Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Wakuu asalaam !
Kwa mujibu wa sheria, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliundwa kwa lengo la kuchunguza, kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa nchini Tanzania. Inatakiwa iwe nguzo ya haki na mwanga wa matumaini kwa kila raia anayetafuta msaada dhidi ya dhuluma na ufisadi.
Lakini uhalisia ni tofauti.
Kwa uzoefu wangu binafsi nilipopeleka ushahidi wa maandishi, taarifa za kina, tarehe, muda, na namba za simu, nilitarajia kutendewa haki kwa weledi na heshima. Nilifanyiwa mahojiano ya saa mbili, maelezo yakachukuliwa kwa kurasa kadhaa, kisha nikaambiwa nitapigiwa simu.
Nilipoitwa tena, nilikutana na afisa niliyeambiwa ndiye mwanasheria wa TAKUKURU. Muonekano wake, mavazi yake, na maneno yake viliniacha na mashaka: badala ya kuzungumza kwa taaluma na heshima, alizungumza kwa masihara na kejeli, akinitolea kauli za kutojali. Hapo nikajiuliza je, hii taasisi bado inatetea wananchi, au imegeuka kuwa sehemu ya kuua haki?
Kwa nini naona majukumu ya TAKUKURU yahamishewe JWTZ
1. Nidhamu na weledi wa hali ya juu
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limejijengea heshima ya nidhamu, utiifu wa sheria na maadili ya kazi. Hili ni jambo ambalo kwa sasa TAKUKURU inalipoteza.
2. Ulinzi dhidi ya ushawishi wa kisiasa na rushwa
Afisa wa jeshi mwenye cheo kuanzia Kapteni ana mafunzo na nidhamu ya kustahimili vitisho na vishawishi. Hii itasaidia kulinda uadilifu wa taasisi ya kupambana na rushwa na dhuluma.
3. Kukaribisha wananchi kwa heshima na usalama
Wananchi wanapopeleka mashauri yao kwa JWTZ, wanajua wako mikononi mwa taasisi inayoheshimu kiapo chake cha kulinda taifa na watu wake.
4. Ufanisi wa utendaji
JWTZ ina mfumo wa mawasiliano wa haraka, unaojali matokeo na unaoweza kuhakikisha mashauri yanashughulikiwa bila urasimu unaokwamisha haki.
Kila wilaya iwe na ofisi maalum ya kupambana na rushwa na dhuluma iliyo ndani ya kambi ya JWTZ.
Ofisi hizo ziendeshwe na maafisa wa JWTZ wenye cheo kuanzia Kapteni, na chini yao kuwe na timu yenye mafunzo maalum ya uchunguzi wa rushwa na kesi za dhuluma za kijamii.
Wananchi waende moja kwa moja huko bila hofu ya kutishwa au kuchezewa shere.
Haki ya raia haipaswi kuamuliwa kwa mdomo wa kejeli au msimamo wa kisiasa. Tunahitaji mfumo ambao hautachelewesha, hautaogopa, na hautauzwa.
Kwa heshima yote ikiwa TAKUKURU haiwezi tena kutimiza majukumu yake kwa ufanisi, basi ni bora majukumu hayo yahamishewe JWTZ, ili haki ipatikane bila upendeleo wala hofu.

Pendekezo la mfumo mpya