naenda as baba alikuwa anasema mpira ni wa wavulana tu, so alikuwa anakwenda na mabraza pekee.
nakumbuka niliwah kuambulia kushuhudia mechi ya ushirika ikicheza na yanga uwanja wa CCP moshi. hi ilikuwa ni mechi ya ufunguzi wakati wa michezo ya majeshi kitaifa. sikumbuki mwaka vizuri ila ilikuwa kama mwezi mzima hivi timu zote za jeshi la polis na wananchi walipiga kambi CCP kulikuwa na michezo yote ilichezwa nafikir ilikuwa kama 1989 ama 1990 hivi. Ushirika wakati huo ni bonge la timu usipime.

Best umenikumbusha tena michezo ya majeshi pale CCP kuanzia soka, basket, netball, kutupa tufe na vikoro koro kibao mikoa yoote it was a full shangwe kwa mwezi mzima kuona manjagu wakipambana aisee....nilikuwa nikitoka shule hadi giza linaingia niko pale...halafu ukirudi home kichapo....

Halafu kumbe ulikaa RAU? Nilikuwa nafika sana pande hizo kuna kinyozi mmoja maarufu sana aliitwa Abunuwasi alikuwa akinyolea chini ya mti hapo RAU....yaani nilikuwa natembea karibu KM 4 kumfuata aisee...

Mida hiyo pia kulikuwa na timu za soka za mashirika ya umma zilikuwa nzuri usipime...mf. Coffe FC, TPC nk halafu kulikuwa pia na Machava FC nimeisikia juzi ndhani imefufuliwa tena.

But all in all Mkuu gfsonwin naona hii trend ya kufa kwa hivi vilabu ni mikoa yote tukianzia na Mwanza Pamba kwishney, Kagera kulikuwa na RTC Kagera ikiwa na mpishi wa mabao aliyeitwa Kasiga Machapati, Pia Tanga Cost ya kina Mgunda na Razack Yusuph ilikuwa tishio bila kuwasahau African Sports ya kina Victor Mkanwa, Mororgoro kukawa na Reli iliyokuwa ikishuka na kupanda daraja kila mwaka ikiwa na wakali kina Dkt Madundo mtambo, then wakaja kina Mbuyu Yondan (Nadhani ni baba yake Kelvin kuna mdau amegusia kw post mojawapo), Mbeya kukawa na Tukuyu Stars ya kina Justine Mtekere na Godwin Aswile (actually Yanga walikuwa wameifanya chuo chao cha mafunzo kwa kuvuna wachezaji wazuri), Songea usipime kukawa na Majimaji ya kina Madaraka Selemani "Mzee wa kiminyio" ambaye alikuwa akiitesa Yanga kama anavyotaka hadi alipokuja Simba. Walikuwepo pia kina Mrope Stephen Nemes nk..Dar kina Plisner enzi za Iddi Pazi na Andrew Godwin, Nyota Nyekundu enzi za kina Omary Mghalike (Mzee wa Offside), Costa Ndunguru...(alikuwa akicheza rafu mbaya!), Idrissa Ngulungu, bila kuisahau RTC Kigoma enzi za kina Sanif Lazaro...dah orodha ni ndefu na muajiri naye ananidai ....

Huyu Mziba kwa vichwa balaa, nasikia hata penalt alikuwa anatamani apige kwa kichwa

Kuna mwaka alikuwa mfungaji bora wa ligi, almost magoli yote isipokuwa moja alifunga kwa kichwa. Huyu alijaacha mpira baada ya kuvunjwa mguu na kipa wa kama sikosei Gor Mahia ya Kenya aliyeitwa Joseph somebody
 
Last edited by a moderator:
Naruhusiwa kutaja majina ya wachezaji waandamizi wa Kijapan?
 
Kuna kipa alikuwa anaitwa Kichochi Lemba. Lakini msisahau majina kama Hamisi Thobias Gaga au Gagarinho (RIP), Kamba Lufo.
 
JUma kachumbali
Paul rwechungura
Juma Kidishi
Athuman China/Juma China.
Salum Kabunda

Huyo jamaa jina lake kamili lilikuwa ni Juma Bakari Kidishi, mchezaji wa zamani wa Malindi ya Zenji....

Hawa jamaa walikwa na timu moja kali sana enzi hizo ikiwajumuisha kina Hassan Wembe, Rifat Said, Edibily Lunyamila, Athanas Michael, Kennedy(Keneth) Malitoli sina uhakika sana na hili jina, pia kulikuwepo na mzungu mmoja toka Bulgaria jina lake limenitoka pia
 
Hahaha sikuwa nimeiona hii...
Miaka ya nyuma kulikuwa na wachezaji ambao majina yao na matendo nadhani vilikuwa vinaendana...
Hapo Coastal Union kulikuwa na jamaa anaitwa Bakari Tutu ​huyo jamaa kuna mechi ashawahi kupiga kibuyu na mchezaji wa timu pinzani hadi gozi la ng'ombe likapasuka...

Wako wengi, ngoja tuwaite watunogeshee mambo hapa...wapo wakuu kina Balantanda, WABHEJASANA, mandieta, ndetichia, watu8, Amiliki, Makoye , Amavubi, Konaball Raia Fulani, Fidel80, Katavi, El Toro, bila kumsahau Saint Ivuga na wengineo wengi. Nadhani wana kumbu kumbu nzuri za majina ya wachezaji waliokuwa wakitajwa tu inakuwa burudani tosha...

Mkuu Dominick Chilambo R.I.P nadhani alikuwa ameshafariki enzi za kina Lubigisa Madata Lubigisa

Umemssahau mtangazaji mmoja aliitwa Dominick Chilambo...alikuwa akianza na Madata Lubigisa, David Mwakalebela, Abdallah bori, George masatu, john makelele, Fumo felician....dah...ukute ni Pamba Vs Ushirika hizo gonga na alivyokuwa akiutangaza utadhani unaangalia kwenye TV..
 
Huyo jamaa jina lake kamili lilikuwa ni Juma Bakari Kidishi, mchezaji wa zamani wa Malindi ya Zenji....

Hawa jamaa walikwa na timu moja kali sana enzi hizo ikiwajumuisha kina Hassan Wembe, Rifat Said, Edibily Lunyamila, Athanas Michael, Kennedy(Keneth) Malitoli sina uhakika sana na hili jina, pia kulikuwepo na mzungu mmoja toka Bulgaria jina lake limenitoka pia

mohamed kachumbari
ally nassoro kibichwa
kipogo shirazi
ikupulika nkoba
nyangema
namajojo
shiwa riambiko
mnyepe
mkude
manga
kaungu
zitto kiaratu
 
Umemssahau mtangazaji mmoja aliitwa Dominick Chilambo...alikuwa akianza na Madata Lubigisa, David Mwakalebela, Abdallah bori, George masatu, john makelele, Fumo felician....dah...ukute ni Pamba Vs Ushirika hizo gonga na alivyokuwa akiutangaza utadhani unaangalia kwenye TV..

George Magere Massatu,bonge la center half wa miaka hiyo
 
Back
Top Bottom