TusubiriWanajukwaa amani kwenu.
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza ningependa kufahamu maisha halisi ya kabila la Wakurya, mila na desturi zao. Bila shaka Wakurya wapo humu na ningependa kujifunza namna walivyo kama nilivyotangulia kusema hapo awali.
Karibu tuelimishane.
Mimi naulizia mila na desturi zao, kuhusu mazuri na mabaya ni tafsiri ya pande moja moja tu kwa sababu kibaya kwako kinaweza kuwa kizuri kwa mwenzako.Tusubiri
Mazuri yote yatasemwa na wao wenyewe wakurya
Yale mabaya ya wakurya yatasemwa na wasio wakurya
Waiting [emoji63] [emoji63] [emoji63] [emoji63]
Eti kama hujanipiga hunipendi!
Huu Uchizi huu!
Tiririka tu tufahamu mila nzima sio hilo tu.Eti kama hujanipiga hunipendi!
Huu Uchizi huu!
Mkuu kama unawafahamu elezea kwa urefu ueleweke.Open school unakijua kichuri? Google hio ndio mboga yao maarufu sana.(jiandae kuila)
Mkuu kuhusu ukakamavu na ujasiri nimeona wakurya wengi wanao hasa vijana na pia wanapenda kujiweka fiti, vipi kuhusu hiyo mila ya kuoa mabinamu ni mila ya kabila zima au ni baadhi ya koo zao tu?Wakurya hulelewa ktk mazingira/malezi ya kuwafanya wahimili kufanya kazi kwenye mazingira magumu eg. Jeshi n.k, wakurya ni wakarimu, wakurya wengi wanajua kuwa wizi ni njia halali ya kupata kipato(japo siyo wote), wakurya ni watafutaji wa mali ndiyo maana wametapakaa mijini na kila sehemu, wakurya ni jasiri bila kujali jinsia yao labda kama amekulia mjini, wakurya wanaongoza kwa kulima bangi huku wakisema kuwa ni dawa, wanakeketa na kutahiri wanaume, wanaoa wanawake wengi japo siyo wote, wanaoa binamu wa shangazi na mjomba ila siyo wa mama mdogo, wanauwezo mkubwa wa kurusha mishale kwa shabaha, pia ni wawindaji ktk mapori madogo na makubwa, wanapenda kumiliki silaha kwa ajili ya kujilinda au kuibia (kwa mfano: MWITA CHACHA MARWA,huyu alikuwa mwanajeshi aliyepigana VITA YA UGANDA lakini alichokifanya Tarime baada ya vita,imebakia stori).
Kwa kutandika viboko nayo ni srhemu ya kudumisha mila na desturi?Ukikosea jiandae kutandikwa viboko vikali sana vya makalioni mbele ya wanakijiji au wakazi wa mtaa husika.
ni koo zote, ila bnamu wa mama mdogo hawaruhusu kuoa.Mkuu kuhusu ukakamavu na ujasiri nimeona wakurya wengi wanao hasa vijana na pia wanapenda kujiweka fiti, vipi kuhusu hiyo mila ya kuoa mabinamu ni mila ya kabila zima au ni baadhi ya koo zao tu?
Kwahiyo ni ruksa kuoa mtoto wa mjomba wako?ni koo zote, ila bnamu wa mama mdogo hawaruhusu kuoa.
ndiyo kama amekukubali unaoa tu.Kwahiyo ni ruksa kuoa mtoto wa mjomba wako?
Ni kabila zima na pia naona hata kwa Waruri, Wajita, Wakwaya, Wahacha,Wasweta,Wasurwa, Wasimbiti n.k pia hufanya hivyo na nami nawaunga mkono kwa kuwa ni jambo jema.Mkuu kuhusu ukakamavu na ujasiri nimeona wakurya wengi wanao hasa vijana na pia wanapenda kujiweka fiti, vipi kuhusu hiyo mila ya kuoa mabinamu ni mila ya kabila zima au ni baadhi ya koo zao tu?
Ndio kwa sababu yule ni dada/kaka yako!. Yaani unaruhusiwa kuoa wa Dada kwa Mjomba.ni koo zote, ila bnamu wa mama mdogo hawaruhusu kuoa.