HAYA HAPA MAMBO MAKUBWA MATATU NILIYOJIFUNZA KWENYE NDOA.
Nina almost miaka miwili kwenye ndoa, kuna mengi nimejifunza ambayo ni mazuri, na yenye kufurahisha.
Mtu anaweza kusema miaka miwili ya ndoa? basi bado ni changa, sikatai ni kweli, lakini mbona kuna watu ndoa zao hazijapitisha hata miezi sita 😂.
Anyways, huku kwenye ndoa kuna mambo mengi mazuri nimejifunza ila leo ntaongea matatu tu kama ifuatavyo:
✅ Upendo – Mapenzi si maneno matamu tu, ni actions ndogo ndogo kama vile kumpa maji ya kunywa, , kumbeba simu yake akiwa anaitafuta, kupeana pole kunapokua na changamoto, kuelekezana na kushikana pale ambapo mnaona kabisa hatuwezi kukubaliana kwenye jambo fulani.
✅ Kuvumiliana – Hii ni skill ya level ya mwisho! Kumvumilia mtu anapokasirika, Ama anapokuamsha mapema wakati wewe ni siku yako ya mapumziko 😂, wakati mwengine unaumwa mnalazimishana kula dawa kwa faida yenu binafsi lakini inakua ugomvi.
Hapa kwenye uvumilivu kuna funzo kubwa, uvumilivu hauendani na ubinafsi hata kidogo,
Binadamu tuna madhaifu mengi sana, So Inabidi uwe na moyo wa simba lakini roho ya kondoo ili kuweza kusonga mbele.
✅ Urafiki – Ukishajua mke/mume wako si tu mpenzi bali pia bestie wako, ndoa inakuwa tamu. For me hii ni pillar moja wapo ambayo pengine inaweza kuniweka kwenye ndoa mda mrefu na huyu wifi yenu. Its all started seven years back, from urafiki to uhusiano to ndoa, and its never gets better than that.
Bonus point, japo hii inawahusu wanaume tu. 👇
☑️ Majukumu - Ndoa ni majukumu, and wewe kama mwanaume unapaswa uyatimize kadri ya uwezo wako, kama bado wewe ni mchoyo, bado unajifikiria mwenyewe kwanza kabla ya wengine basi usiingie huku patakushinda. Ni sawa wewe kuvaa shati moja mwaka mzima ili familia ile na ipate mahitaji yote muhimu. kwenye ndoa mwanaume ni provider wa kila kitu, hakikisha haufeli katika hilo.
Vipi kuhusu CHANGAMOTO .....?
Mpaka sasa changamoto kubwa ninayokutana nayo ni kulazimishwa kuoga kila siku kabla ya kulala hata kama jioni nimerudi nimeoga.
Halafu pia, kwanini nilazimishwe kubadilisha boxer kila siku wakati sijatoka hata jasho kutwa nzima? huu sio uonevu wazee?
Pia nikitumia kitu lazima nirudishe mahala pake hata kama ntakitumia tena soon 😂.
Kuna mengi sana kwenye ndoa lakini mwisho wa siku, ndoa ni safari ya kucheka pamoja, kusaidiana, na kupambana na maisha kama team.
Kuna jamaa mmoja wakati anasoma hii post hapo anajisemea kimoyo moyo kwa hasira
"MTAACHANA TU"
😂😂😂
NB: C & P