Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Baadhi ya makada na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka mikoa mbalimbali, ikiwamo Dar es Salaam wamejipanga leo Desemba 18, 2024 kwenda nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, Mikocheni kumuomba agombee tena nafasi hiyo.
Hadi sasa Mbowe hajaweka wazi kama atawania nafasi hiyo au la.
Mmoja wa waratibu wa mchakato wa kwenda kwa Mbowe aliyeomba jina lake lisitajwe ameieleza Mwananchi Digital kuwa wanajipanga kwenda kuonana na Mbowe nyumbani kwake.
"Tukio la kwanza kwenda nyumbani kwake leo saa tano asubuhi kumuomba agombee uenyekiti wa chama. Kutakuwa pia na viongozi mbalimbali wanaokwenda kumuomba Mbowe agombee tena uenyekiti, akikubali tutakwenda kumchukulia fomu makao makuu.
"Kwa sasa hatujaona mtu mwenye sifa ya kuwa kiongozi zaidi yake. Mbowe atasema atakubali kugombea au la, akikubali ataletewa fomu kwa ajili ya kuijaza," amesema.
Tayari Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu amechukua fomu kugombea nafasi hiyo.
Pia, Soma: CHADEMA watoa tamko zito, John Mnyika aanika gharama za fomu za kugombea na kutoa mwongozo