Hii Magamba Secondary imenifurahisha sana jina lake. Lina uhusiano wowote na wale wenzetu waliojivua magamba? Lol!Magamba Secondary (sasa ni University College ya chuo cha Tumaini kwa jina la SEKUCO)
umetaja wachaga suburi RIWA aje hapa...
Inaelekea hayo makabila uliyoyataja ndo yamebahatika kutoka na kuish nje ya tz kwa wingi klk makabila mengine
Inaelekea hayo makabila ya kaskazin yanakupa headache sana kwa jinsi watu wake walivokamua shule eeh?
Mimi mwenyewe wa Kaskazini, ila tu nimejaribu kufikiria kama kweli inaingia akilini kutangaza kwa redio za bongo (hata pasipo kwenda shule) eti ujumbe utafika Moscow.
Wachaga bana kweli hawaishiwi vituko
huku bado ni afrika, msiba ni janga la jamii nzima, tungeweza kuandika barua pepe ni sawa, ila utawaandikia wangapi wanaohusika? kutaja ndugu na mahala walipo ni muhimu, mfano akina fred swai wapo wengi sana, sasa ili ueleweke na kuondoa mkanganyiko ni lazima useme fred swai wa nelspruit, afrika kusini, ili fred swai wa tra asije akadhani ni yeye, au rafiki yake fred swai wa crdb bank, au yule wa edinburgh asije akasikia tangazo akadhani rafikiye amefiwa bure na kuanza kumtex meseji za pole na r.i.p, sijui nimeeleweka?