Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

wabongo wanapenda kilamtu ahangaike🤣🤣🤣
ukila kilaini wanakushtaki maaamaeeee
nilivyotoka chuo nikaenda kwa mzee,nikamiliki kila kitu chake,na mzee kwenye inshu za pesa huwa hana habari kabisa,yeye ilimradi kazi zinaenda

Hii hali ya kupewa kila kitu iliwachukiza sana wanajamii utazan mali za mzee zilikuwa zao
 
Kuna kosa la kutoa taarifa ili polisi wafanye uchunguzi ?!!! Au anawashitaki kina nani ? Au huo ni mpango wake wa kuvuna pesa za wadau kwa kufundisha hio so called mbinu yake ya kupata mamilioni kwa kubeti ?
Kwa kupata mamilioni Kwa mbinu anayotumia Kwa masikini ni ngumu sababu jamaa anabeti mechi Moja anaweka hata million 10
 
Kuna kosa la kutoa taarifa ili polisi wafanye uchunguzi ?!!! Au anawashitaki kina nani ? Au huo ni mpango wake wa kuvuna pesa za wadau kwa kufundisha hio so called mbinu yake ya kupata mamilioni kwa kubeti ?
Anataka kubet mahakamani pia 😄
 
Kuna kosa la kutoa taarifa ili polisi wafanye uchunguzi ?!!! Au anawashitaki kina nani ? Au huo ni mpango wake wa kuvuna pesa za wadau kwa kufundisha hio so called mbinu yake ya kupata mamilioni kwa kubeti ?
Unapoamua kutoa taarifa uwe umejiridhisha, otherwise huna kinga. Hapo wa kulaumiwa ni Polisi kwa kutoa taarifa za watoa taarifa. Polisi wana kinga kisheria, wangeweza kufanya kazi yao bila kuwataja watoa taarifa. Kitendo cha kuwataja watoa taarifa kinapelekea kujenga uhasama ndani ya jamii na hatimaye watu kuishi kwa visasi na hata kuumizana au kutiana hasara.
Mfungua madai yupo sahihi sababu amedharirishwa kwa kuwa hakuna sheria inayomtaka kujitambulisha yeye na shughuli zake kwa majirani.
 
kwa hiyo jirani kutoa ripoti polisi ni vibaya?haya incase ikiwa jamaa alikuwa drugs dealer?

mahakama haitatenda haki,kwani hiyo ni kawaida kuhisi.
We naye mwehu, sasa mahakama haitendi haki kwani hapo mahakama imeshatoa maamuzi yoyote? Wale walivyoreport polisi ni sawa maana kama mtu unamuhisi vibaya una uwezo wa kumreport na polisi walivyofanya naye mahojiano ni sawa pia, na wamejiridhisha kuwa jamaa ni mtu wa kubet tu na wamemuachia aendelee na mambo yale kwahiyo hadi hapo hakuna aliyekosea. Ila jamaa yeye ameona amedhalilishwa na ameamua kwenda mahakamani, ni haki yake pia hivyo tuiachie mahakama ifanye kazi yake.
 
Unapoamua kutoa taarifa uwe umejiridhisha, otherwise huna kinga. Hapo wa kulaumiwa ni Polisi kwa kutoa taarifa za watoa taarifa. Polisi wana kinga kisheria, wangeweza kufanya kazi yao bila kuwataja watoa taarifa. Kitendo cha kuwataja watoa taarifa kinapelekea kujenga uhasama ndani ya jamii na hatimaye watu kuishi kwa visasi na hata kuumizana au kutiana hasara.
Mfungua madai yupo sahihi sababu amedharirishwa kwa kuwa hakuna sheria inayomtaka kujitambulisha yeye na shughuli zake kwa majirani.
Kumdhalilisha kwa kutoa taarifa polisi ? Ametoa taarifa polisi au ameandika kwenye magazeti au kuwatangazia watu ? (angetangazia jamii hio ndio ingekuwa slander) ila kama ametoa taarifa kwamba jamaa simuelewi ni kwamba amewapa kazi polisi wafanye uchunguzi (sio wamshike) bali wachunguze sasa kama walimshika bila uchunguzi wa kina huo ni uzembe wa polisi sio mtoa taarifa..., vilevile polisi wana haki ya kuja kuchunguza kuna nini kinaendelea kama wana vibali maalumu ni kama ukisimamishwa kwenye gari na kuombwa leseni yako haimaanishi wamekwambia hauna leseni ?
 
Nakazia hii ni chai
#kataa chai
#chai ya moto ni hatari sana kwa afya💔
e48cf8504295a355cb61b0993a65f09a.gif

Wakuu Kuna jamaa hapa mtaani alikua anahisiwa anafanya shuguli haramu sababu anamaisha mazuri ila kazi yake haijulikani

Sasa Kuna majirani wawili wamemripoti polisi akaja kukamatwa. Sasa akiwa huko polisi akasema yeye kazi yake ni kubeti na analipa Kodi Kwa serikali kupitia mikeka yake anayoshinda na kweli kaonyesha mikeka anakula mamilioni ya pesa ni aina ya watu wanaoweka pesa nyingi sana kwenye mechi.

Sasa kingine kaenda mahakamani anawashitaki majirani zake hao wawili Kwa kosa la kumdhalilisha na anadai fidia million 500 na ana mawakili wake kabisa wa 3

Hivi hii kesi anaweza kushinda huyu jamaa ishu ipo serious sana
NI hivi, kesi ya kudhalilisha inahitaji umdhalilishe au umtukane mtu kwa tuhuma au taarifa za uongo kwa uma (public) katika namna ya tangazo, matamshi au chapisho. Kumripoti mtu polisi sio kumdhalilisha, hata kama hizo tuhuma a u taarifa itakuja kuthibitika sio za kweli, kwa sababu unaporipoti polisi hakuna uma unaohusika ambao utakufanya wewe uone hadhi yako imechafuliwa. Upelelezi wa polisi hautangazwi hadharani, na wao walienda kuripoti polisi in confidence kwa nia nzuri sio kudhalilisha. Polisi wangechunguza kwa siri, kama ilivyo kawaida. Kama polisi waliwatangazia watu juu ya hiyo taarifa waliyopewa wao ndio wanapaswa kushitakiwa.

Kimsingi, kitendo cha huyu mtu kwenda kuwafungulia mashitaka hawa watu kimemdhalilisha kuliko wao kwenda kuripoti polisi, kwa sababu yeye ndie amelifanya jambo hili lifike kwenye jumuia. Kwa hiyo amejiddhalilisha mwenyewe. Hii kesi atashindwa, ni bora aifute asije akalipishwa gharama za kesi. Hao wanasheria wanamdanganya wanataka kumlia hela yake tu wakijua hakuna kesi hapo
 
Kumdhalilisha kwa kutoa taarifa polisi ? Ametoa taarifa polisi au ameandika kwenye magazeti au kuwatangazia watu ? (angetangazia jamii hio ndio ingekuwa slander) ila kama ametoa taarifa kwamba jamaa simuelewi ni kwamba amewapa kazi polisi wafanye uchunguzi (sio wamshike) bali wachunguze sasa kama walimshika bila uchunguzi wa kina huo ni uzembe wa polisi sio mtoa taarifa..., vilevile polisi wana haki ya kuja kuchunguza kuna nini kinaendelea kama wana vibali maalumu ni kama ukisimamishwa kwenye gari na kuombwa leseni yako haimaanishi wamekwambia hauna leseni ?
acha kupanic au wewe ndio hao madada majirani? Mahamaka itaamua
 
Back
Top Bottom