Majini yaliyozagaa Moshi miaka 2002

Kigger

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
850
Reaction score
772
Habari! Wadau kati ya miaka ya 2002 hivi sijui kama nitakuwa nimekosea nilikuwa mdogo sana lakini nakumbuka tukio ambalo lilivuma miaka iyo kuhusu kuzagaa majini ya boss wa adventure pale majengo.

Kipindi iko watu walikuwa wasema wanakutana na majini mara kwenye daladala linatoa mkono kutoka seat ya mwisho konda alipo.

Wengine sijui wanasema wanaingia gest sijui linazima taa yani mambo yalikua mengi.

Kama kuna mtu atakuwa anafahamu hiki kisa basi atujulishe.
 
Mimi nakumbuka ilizuka tetesi kwamba wafuga nywele (Rastafari) wanachuna watu na kuondoka na ngozi kwenda kupiga mnada.

Wanakukamata, wanakupiga nusu kaputi, wanakuchuna ngozi wanaondoka zao.

Nilikuwa nasisimkwa balaa. Ukizingatia kwetu ni huko msituni, kuna mto usiokauka.. Wakadai ndo huko mtoni wanapofanyia usheitwani.

Nakumbuka ni 92 mpaka 94 hivi.
 
majini yapo kila sehemu, hapo kariakoo karibia ya robo unakutana nao ni majini, pale njia panda ya Magomeni mataa kuna majini sana, pwani baharini huko ndio usiseme.

Hata hivyo pwani na mikoani kote mambo hayo yapo, isipokuwa mkoani utakutana na misukule usiku kwenye vichaka au mabonde huko, vipimbi vile vifupii/vistuli, misyuka (kwa wale wenzangu wa mbeya) hivyo mashetan yapo everywhere dunia nzima. hata ulaya yapo though dunia ya kiarabu yamezidi hasa haya ya kimasikini ya kupagawa watu au kuingilia watu wa kiume na kike.
 
Habari! Wadau kati ya miaka ya 2002 hivi sijui kama nitakua nimekose nilikua madogo sana lakini nakumbuka tukio ambalo lilivuma miaka iyo kuhusu kuzagaa majini ya boss wa adventure pale majengo....
Nakumbuka Sana kulikuwa na ya kike yanavutia Kweli na ya kiume pia[emoji28][emoji28][emoji28] Kwa nilivyokuwa nasimuliwa enzi hizo.. sasa sijui ni story au lahh.. maana story zilivuma mpaka miaka ya 2004 hivi nadhani ndiyo ilimfanya mpaka Mh Temba akainguzia kwenye nyimbo yake ya Side Mnyamwezi[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji1430][emoji1430][emoji1430][emoji1430][emoji1430]

#I believe in Jesus of Nazareth..
 
tabora kulikuwa na mfungo wa pipi(ile shepu ya sanda ya maiti za kiislam)[emoji851][emoji851][emoji851]

ilikuwa ni mtihani sana kuamka mapema kuwahi shule,maana story ni kwamba ukikutana nalo linakubaka na kukuua.

mmiliki alikufa yakatawanyika hivyo[emoji1550][emoji1550]
 
Asante kwa kukumbuka iki kisa kilikua kikubwa ezi zile ebu wadau waje watuelezee

Sent from my YAL using JamiiForums mobile app
 
Wabongo mafala sana. Kuna mganga mmoja alikuwa anachukua unga fulani, anauweka kwenye karatasi na kujidai kupiga manyanga. Mara ule unga unawaka moto. Watu wanaanza kustaajabu na kusema huyu ndiye mganga. Kumbe kuna chemical kibao ambazo zikikutana na hewa zinashika moto. Kazi yake ilikuwa kutoa wachawi. Anapiga pesa balaa.

Mwingine anasema kuna popo bawa. Mwingine, mwingine anasema kuna radi na mamba za kutumwa. Yaani mambo ya kifala kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…