Majina ya wanaCCM waliochukua fomu za Uspika

Majina ya wanaCCM waliochukua fomu za Uspika

Ni nini sababu za wanaCCM wote hawa kujitokeza mwaka huu 2022 kugombea nafasi ya uspika kupitia chama chao,

  • Je ni ongezeko la demokrasia ndani ya chama cha CCM ?
  • Kutoridhika kwa mwenendo wa Bunge kuburuzwa
  • Wagombea hawa 2022 katika makumi uspika ni dalili mtifuano ndani ya CCM kwa nafasi zote udiwani na ubunge 2025
  • Chama kimeshindwa kudhibiti nidhamu ya wanachama kujipima kikweli kweli wao wenyewe binafsi kuwa "wanatosha" kuwania uongozi ?
  • N.k
Hiyo ni indicator kwamba 2025 sa100 Hana chake.
 
Wengine wamechukua tu form ili kuanza kutengeneza CV zao ijapofika 2024/25...
 
OMBI;- CCM ISIINGILIE KATIKA KUKATA WATU,BUNGE LENYEWE LIMPATE SPIKA WAKE KWA NJIA YA KURA,KILA MMOJA AJIELEZE,AND THEN WAPIGIWE KURA,KWA MIZUNGUKO MITATU KATIKA KUMPATA SPIKA (NAOMBA WAIACHIE DEMOKRASI ITAWALE KATIKA KUMPATA SIPIKA)


Wapigiwe kura watu 71😢😢😢😢😢😢
 
Hiyo ni indicator kwamba 2025 sa100 Hana chake.


Husicheze na Dora chezea sharubu, Hana chake kwa sababu gani labda Hasitake mwenyewe mpende msipende lazima amalize vipindi vyake vyote viwili inshallah
 
Hiyo ni indicator kwamba 2025 sa100 Hana chake.

Ina maana sasa ndani ya CCM kuna wanachama wanaendekeza chokochoko za kupima uwezo wa nguvu ya mwenyekiti wa CCM Taifa, CC Kamati Kuu ya chama na NEC Halmashauri ya Chama katika kusimamia nidhamu yao kupitia utaratibu, mazoea, kanuni, katiba ya chama na viapo vya mwanaCCM kujipima kama anatosha au la ?
 
Hii taarifa ni ya lini?, manake hapo kuna trhe 16/11/2015
 
Sophia Simba, Andrew Chenge, Stephen Maselle, na wengine wote walionyanyaswa na jiwe anafaa kuwa spika

Msukuma na sukuma gang wote wanapoteza muda tu.
 
Hizi ni mfululizo wa nukuu kutoka kwa watia nia kiti cha Spika
Unguja Zanzibar
Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui

LUHANGA MPINA - NINAOMBA USPIKA KURUDISHA MENO YA BUNGE

Chini yangu bunge halitaburuzwa, litakuwa bunge huru na la mfano ktk Jumuiya ya Madola. Tutaishauri kuisimamia na pia hata kukataa miswada isiyokubalika kwa niaba ya wapiga kura wetu ...
 
Nitaleta mabadiliko ndani ya Bunge, hakupepesa anatamani Bunge na wabunge wabadilike ..

Prof. Handley Mpoki Mafwenga ni miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu hizo makao makuu ya CCM Dodoma na ni mtumishi wa Serikali

 
Andrew Chenge : Kila siku nawafundisha , Msiwahishe mambo ninyi waandishi wa habari, acheni chama kiamue nani anafaa kuwania nafasi ya uspika..

 
Naunga mkono hoja
P
Unaunga mkono hoja kwa sababu msukuma sivyo, mbona hujamuunga mkono Tulia Akson?
 
Unaunga mkono hoja kwa sababu msukuma sivyo, mbona hujamuunga mkono Tulia Akson?
P
 
Wanachama wa CCM wanaotia nia kugombea nafasi ya uspika baada ya Spika Job Y Ndugai kujiuzulu January 2022 ni hawa wafuatao :
  1. Andrew Chenge : mwanasheria mkuu wa serikali wa zamani
  2. Sophia Mathayo Simba : Waziri wa zamani wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora), ni Mwenyekiti wa zamani Umoja wa Wanawake Tanzania UWT

https://www.ippmedia.com › habari
Dalili moshi wa kijani U-spika CCM kuanza kuonekana rasmi - IPPMEDIA


8 hours ago — JOTO la uchaguzi wa spika ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi ... Awali kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilipangwa kufanyika juzi...
 
15 January 2022
Taarifa toka makao makuu ya CCM Dodoma pia kutoka Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba na Afisi ya CCM Kisiwandui Unguja Zanzibar .

Wanachama wa CCM wanaotia nia kugombea nafasi ya uspika baada ya Spika Job Y Ndugai kujiuzulu January 2022 ni hawa wafuatao :
  1. Andrew Chenge : mwanasheria mkuu wa serikali wa zamani
  2. Sophia Mathayo Simba : Waziri wa zamani wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora), ni Mwenyekiti wa zamani Umoja wa Wanawake Tanzania UWT
  3. Dr. Mussa Shafii Ngonyani
  4. Wakili Faraji Rushagama
  5. Rahmaddin Rashid Ismaili - mwanafunzi UDSM
  6. Hamisi Rajabu
  7. Festo John Kipate
  8. George Francis Nangale : Mbunge wa zamani Bunge la EALA
  9. Barua Abdi Mwakilanga : mwanadiplomasia toka Buguruni DSM.
  10. Zahoro Rashid Hanuna : Afisa Biashara Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
  11. Thomas David Kirimbunyo
  12. Angelina Bello John
  13. Eng. Abdulaziz Jahad Hussein
  14. Dr. Tulia Ackson : Naibu spika chini ya Job Ndugai
  15. Dr. Thomas Kashililah : katibu wa bunge wa zamani
  16. Stephen Masele : naibu spika wa zamani Bunge la Afrika
  17. Mussa Azzan Zungu : meya wa zamani wa Ilala Dsm.
  18. Joseph Musukuma :
  19. Ezekiel Maige : waziri wa zamani
  20. Asia Juma Abdallah : mkuu wa wilaya wa zamani
  21. Dr. Titus M. Kamani : waziri wa zamani
  22. Tumsifu Mwasamale : Afisa Maendeleo ya vijana mkoa wa Dodoma
  23. Prof. Handley Mpoki Mafwenga : mtumishi wa serikali / umma
  24. Goodluck Mlinga : mbunge wa zamani wa CCM
  25. Prof. Norman Adamson Sigala : mwanasiasa toka jimbo la Makete, msomi mhadhiri
  26. Hatibu Madata Mjega :
  27. Dr. Linda Salekwa Ole Saitabau : mhadhiri chuo Kikuu cha Teknolojia Mbeya na mtafiti wa magonjwa yanayoambukiza na chanjo
  28. Emmanuel Simon Sindama
  29. Bi. Uwesu Msumi
  30. Hilal H. Seif
  31. Wakili Emmanuel Paul Mngare
  32. Athumani Mfutakamba
  33. Wakili Nduruma Majembe
  34. Mwemba Burton Mwemba : marketing expert and media presenter / msanii Mwijaku
  35. Henry Erasto Kessy
  36. Josephat Malima
  37. Adam Nyanyavanu
  38. Eng. Stella Manyanya: mkuu wa mkoa wa zamani
  39. Andrew Kevella
  40. Luhanga Mpina
  41. Hussein Migoda Mattaka
  42. Dr. Godwin Maimu : expert in CAPACITY BUILDING AND MICROFINANCE SERVICES
  43. Mohammed Ali Mmanga : mgombea ubunge wa zamani
  44. Esther Stefano Makazi : Kada wa CCM
  45. Comrade Amos Sollo : Mwanafunzi Chuo Cha Elimu ya Juu
  46. Godwin Kunambi - mkurugenzi wa zamani wa jiji la Dodoma
  47. Goodluck ole Medeye
  48. Juma Hamza Chumu
  49. Baraka Omary Byabato
  50. Hamidu Chamani : kada wa chama, Mtaalam mbobezi wa masuala ya kodi
  51. Fikiri Saidi : mkuu wa wilaya wa zamani
  52. Bi. Dotto Balele Mgasa
  53. Wakili Onyango Otieno
  54. Eng. Samuel Hayuma
  55. Merkion Ndofi
  56. Abwene Majula
  57. Patrick Nkandi
  58. Dr. Edison Wazoel Lubua : Doctor of Philosophy (PhD)Information Systems & Technology
  59. Alex Msama
  60. Samwel Magero : mjumbe wa Kamati kuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA),
  61. Peter Mjemu : mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Chato mwaka 2020
  62. ..



Toka Kumbukumbu mwaka 2015 :
waliogombea nafasi ya uspika toka vyama mbalimbali walikuwa wanane (8) tu

WALIOPITISHWA NA VYAMA VYA SIASA KUGOMBEA NAFASI YA USPIKA 2015​

Jumla ya wagombea nane (8) wamejitokeza kugombea kiti cha Spika wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Katibu wa Bunge, Dkt Thomas Kashilillah amesema, “nimepokea majina nane kutoka vyama nane vya siasa watakaogombea nafasi ya Spika wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano .”

Amewataja waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa ni, Mhe. Peter Leonard Sarungi kutoka chama cha Alliance for Tanzania Party (AFP), Mhe. Hassan Kisabya Almas kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Mhe. Dkt. Godfrey Rafael Malisa kutoka Chama cha Kijamii (CCK), na Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wengine ni Mhe. Goodluck Joseph Ole Medeye kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Richard Shedrack Lyimo kutoka Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Mhe. Hashim Spunda Rungwe kutoka CHAUMMA na Mhe. Robert Alexander Kasinini, Chama cha Democratic Party (DP).

Kwa mujibu wa Dkt Kashilillah, uchaguzi wa Spika utafanyika kesho tarehe 17 Novemba, 2015 kuanzia saa tatu asubuhi katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Mbali na kutaja majina ya wagombea wa Spika wa Bunge, Dkt Kashilillah amesema mpaka tarehe 16/11/2015 jumla ya wabunge 348 wamekwisha sajiliwa.

Aidha Dkt Kashilillah amesema kuwa maandalizi yote kwa ajili ya mkutano wa 11 wa bunge yamekamilika.

Katika mkutano huo wa kwanza wa bunge la 11, kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo kumchagua Spika, Naibu Spika na kuthibitisha jina la Waziri Mkuu

Source : Parliament of Tanzania


January 31 , 2022
Dodoma, Tanzania

MCHAKATO WA NDANI YA CCM KUMPITISHA SPIKA, WABUNGE WA CCM WAMPITISHA MGOMBEA WAO MMOJA KWA KAULI MOJA



Kutoka ukumbi uliopo makao makuu ya CCM mjini Dodoma, Caucus ya wabunge wa CCM kwa kura za wazi wapitisha jina moja lililopendekezwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, jina hilo ni la Dr. Tulia Ackson kuwa mgombea pekee wa CCM. Jumla ya wanachama 69 walijitokeza kuwania kuchaguliwa kuwa wagombea / mgombea wa uspika kupitia CCM.

Source : Wasafi Media
 
Back
Top Bottom