Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Kumhisi mtu ukamhusisha na uharifu ni kumdharirisha, hata kama taarifa hiyo ilipelekwa Polisi.
Polisi wana kinga, ndiyo maana hawakupaswa kuwataja watoa taarifa sababu watoa taarifa hawana kinga dhidi ya taarifa wazitoazo pia zinaweza kuwarudia ikiwemo kufunguliwa kesi au visasi vinginevyo.
Mtoa taarifa si mkosaji mbele ya Polisi, lakini ni mkosaji kwa yule aliyetolewa taarifa. Aliyetolewa taarifa ana haki ya kuishi maisha yake, sheria haimlazimishi kujitangaza shughuli zake kwa majirani.
 
Kama halijafika kwèñye Umma.
Mtoa Mada angejuaje?

Polisi wanapokuja kukuchukua Hapo mtaani unafikiri wanakuja kuzidi Umma usijue?

Hao lazima wakutwe na Kesi ya kujibu.

Tangu lini Hisia za Mtu sikapelekwa Polisi au Mahakamani?

Unajua Kwa Wengine Polisi kuja nyumbani Kwao Kwa Kesi isiyo na kichwa Wala miguu ni kuwaumiza kihisia?
 
Naile
d. Labda hao majirani zake amewakadiria na kuona wepesi. Lkn nje na hapo ajipange hiyo hela ya kubeti kulipa gharama za kesi baadae, kama hawana wakili waweke tu mlipaji yupo huyo huyo
 
Hamna kesi hapo,kwani ukienda kumripot mtu unatoa na taarifa kabisa?
Amedhalilishwa vipi?kikubwa kazi yake imejulikana.
 
Watu wanaongea kiurahisi sana. Hao jamaa hawana kinga, lazima walipishwe mzigo mrefu.
 
Huo utakuwa upumbavu wa hali ya juu wa Polisi, na labda ni kawaida yao. Polisi hawapaswi kwenda kumchukua kwa sababu kuna mtu kasema ana shaka nae, wanapaswa kupeleleza. Wakimchukua kwa ajili ya tuhuma watamfungulia jarida la kesi litakalosema nini, kuna watu wana shaka na chanzo cha fedha zako?

Na pia, Polisi wanapomchukua mtu hawaitishi mkutano kuutangazia umma kwa nini wanamchukua.

Sasa suala la mtoa mada amejuaje yeye anapaswa kutuambia. Lakini ni wazi amejua kwa kuwa huyo bwana amefungua kesi.

Upumbavu wa Polisi hapo pia unaweza kuwa, huyu bwana amejuaje kwamba jirani zake ndio wamemripoti? Hao waliomripoti wanaweza kuwafungulia mashitaka polisi kwa kuvujisha taarifa zao!
 
Watu wanaongea kiurahisi sana. Hao jamaa hawana kinga, lazima walipishwe mzigo mrefu.

Hata kama Stori NI chai lakini inaweza Kutoa Mafunzo miongoni mwetu.

Kitendo cha Afisa kubeti kujua waliomtuhumu Polisi tayari ni Umma umejua.

Alafu Hisia za kîla Mtu zikipelekwa Huko Polisi au Mahakamani si itakuwa sokomoko.
HISIA pekee NI ramli chonganishi.

Mtu kuanzia kuhangaika Huko Polisi alafu Kwa kuhisiwa tuu huo NI usumbufu àmbao lazima ulipiwe ikibainika NI hisia za uongo.
Kwa Sababu kama ikithibitika Hisia zilikuwa za kwèli Aliyepelekwa Polisi angewajibishwa
 
acharoho mbaya
Kuwa na wasiwasi ni jambo ka kawaida na mahali walikopeleka taarifa ni mahali sahihi.
Sasa hivi kuna matukio mengi ya ajabu kwa hiyo kutoa taarifa ni muhimu.
Kazi kubwa ya polisi ilikuwa ni kumpeleleza huyo mtu na kujua kazi anayoifanya ,sioni kosa la watoa ripoti
 
Anashinda kiulaini kabisa, pengine hata hiyo kushikwa ni mchongo wake.
 
Umeingea point.
Kwa hisia zao juu ya watu wengine, watoa taarifa wana msaada mkubwa sana kwa Polisi.
Bahati mbaya kwao, mbele ya Mahakama watatakiwa kutoa facts, siyo hisia.
 
Hao majirani kazi zao ni zipi kwanza maana hadi wanapata muda ya kufuatilia ya watu watakuwa madon wa mtaa nini?
 

Wewe kuwa na shaka na Mtu hauna tofauti na ramli chonganishi àmbalo ni Kosa Kisheria
Huna tofauti na Mganga WA kienyeji anayetumia Hisia Zake kushuku Watu.

Mahakamani atafunguliwa Jalada la kumtuhumu mtu Kwa kufanya Kazi haramu, Ambazo hajazitaja.

Hiyo Kesi haina tofauti na Kesi ya Mwijaku Vs Masoud Kipanya
 
Umeingea point.
Kwa hisia zao juu ya watu wengine, watoa taarifa wana msaada mkubwa sana kwa Polisi.
Bahati mbaya kwao, mbele ya Mahakama watatakiwa kutoa facts, siyo hisia.
Watoa taarifa sio lazima watoe ushahidi mahakamani, labda iwe wanatoa taarifa juu ya tukio waliloshuhudia. Kwa suala kama hili, kwa mfano ingekuwa kweli mripotiwa alikuwa anafanya mambo haramu, ingekuwa ni juu ya Polisi kupeleleza na kupata ushahidi wa kumtia hatiani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…