Aliyekuambia wachaga sio wachawi ni nani. Kwani kutambika na kutoa sadaka za damu za mbuzi kuku na ngombe.. kumwaga ulezi na maziwa kupeana kwa mizimu ya mababu wiokufa zamani kila mwisho wa mwaka kuna tofauti gani na uchawi. Tena bora uchawi mwingine lakini sio huo wa kutambikia mizimu. Ndio maana wanafanikiwa sana kibiashara na huwezi kushindana na mchaga maana huo uchawi wa kafara za wanyama na watu ni mkali kupitiliza asikwambie mtu. Otherwise uwe mtu wa maombi sana ndio utampiku mchagga anayetumia nguvu za MIZIMU kwenye biashara au kazi yake.... me ni mchaga nakwambia uhalisia ninaoujua..
Kwenye ukweli tukiri tu. Labda kama matambiko na uchawi vikae katika vikapu tofauti.
Mfano ukuriani, wale wanaoitwa wazee wa kimila wana technoloji za kienyeji zinatisha, wakiamua kutumia kumuadhibu mtu. Ni kabila langu japo, kwa sababu flani flani siiwezi lugha.
Lakini nimekaa na kusikiliza na kuona baadhi ya mambo.
Kuna kijana aliwahi kuwavaa wazee wa kimila katika kikao, huwa wakati mwingine wanakaa kwa kupeana migongo wakati maongezi yaliendelea akawatukana sana.
Wale wazee kuna siku wakamfuata mkuu wa kituo cha polisi wakamwambia kuna tembo atakuja hapa ndani ya wiki hii, msihangaike nae, ataondoka mwenyewe akimaliza kazi yake. Mkuu akaona kama jokes tu.
Kweli baada ya siku kadhaa mchana kweupe akatokea tembo na eneo sio hata karibu na mbuga, ajabu yule kijana akawa anamkimbiza tembo na fimbo, imagine fimbo!!!🤔.
Tembo akamaliza kazi yake(akamuua), kuchikichia maporini.