Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Aha mkuu sasa wewe ndio mtu sahihi wa kutuhabarisha sisi huku kama matukio kama haya yapo huko, na ikitokea inakuwaje maana comments za uzi huu nyingine zinaona wanaopenda kuchungulia mambo ya jirani wako sawa.
 
Hapa kuna mambo matatu
1. Tabia ya kutaka kujua jirani anafanya kazi gani, hata kama huyo jirani hajakuletea tatizo

2. Kuona mwamba yuko vizuri kila idara wakaanza kuwa na hisia tofauti. Angekuwa na maisha "mabaya " je ingekuwaje

3. Kumripoti kwa walinzi wa amani na kutoa taarifa kwamba mwamba sio raia mwema.

kwa upande wangu Mwl. Julius Kambarage Nyerere alikuwa sahihi kupiga vita ujinga kwa kutoa elimu bure kabisa kabisa ila naona alifanikiwa asilimia moja. Katika hiyo moja mimi nimo humo.
 
wabongo wanapenda kilamtu ahangaike🤣🤣🤣
ukila kilaini wanakushtaki maaamaeeee
Ndiyo maana sisi wajanja tunajua namna ya kufanya kamwe hutasikia kelele kama hizi
Kula nyama nyamaza
 
Vibongo vingine vina roho mbaya tu apo ata hakiwadai fidia laki 5 hawana vitabaki kulialia tu
 
Mbaya zaidi majirani pesa ya kumlipa hawana, Watauza hadi mkundv hahah
 
kwahiyo wewe unataka jirani akupe taarifa zake zote za njia ya kipato chake sio?
Swala sio kunip taarif zote,kumbuk kuw hata litakapotokea janga lolote katik mazingir mnamoishi ni sisi majiran tutakaotumik kusaidia/kuwajibik juu ya hilo.pengne wew ujawai ishi nchi za watu pengine ungejua watu wanavyojali usalam wao.hili jambo limejikita San kwny swala la usalam kiukwel huwez ishi na mtu ambae humu elew ama anaejengea watu hofu
 
suala la kutokujua njia za kipato za jirani yako linakueaje tatizo kwako? hapo suala la usalama wako linahusikaje? wabongo umebea unatutesa sana. sasa Jirani anaeishi nyumba nyengine unataka umuelewe ili iweje? typical mambo ya kibuzabuza tu
 
Aha mkuu sasa wewe ndio mtu sahihi wa kutuhabarisha sisi huku kama matukio kama haya yapo huko, na ikitokea inakuwaje maana comments za uzi huu nyingine zinaona wanaopenda kuchungulia mambo ya jirani wako sawa.
Mkuu,

Huku ukitaka unaweza kuishi miaka 20 jirani wa nyumba ya pili humjui.

Kila mtu na mission zake.
 
Naziona pande zote mbili hapa, ingawa ni kwa kutumia taarifa chache/ finyu zilizowakilishwa hapa.

Kwa upande mmoja, majirani labda wamehisi au wameona kitu ambacho si sawa.

Katika spirit ya ‘if you see something, say something’, wakaenda polisi kutoa taarifa.

Kwa hilo naelewa. Maana tuseme labda jamaa angekuwa ni ghaidi na humo ndani kwake anashinda na kupanga maafa, halafu itokee siku moja anafanikiwa, watu wangehoji mengi sana ikiwemo kwa nini majirani hawakusema chochote walipohisi kuna jambo ambalo haliko sawa hapo nyumbani kwake.

Kwa upande mwingine, naiona na kuielewa haja ya ‘mind the business that pays you’ [mind your own damn business].

Ni suala la balancing act: watu kujali mambo yao na kwa wakati huo huo kuwa ni concerned citizens.

Polisi baada ya kumhoji, kama wangebaini anajihusisha na mambo haramu, hao raia ‘wema’ wangepongezwa.

Lakini kwa vile jamaa hajakutwa na chochote kilicho haramu, ni rahisi sana kuwalaani majirani kwa kuyafuatilia maisha ya jirani mwenzao.

Mwisho, ukweli wa mambo ni kwamba, sisi binadamu tunapenda sana kufuatiliana. Ni asili yetu kuwa wadadisi.
 
Ta
Tangazo limekaa kibingwa
 
suala la kutokujua njia za kipato za jirani yako linakueaje tatizo kwako? hapo suala la usalama wako linahusikaje? wabongo umebea unatutesa sana. sasa Jirani anaeishi nyumba nyengine unataka umuelewe ili iweje? typical mambo ya kibuzabuza tu
🤣 Mwanang kuw uyaone ama tembea ujue mazamzam ya Dunia.
 
Mkuu tatizo sio kupeleka repoti Polisi, bali sababu iliowafanya wapeleke hio ripoti. Mtu kuwa na maisha mazuri alafu mkawa hamzijui mishe zake ndio sababu tosheleza za kukufanya muwe na shaka nae na kwenda kupeleka repoti polisi?
 
Walichoenda kukiripoti polisi ni kipi hasa? Unayo ripoti yao neno kwa neno?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…