Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Ila wabongo na somebodyelse life 🙌🏽😁… Sasa hapo wanaridhika wenyewe baada ya kujua issues zako

Mimi askari wakinihoji nawaambia mimi nauza ushauri wa mahusiano kwa waliokutwa na majanga kwa njia ya mtandao.
 
Na ndio maana kuna Mabalozi wa mitaa, walitakiwa walifikishe kwa balozi kisha baloz ndo alifuatilie kwa hekima likimshinda ndio alipeleke polisi.
Kutoa taarifa unaweza kutoa taarifa wakati wowote mahali popote ukiona kuna viashiria vya uhalifu... haijalishi kama una uhakika au hapana..., kazi ya upelelezi sio yako ni ya polisi na sio kila taarifa lazima waifuate bali wataichunguza, pia wanashauri sana raia kutoa taarifa pindi wakiona mambo ndivyo sivyo...
 
Wewe hujui walisema nini kule polisi. Kwa ninavyojua, ukienda kutoka taarifa za kumshuku mtu, asingekuja kukamatwa km mwizi. Kuna wengine wanaenda mbali na kusema ni mwizi sababu tukiacha vijiko havionekani n.k. Hiyo tayari inaweza kufanya polisi wakukamate. Hata km ni Mimi, Tangu nizaliwe sijawahi kwenda police, alafu Kwa sababu tu za wivu unanipeleka kule, aisee....
Kama wameenda kumshitaki kama mwizi, hilo ni kosa sasa.
 
Wakuu Kuna jamaa hapa mtaani alikua anahisiwa anafanya shuguli haramu sababu anamaisha mazuri ila kazi yake haijulikani anashindwa ndani akitoka jioni

Sasa Kuna majirani wawili wamemripoti polisi akaja kukamatwa. Sasa akiwa huko polisi akasema yeye kazi yake ni kubeti na analipa Kodi Kwa serikali kupitia mikeka yake anayoshinda na kweli kaonyesha mikeka anakula mamilioni ya pesa ni aina ya watu wanaoweka pesa nyingi sana kwenye mechi.

Sasa kingine kaenda mahakamani anawashitaki majirani zake hao wawili Kwa kosa la kumdhalilisha na kumpotezea mda wa kufanya mambo yake ya msingi na anadai fidia million 500 na ana mawakili wake kabisa wa 3

Hivi hii kesi anaweza kushinda huyu jamaa ishu ipo serious sana
Basi usikute hao waliokwenda kumshitaki mahakamani ni kina Juma kisa tu kwa sababu wao hawana kazi.
 
Kumbe tunaongelea hisia hapa ? Kama ni hisia basi tunaweza kusema lolote tunalotaka hapa nimejibu accordingly na mada ilivyoletwa hayo mengine ni ya ziada na ndio yatajulikana huko na hapo atashitaki vitendo vya lugha mbovu kwake na sio kuwashitaki wadau kutoa taarifa polisi

Hivi mkuu unajua kusoma kilichoandikwa au una uwezo wa kuongezea yako ya kwenye mawazo yako hata kama hayajaandikwa ? Kwamba ni ajabu kwa watu kupeleka kesi ambazo hazina mashiko na mwisho wa siku kutupiliwa mbali ?

Na hii taarifa umeitoa wapi kwa mleta uzi au kichwani mwako ?
Ngoja nkuache , we endelea kutimzama jamaa kama mwehu kwa kuwashitak hao majiran kwa udhalilishaj

Tusema jamaa tumweka kwenye lile kundila wehu wafungua kesi zisizo na kichwa wala miguu
 
Back
Top Bottom