Source plz??? I have never heard some of the tribes mentioned, like those in red. Some of the mentioned tribes are not tribes as such but clans within a tribe. Some of the mentioned are "extinct", i.e. they have integrated themselves into bigger ones.
WaAlagwa, kabila ili linapatikana wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma, ila wengi kwa sasa wameingiliana na Sandawe
WaAkiek au
WaOgiek, wanaishi kati ya Tanzania na Kenya, na Lugha yao ni
moribund. Ila wengi wao kwa sasa wanaongea Kimaasai
WaAssa wamemezwa na Wamaasai waishio kaskazini ya Tanzania. Kwa sasa wapo wachache sana na wamemezwa na kabila la Kimaasai, ukiwaona wanataka kufanana na kabila la Wadorobo (Wandorobo).
WaDatooga, kwa jina lingine wanajulikana kama
Wamang'ati. Wanapatikana kusini mwa bonde la Ngorongoro. Kuna makabila ambayo wanafanana nayo, au matawi yenye kushabihiana.
Wabajuta
Wagisamjanga (Kisamajeng, Gisamjang)
Wabarabayiiga (Barabaig, Barabayga, Barabaik, Barbaig)
Watsimajeega (Isimijeega)
Warootigaanga (Rotigenga, Rotigeenga)
Waburaadiiga (Buradiga, Bureadiga), ndio hao Watindiga.
Wabianjiida (Biyanjiida, Utatu)
WaDhaiso, au WaDaiso, ni kabila lililoko kwenye Milima ya Usambara katika Wilaya ya Muheza wa Mkoa wa Tanga katika kaskazini mashariki mwa Tanzania. WaDhaiso wana mahusiano ya karibu sana na WaSegeju.
WaGorowa, wanapatikana Dodoma na Mkoa wa Manyara. (Cushitic language )
WaJiji, kabila linalopatika Ujiji Kigoma. Ila wanawekwa kundi moja na WaHa.
Wakisankasa, wanapatikana Kaskazini mwa Tanzania. Wakati mwingine wanafananishwa au kuwekwa kundi moja na Wandorobo.
NB:
Hayo yote ni makabila mkuu, haijalishi ukubwa au udogo wao, kila kabila lina haki ya kutambuliwa uwepo wake, hata kama wamemezwa na makabila makubwa.
Kila kabila hapo juu, kuna link ambayo inaweza kukusaidia kupata maelezo zaidi.