Majungu na fitina dhidi ya Waziri wa Nishati nani yupo nyuma?

Ni fitna tu.....

Angalia hili.....

Wameeneza uongo kuwa mkurugenzi wa TPDC ndiye mwenye mamlaka ya kuisemea STOCK ya mafuta mbali kabisa na UHALISIA wa mhusika ambaye ni KAMISHNA WA PETROLI NA EWURA 🤣🤣🤣

Nchi ngumu hii ......
 
Chukua soda kwa Mangi mkuu, mimi nitalipa.
 
Tunamuomba Rais wetu Samia kamwe asikubali kuyumbishwa wala kubabishwa na makelele ya VYURA.
 
Kwani uongo??,Ni dhahiri shairi kuwa jamaa Wizara imemshinda,kila Siku umeme unakatika, Mbona enzi za Kalemani ishu hizo hazikuwepo??.
Ngoja atatimua Watendaji wa TANESCO WOTE wale wanao muhujumu wanafahamika.
siku zao zinahesabika.
 

Mwambie afanye hivi ahakikishe umeme haukatiki kwenye utawala wake, unaunganishwa na kuwafikia vijiji, miji yote kwa bei nafuu.

Huyu ambaye aliiba mitihani akatimuliwa, kwenye wizara ya mawasiliano akaleta sheria za kudhibiti vyombo vya habari, wizara ya mazingira ikamshinda.

Huyuhuyu aliyechukua zaidi bilioni moja NSSF kinyume na sheria, aliyeiba kura na mwenzake Nape Masaki uchaguzi wa 2015, kigogo wetu, aliyefanya campaign kubwa kuichafua serikali. Hafai kuongoza hata kijiji. Ale bata huko Masaki, wameiba vya kutosha.

Ukimuacha yote yatajirudia na pamoja na kuratibu kuua uchaguzi ujao, campaign ya fitina dhidi ya upinzani na yoyote potential na kubana zaidi mitandao.
 
Ndiyo kakutuma uje kumtetea kijinga namna hii!!

1. Unakumbuka alimwita katibu mkuu wake aende ofcn kwake kujieliza kwamba ni kwa nini ametoa taarifa ya uongo kwamba kuna upungufu wa maji katika mabwawa ya umeme. Je hiyo taarifa ya katibu ilikuwa ni ya uongo?

2. Unakumbuka alitwit kwamba tatizo la umeme linalojitokeza sasa ni kwa sababu ya ubovu wa mitambo. Kwamba awamu ya 5 mafundi waliogopa kuzima mitambo ya umeme ili kuifanyia matengezo kwa kuhofia kutumbuliwa. Je ni kweli kwamba tatizo lililopo la umeme chanzo ni ubovu wa mitambo?

Ukipata majibu ya maswali hayo utaacha tabia ya kijipendekeza kijinga. Na kama wewe ni ME wazazi wako wana hasala.
 
mimi huwa situmwi na wala hakuna wa kunituma, pia huwa singoji kutumwa bali najituma mwenyewe kama mzalendo kwa Nchi yangu na kwa viongozi wangu.

Nikiwa Mkiristu safi nafundishwa ktk Biblia kutii Mamlaka.

Sipendi kuona viongozi wakichafuliwa bila sababu zaidi ya chuki binafsi.

Hayo mambo ya kiutawala wa ndani siwezi kuyajua.
kila ofisi ina utaratibu wake wa kutoa habari.

Tuache kumchafua Makamba kwa chuki binafsi na dhana zisizo za msingi, tumuache achape kazi, kama kuna tatizo tumshauri kwa masilahi ya Nchi.
 
Kwa kweli yatawashinda mahasidi wote wanaomsakama Januari!

Watatahayari!
 
Hofu ya kukubalika kama rais mtarajiwa.
 
Wewe #Matola mleta mada ni nani yuko NYUMA YAKO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…