Majirani zetu na kufundisha kiswahili mashuleni

Wana JF,

Leo Tarehe 5/7/2023 asubuhi wakati nasikiliza BBC kupitia Radio Free Afr., nimeshangaa kusikia kwamba nchi moja wapo ya majirani zetu wameamua kufundisha lugha ya KISWAHILI katika primary schools zao.

Sasa, kilichokuja kunishangaza ni kusikia mwalimu shuleni akiwafundisha watoto kwamba siku ya Jumatano ni siku gani ya week? Wanafunzi wote wakasema Jtano ni siku ya Tano ya week.

Hivi kiukweli mniambie, siku ya Juma tano -J5 tunavyoelewa hapa Tanzania ni siku gani au siku ya ngapi ya week?

Nasubiria majibu..........
Hao ndio wako sawa.

Jumamosi ni siku ya kwanza katika wiki.
 
Wiki haina siku 30 , bali ina siku saba
hapo vipi 👇👇👇👇👇👇👇👇👇2 Petro 3:8 “Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
 
Hiyo ni kwa Mungu,bali siyo kwa wanadamu.halafu huyo petro alikuwa binadamu kama wewe, ila tu alikuwa mwanafunzi wa Yesu.

Sasa siku zote akili ya mwanafunzi huwa ailingani na mwalimu
 
Hizo siku 7 za wiki unazipata wapi...
 
Wana JF,

Leo Tarehe 5/7/2023 asubuhi wakati nasikiliza BBC kupitia Radio Free Afr., nimeshangaa kusikia kwamba nchi moja wapo ya majirani zetu wameamua kufundisha lugha ya KISWAHILI katika primary schools zao.

Sasa, kilichokuja kunishangaza ni kusikia mwalimu shuleni akiwafundisha watoto kwamba siku ya Jumatano ni siku gani ya week? Wanafunzi wote wakasema Jtano ni siku ya Tano ya week.

Hivi kiukweli mniambie, siku ya Juma tano -J5 tunavyoelewa hapa Tanzania ni siku gani au siku ya ngapi ya week?

Nasubiria majibu..........
Neno ‘mosi’ linamaanisha ‘kwanza’ , sasa anzia hapo
 
Lakini nafikiri kuna tatizo sehemu furani. Kwanza tujiulize, nani aliumba hizi siku? Na kwanini mpaka leo hakuna juma moja (a week ) lenye siku zaidi ya 7? Ina maana tukirudi kwenye Biblia Kitabu cha Mwanzo 1:1-30 Mungu ndie anajua zaidi kuhusu hizi siku mpaka alipoumba mwanadamu siku ya sita (6) .
Akamaliza hapo alafu katika kitabu cha Mwanzo 2:1-2 akaiweka hiyo siku ya 7 na akamwambia mwanadamu apumzike ktk siku ya 7- Saba ya week na Mungu pia akapumzika siku hiyo.

Sasa, hiyo Jumapili, uliyosema kwamba ndo siku ya 2-Pili ya week, Bibblia katika Luka 24:1-3 inasema ni siku ya Kwanza ya week ( First day of the week) siku ambayo Yesu alifufuka kutoka kaburini.

Kwahiyo, Kalenda ya Roman Katoliki iko sahihi sana maana inaanza week na siku ya Jumapili. Tafuta hata kwenye Dictionery inasema hivyo pia.

Therefore, Juma tano ni siku ya Nne ya week- 4th day of the week.

Waliopata hili swali so far ni watu wawili katika JF. Big- up.
 
Kikatiba siku ya kwanza ya juma ni Jumatatu

Kibiblia siku ya kwanza ya juma ni Jumapili
Very Good Equitable umelipata jibu la swali.
You are very clever, excellent, second to none!!!
 
Neno ‘mosi’ linamaanisha ‘kwanza’ , sasa anzia hapo
Mku jiongeze ufurukute kutafuta maarifa. Kwani Vitabu vya Dini vinasema Yesu alifufuka Jumamosi?
Hayo ni majina tu. Ukweli uko katika Biblia maana Mungu ndie aliumba hizi siku. Soma tena Luka 24:1-3 ujue siku ya kwanza ya week ni siku gani. Fanya reference pia kwenye Dictionery uelimike mku usikae na mawazo mgando.
 
Lugha ni maelewano, sio dini
 
Back
Top Bottom