Makaburu warejeshewe usukani wa utawala wa Afrika Kusini?

Makaburu warejeshewe usukani wa utawala wa Afrika Kusini?

Makaburu ndio wanaiongoza ile Nchi, wameshikilia uchumi wa S.A. Wao ndio wanaamua nani awe Rais.
 
South Africa imetumbukia 'into chaos' kwa kupuuza sekta za huduma ndogo ndogo ambazo kimsingi ndizo zinaajiri watu wengi kama vile boda boda, mama lishe, ufundi, kilimo, kazi za ndani nk.
Mkuu, kwani South Africa ina upungufu wa ajira? Mbona huko kumejazana watu wengi kutoka Mataifa mbalimbali wakiwemo Watanzania wakifanya kazi?

Kwa sababu Tanzania imeikumbatia sekta ya huduma "ndogo ndogo", imeweza kutafuta tatizo la ajira?
 
Mkuu, kwani South Africa ina upungufu wa ajira? M ona huko kumejazana watu wengi kutoka Mataifa mbalimbali wakiwemo Watanzania wakifanya kazi?

Kwa sababu Tanzania imeikumbatia sekta ya huduma "ndogo ndogo", imeweza kutafuta tatizo la ajira?
Not really. Their currency is overvalued as well.
They are beaten on export markets due to that.
 
Tungechelewa kidogo .....nchi ingejengwa sana hii....kulokuwa mpango reli toka dar mtwara ruvuma hadi Mbeya....ring road za maana nyingi kuzunguka nchi yote......
Suluhisho ni moja tu wote tujiue commit suicide tuwaachie CCM nchi yao waaendelee kutawala.
 
Je, vyombo vya ulinzi na usalama,vimewatenga wazungu? Kama na wao wamo,basi haimaanishi kwamba wazungu wakipewa hali hiyo itaisha
 
Hakuna nchi ya sisi pumbavu weusi ambayo ipo salama.
Hawa wanaoitwa wasomi ndio watafanikisha whites kututawala tena black Afrikan.
Wamekuwa ni hatari zaidi ya wakoloni weupe.
 
Je, vyombo vya ulinzi na usalama,vimewatenga wazungu? Kama na wao wamo,basi haimaanishi kwamba wazungu wakipewa hali hiyo itaisha
Uongozi ndiyo huamua mustakabali wa kila kitu. Kama dereva aliyekalia usukani ni "mbovu", anaweza kusababisha ajali hata kama abiria wake wote ni madereva wabobevu.
 
Ingawa Afrika Kusini ni mojawapo ya nchi zilizoendelea duniani, inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa usalama. Mara kadhaa kumesharipotiwa na vyombo vya habari juu ya matukio ya kihalifu katika majiji makubwa kama Johannesburg, n.k.

Sina uhakika kama matatizo kama hayo yalikuwepo pia kipindi cha utawala wa Wazungu. Hisia zangu zinanishawishi kuamini kuwa hata kama changamoto za kiulinzi zilikuwepo, si kwa kiwango kama cha sasa.

Kwa kuwa hali ya mahali hutoa taswira ya aina ya uongozi uliopo, hakuna namna itakosekana kuuhusisha utawala wa sasa ambao kimsingi ni wa weusi, na hali hiyo. Pengine, utawala uliopo umeshindwa kukabiliana ipasavyo na hiyo changamoto.

Unafikiri, Makaburu wangerudishiwa usukani wa utawala wa South Africa kungeweza kuleta mabadiliko chanya kiuchumi, kisiasa na kiusalama?
Kasome kuhusu apartheid kisha ndiyo uje na mada kama hizi
 
Yaani unamaanisha Apartheid Policy irudi humo Azania?

Weusi waishi kama mateka wa kivita huku wakibaguliwa kila sekta ikiwemo kutengewa barabara zao, madarasa, na mabasi yao?

Chura anapenda maji lakini siyo ya moto
 
Hata Tanganyika apewe muingereza
Hapana mkuu! Waingereza si Watanzania. Lakini Makaburu ni Waafrika Kusini kama ilivyo kwa Wazulu. Sisi tunachoweza kufanya ni kuwapa haki sawa wote wanaoishi Tanganyika bila kujali ngozi yake. Na kama kuna Muingereza anapenda kuja kuishi Tanganyika, tutamkariabisha kwa mikono miwili na kumpa uraia.
 
Yaani unamaanisha Apartheid Policy irudi humo Azania?

Weusi waishi kama mateka wa kivita huku wakibaguliwa kila sekta ikiwemo kutengewa barabara zao, madarasa, na mabasi yao?

Chura anapenda maji lakini siyo ya moto
Big NOOO!

Suala la apartheid lilikuwa zama zile. Kwa sasa haliwezekani.

Ubaguzi wa rangi haukuanzia South Afrika, ulikuwepo hata Marekani. Lakini Marekani ilishaondokana na hilo tatizo kwa sehemu kubwa sana, ndiyo maana imeshaongozwa na mtu mwenye asili ya Afrika. Hata Afrika Kusini si rahisi hilo kurejea.

Katiba ya South Afrika ipo imara. Ikitokea Mzungu akapewa fursa ya kuiongoza, hatafanya hivyo kwa presidential decree, bali kwa mujibu wa Katiba ya South Africa. Katiba haitamruhusu kuurejesha huo uovu.
 
Hakuna nchi ya sisi pumbavu weusi ambayo ipo salama.
Hawa wanaoitwa wasomi ndio watafanikisha whites kututawala tena black Afrikan.
Wamekuwa ni hatari zaidi ya wakoloni weupe.
Mbona hasira hivyo mkuu?

Nimeiosoma comment yako zaidi ya mara moja! Nimebaki najiuliza "nini kimemkwaza huyu kiongozi?"
 
Mkuu, kwa ulimwengu huu wa utandawazi, unaweza ukawa na umri wa miaka kumi na tano lakini ukawa unafahamu kwa undani maisha ya watu walioishi miaka elfu mbili iliyopita kama vile ulikuwa ukiishi nao.

Makaburu ninewajua "majuzi" tu kupitia vitabu.

Kwani una mashaka na vitabu mkuu?
Hata miaka ya 90 hakuna alie muona kaburu.Zilikuwa stori za kusikia kwenye redio na TV na movie ya SARAFINA. Labda kama aliishi SA.
Unaweza ukawa umewajua vizuri kuliko sisi tuliosikia tu na kusoma historia ya apartheid kama wewe.Asikutishe.
 
Back
Top Bottom