Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

MAJIRANI wawili ndio walimshitaki na walikua polisi na yeye akiwepo
Hapo ndipo walipojichanganya...

Mambo kama haya inabidi uwe "Anonymous"..


Unaenda kutoa taarifa kisha wewe identity yako inakuwa siri..

Sasa kwa style hiyo waliyoenda nayo jamaa ana haki kuwashitaki pia, maana wao hawajaenda kutoa taarifa ya kumtilia mashaka, bali wameenda ku-accuse directly.
 
kwa hiyo jirani kutoa ripoti polisi ni vibaya?haya incase ikiwa jamaa alikuwa drugs dealer?

mahakama haitatenda haki,kwani hiyo ni kawaida kuhisi.
Wala sio. Wao walitimiza wajibu wao,walikua sahihi. Na sasa jamaa naye aache atimize wajibu wake kwa mujibu wa sheria. Naye yuko sahihi. Kwakifup wote wako sahihi.

Acha majirani wapambane na uhalisia. Kwan hawakuwah sikia usemi wa "no research not right to take action"???
 
Sheria ya Whistle blowing inawalinda hao majirani wala wasibabaike wao walitoa taarifa Polisi kwa nia njema kutokana na wasiwasi waliokuwa nao. Hivyo wasishituke, Polisi watakuwa mashahidi wao wazuri tu.
 
Hakuna kosa, wao wameeipoti wasiwasi wao isije kuwa wanaishi na jambazi sugu mtaani, uchunguzi umefanywa na polisi na hao jamaa hawakumtuhumu moja kwa moja..... Wakihukumiwa wananchi hawatakuwa tena na uhuru wa kuripoti pale wanapokuwa na maqhaka na watu ama kikundi cha watu
 
Reactions: UCD
Ninachohisi jamaa aliwaambia polisi wamtajie na nadhani aliwapa pesa maana jamaa yupo vizuri kipesa
Hapo mi kama jirani nawakataa polisi mchana kweupe kabisa labda niwe nimesaini maelezo kwa dole gumba ila bila hivyo nawakataa kweupe
 
Sheria ya Whistle blowing inawalinda hao majirani wala wasibabaike wao walitoa taarifa Polisi kwa nia njema kutokana na wasiwasi waliokuwa nao. Hivyo wasishituke, Polisi watakuwa mashahidi wao wazuri tu.
Wakamuulize huyo whistle blowe maarufu Snowden alivyonusurika.
Sheria mbele ya wabobez hainaga jibu la moja kwa moja. Inategemeana na vile unavyoitafsi na kuijua madhaifu yake in correlation to other situations. Kuna loopholea kwenye kila the so called sheria
 
Hawezi kushinda hiyo kesi, ni jukumu la mwananchi kutoa taarifa polisi kwa mtu asiyemuelewa, raia hawajamfungulia mashitaka bali wametoa taarifa polisi, wafanye kazi yao.
 
Aisee hii ni hatari na jamaa yupo serious
 
Ila watanzania, 🙌
 
Hawezi kushinda hiyo kesi, ni jukumu la mwananchi kutoa taarifa polisi kwa mtu asiyemuelewa, raia hawajamfungulia mashitaka bali wametoa taarifa polisi, wafanye kazi yao.
Sawa ngoja tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…