Majira yametimia ambapo viongozi watakataa viti vyao…

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam!

Ule mwisho uliotarajiwa, unakuja kwa njia ngumu sana na ya kutisha.

Ni majira yameruhusiwa kutokea duniani Ili kuwakusanya watu pande kuu mbili.

Na pande hizi ni pande mbili za kiimani, SI kidini. Yameruhusiwa majira ya vita, ufunguo wa vita hii ulianza 2020 Corona iliporuhusiwa kuingia duniani, sasa ni vita zinaendelea,

Ile vita ya Gaza, Ukraine na Urusi, Kisha Israel na Irani.

Mtu na asikudanganye, hakuna vita kuu ya tatu ya Dunia, vita ijayo ni vita ya kiimani, wamwaminio KRISTO YESU/Yeshua vs wamkataao.

Vita inayoendelea ya Iran na Israel inaenda kukua, marafiki wa Iran wataungana kupigana na marafiki wa Israel. Mbeleni inageuka inakuwa vita ya kisasi kiimani, watakatifu, wamwaminio Yesu wataonekana maadui na kuanza kuwindwa, pa kukimbikia ni huku Nyikani ambako Nabii, Mtumishi wa Mungu atakuwa amekalia kiti Cha ufalme kwa niaba ya Mungu kuruhusu mabadiliko haya muhimu Katika nyanja mbalimbali.

Wazalishaji wa mafuta wataacha kuzalisha mafuta sababu ya vita, mifumo ya kusafiri na usafirishaji itakufa, meli zitazamishwa za kusafirisha Nishati ya mafuta madawa nk nk, ndege zitaangushwa, mambo yatabadikika.

Na Katika vita hii, mataifa yatapigana Hadi kwa nuclear, Hali itakuwa Tete duniani.

Hapatakuwa Tena na mikopo kwa nchi maskini sababu Kila nchi itajifungia kutatua matatizo yake. Ajira zitavurugika, kilimo pekee ndio secta itakayosurvive, shambani ndio patakuwa mahali salama.

Umoja wa Mataifa utasambaratika sababu ya vita na uchumi kuwa mbaya na uchumi wa Dunia kuanguka.

Nchi za Afrika zitataabika sana sababu hapatakuwa na mawasiliano na nchi za huko mbali, nchi za Afrika zitalazimika kutafuta namna ya kujitegemea.


VIONGOZI WATAKIMBIA NAFASI ZA KISIASA.

Katika Hali hii ngumu, hapatakuwa na pesa za kuiba, Hali itakuwa Tete, viongozi wasio na dira na wezi na mafisadi watatimuliwa na wananchi sababu Hali itakuwa ngumu,

Itafika time, kiongozi anakosekana, Kila atakayechaguliwa, ataogopa sababu ya hali ngumu.

Ndipo kutainuka viongozi sahihi waliochaguliwa na Mungu kuzisaidia Nchi za Afrika kwa njia ngumu, Wataibuka Marais watakaoisaidia Afrika kuzalisha chakula na kujitegemea, Afrika itailisha Dunia na Nchi tajiri zitarudi kuomba msaada Africa.

Injili itahubiriwa duniani kote kutokea Africa, Utaotokea uamsho mkubwa kuanzia Afrika kwenda Dunia nzima kuwakusanya wana wa Mungu.

Watakatifu watakusanywa KUPITIA Hali hii ngumu ijayo iliyoruhusiwa, na hapo ndipo unyakuo utaotokea.


Na Tanzania ndio nchi itakayokuwa funguo kuongoza Afrika kuwa dola kuu na kuongoza uamsho wa kiuchumi, kiimani kwa Kristo Yesu nk nk.


Ni lini?

Ni majira haya haya ya miaka 7. Yaani 2021-2030....

Mungu ibariki nyikani.

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿

Aamen
 
Gentleman,
hii si ramli na imani potofu za kishirikina kabisa?
kuna hatua za maendeleo zozote zinaweza kupigwa na jamii yenye fikra useless kama hizi kweli?🐒
 
Gentleman,
hii si ramli na imani potofu za kishirikina kabisa?
kuna hatua za maendeleo zozote zinaweza kupigwa na jamii yenye fikra useless kama hizi kweli?🐒
Asipo angalia anaweza jikojolea kitandani 🤔
 
Hadi hali inafikia hapo, wewe na familia yako mtakuwa mshakufa zamaaaaaani.
 
Acha na mimi nivute kidogo ili niweze kuendana na ndoto zako... Afrika iilishe dunia kwa kilimo cha jembe la mkono?
Tanzania iongoze Africa kuwa dola kuu wakati hatupo hata top 5 ya nchi zenye viwanda afrika?
 
Katika Hali hii ngumu, hapatakuwa na pesa za kuiba, Hali itakuwa Tete, viongozi wasio na dira na wezi na mafisadi watatimuliwa na wananchi sababu Hali itakuwa ngumu,
Sawa umeandika vyema lakini kwenye hili watakaoumia ni Wananchi wa kawaida peke yao. Vyombo vingine vitakuwa vina neemeka tu.
Ila tu na wao wataishi kwa wasi wasi mkubwa.
 
Hebu jiongeze soma kuhusu “Operation Ajax” ya mwaka 1953 kwanini Ml6 na 🇺🇸 walitaka kumuondoa Mohammed Mossadegh wa Iran ndio utajua wazungu ni makanjanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…