Majira yamebadilika sana, badala ya kusubiri watalii waje, tubebe wanyama wetu tukawatembeze hukohuko na pengine kuwauzia kabisa

Majira yamebadilika sana, badala ya kusubiri watalii waje, tubebe wanyama wetu tukawatembeze hukohuko na pengine kuwauzia kabisa

paul sylvester

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2020
Posts
3,503
Reaction score
3,499
Wanajamvi Amani kwenu

Hivi leo dunia imebadilika, majra nayo na nyakati zinazidi kubadilika

Huko tuendako, kwa sababu ya milipuko ya magonjwa na masharti yanayotokana na milipuko hiyo ya magonjwa inatufanya walimwengu tuishi kidizaini kama tulikuwa na utalii. Mtu kusafiri kwenda mahali inamuwia ugumu Kwa sababu ya usalama wa maisha yake.

Nchi yetu kwa takwimu za miaka mitano iliyopita tunaambiwa kwamba tembo wetu nchi nzima walikuwa ni 10k tu. Leo tunaambiwa tembo wamezaliana kama dagaa hadi kufikia 60k+. Hongera kwa serikali kuwalinda hawa tembo na kuongezeka kwake ni matunda ya serikali iliyopo.

Bahati mbaya iliyopo leo wanyama wetu wameongezeka sana, na hii inakuwa ni nzuri hasa kwa watalii kuvutika kirahisi kwa sababu ya ongezeko la wanyama hao. Watalii kuwapa uharaka wa kuona wanyama wengi na kwa muda mfupi pindi wanapotembelea mbuga zetu, lakini sasa kuna hili la Corona.

Je, tunaweza kuwabeba wanyama wetu kuwatembeza huko wanakotokea watalii Ili nchi ijipatie fedha kama kawaida?

Ukiondoa hilo je, sasa kwa kuwa wanyama hawa wameongezeka kiasi cha kuwa wanavamia tu hadi makazi ya wananchi na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi hao. Serikali haioni sasa ni wakati wa kuwavuna hao wanyama pengine kwa kuwauzia mabeberu ndovu Ili serikali ipate mapato ya kuendeleza miradi yake ukiondoa suala la kuwabeba na kuwatembeza huko Ulaya wanyama wetu.

Nasema hivyo Kwa sababu Serikali ndiyo mmiliki wa maliasili hizi. Lakini cha ajabu imekuwa ikipata hasara kubwa kwenye swala la ujangili licha ya kutumia gharama kubwa sana ya kuwalinda hawa wanyama.

Kipindi cha nyuma karibu Kila siku tulikuwa tukisikia majangili yakutwa na ndovu, majangili sijui yamepakia twiga kwenye ndege na kupeleka ulaya kuwauza, majangili yameiba hizi mali na Serikali kuendelea kupata hasara.

Tunapozungumza leo nguvu ya serikali na matunda ya uwekezaji jwa ajili ya kuwalinda wanyama hawa imeenda sambamba na ongezeko la wanyama hawa. Hongera sana kwa hili

Kwa sasa serikali yetu inaonyesha kuzidiwa kiasi cha wanyama hao kuwa kero tena Kwa jamii. Maana hawalindwi ipasavyo, wanavamia mashamba na kuleta maafa kwa wananchi. Umefika wakati sasa wa serikali kufaidi matunda ya uwekezaji wake, na kwakuwa majangili yamedhibitiwa basi serikali ianze kuvuna hawa wanyama Ili nchi ianze kunufaika na uwekezaji huo.

Tumeona baadhi ya wanyama ambao hutumika kama kitoweo kuna mabucha yamefunguliwa. Wananchi tunajiamulia tu kwenye familia zetu, kwamba leo ni aina gani ya nyama tule, basi tunaingia tu kwa mabucha na kuchagua nyama tutakayo.

Swali linabakia kwa hao tembo, kwanza sidhani kama wanaliwa. Sasa ni zamu ya serikali tena iamue kuanza kuwapunguza Ili yenyewe ndio iwe muuzaji mkuu wa ndovu na nchi iendelee kujiletea maendeleo makubwa na kwa kasi


Wajivu wa mambo mnasemaje?
 
Hata kule wana ma ZOO kila aina ya wanyama wapo hadi siafu!

Watalii sababu ya kuja huku sio wanyama kiviile sababu kule wapo kwenye ma ZOo.

Ila wanataka waone wanyama wakiwa kwenye natural habibat zao.

Wazungu pia wengi wao wanakuja kwa ajili ya LANDSCAPE,SCENERY and CULTURE na pia kuja kula dada zetu maana wanasema ni wamoto balaaa
 
Nilifikiri ungehamasisha tubebe wake zetu na watoto tukatalii kukuza utalii wa ndani.
Mkuu, si kwamba watu wanaposema hawana pesa wanaongopa, wanasema kweli kabisaaa,

Uihamasishe familia kwenda kufanya utalii Kwa kutumia kipato gani mkuu
 
Hao wanyama kila mtu agawiwe anaowataka awaweke zizini mwake
Kwani sisi ,sihatujakuwa na lockdown,sasa imekuwaje watalii wasije hata tuwaze kuwapelekea watalii wanyama huko huko walipo? Kweli majira yaenda kasi na sii mchezo.
 
Hao wanyama kila mtu agawiwe anaowataka awaweke zizini mwake
Bujibuji wewe tutakugawia Tembo uone mziki wa kuwalisha. kama ng'ombe wa maziwa tu ni shida kuwalisha,Je tembo?
By the way 'Jiwe' ameshapatikana mahali alipo?
 
TANAPA wafunge kamera nyingi kwenye mbuga watu wawe wana Subscribe wanaingia online wanapata picha live za vijinyama vya pori usiku na mchana na wakati huohuo kipato kinaingia
 
TANAPA wafunge kamera nyingi kwenye mbuga watu wawe wana Subscribe wanaingia online wanapata picha live za vijinyama cha pori usiku na mchana na wakati huohuo kipato kinaingia
Kufanya hivyo pia lazima beberu asiyependwa ashiriki,ama kwa tekinologia, ama vinginevyo.
 
Back
Top Bottom