Makabila haya, yanaweza kuwa na makando kando mengine lakini suala la uchawi ni nadra kwao

Maisha yakabana mpaka basi. Nikamuambia mzee naomba kama kuna tambiko tufanye mimi hali ni mbaya akaniuliza ni lini katika kijiji chetu umewahi sikia kuna tambiko nikajibu sijawahi akaendelea kama hujawahi ndiyo ujue hayo mambo hakuna.
kabila lenu halina koo za kichifu
 
Kwenye ukweli tukiri tu. Labda kama matambiko na uchawi vikae katika vikapu tofauti.

Mfano ukuriani, wale wanaoitwa wazee wa kimila wana technoloji za kienyeji zinatisha, wakiamua kutumia kumuadhibu mtu. Ni kabila langu japo, kwa sababu flani flani siiwezi lugha.

Lakini nimekaa na kusikiliza na kuona baadhi ya mambo.

Kuna kijana aliwahi kuwavaa wazee wa kimila katika kikao, huwa wakati mwingine wanakaa kwa kupeana migongo wakati maongezi yaliendelea akawatukana sana.

Wale wazee kuna siku wakamfuata mkuu wa kituo cha polisi wakamwambia kuna tembo atakuja hapa ndani ya wiki hii, msihangaike nae, ataondoka mwenyewe akimaliza kazi yake. Mkuu akaona kama jokes tu.

Kweli baada ya siku kadhaa mchana kweupe akatokea tembo na eneo sio hata karibu na mbuga, ajabu yule kijana akawa anamkimbiza tembo na fimbo, imagine fimbo!!!🤔.

Tembo akamaliza kazi yake(akamuua), kuchikichia maporini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…