Wizara ya Afya inapenda kuwataarifu waombaji wa ajira za kada za afya zilizotangazwa kwenye Tovuti ya Wizara ajira.moh.go.tz tarehe 21 Aprili, 2023 na kufungwa tarehe 04 Mei, 2023 kwamba taratibu za kuchambua maombi ya kazi zimekamilika.
Waombaji wote waliofaulu na ambao majina yao yameorodheshwa kwenye tangazo hili wanatakiwa kuripoti Ofisi za Wizara katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Mirembe kuanzia tarehe 30 Juni, 2023 hadi 13 Julai, 2023 ili kukamilisha taratibu za ajira.